Nahisi kuna ka movement cha wafanyabiashara na mabeberu wanaotaka kuirudisha covid 19 kwa kasi ili wapige hela.

SIO KWA TANZANIA YA LEO, WATAKWAMA
Kwa hiyo WHO inashirikiana nao?
 
Kuna rafiki yangu yupo Morogoro amenipigia simu leo kuniambia kuwa Corona ipo nichukue tahadhari.

Mtaani kwao modeko wamezika mtu alikuwa na dalili zote za Corona alipokuwa hai.
Wajinga wanasema eti ili ujue korona ipo badi umjue na jirani aliyefariki kwa korona.
Watu wakijielimisha vizuri abc za korona ni rshisi kujua kama ipo au haipo.
Sio lazima kila aliyepata maambukizi augue, awe mahututi, au afe.
Mtaa mmoja kunaweza kuwe na watu kimi walioambukizwa lakini asilazwe au asife mtu.
So tunapaswa pia kujifunza kuishi nayo na tusiwe tu wajinga kusema ipo, haipo
 
Aliyetuita sisi wa afrika MASOKWE wala hakukosea.
Tuna ufahamu mdogo sana
 
Ana haki ya kusema hivyo sababu hakuna vipimo vya corona hospitali nyingi
 
Usifanye utani aisee ninapofanyia kazi wenzangu wawili ndugu zao wamefariki kwa dalili zote za ilo tatizo, shida ni kwamba vipimo havipo kwenye hospitali nyingi pia ni ghali,by the way siku utakayoamini corona ipo ni siku itakapogusa familia yako
 
Hebu niongee moja kwa moja tuelewane

Kwanza achana na hicho kichwa cha habari

Tunalaumu sana, na kulalamika na ni sahihi kabisa maana ni haki yetu

Binafsi sifurahishwi na utaratibu wa serikali kushindwa kutuweza wazi kila kitu mimi sipendi siri inatucost sana
Kuna mambo mawili hapa

Nyie mnaoilaumu serikali, tuelezee ninini mnataka kifanyike kumaliza tatizo la covid?toeni solution...

Na nyie mnaounga mkono kila kitu tupenu solution ya tatizo maana sasa dunia ipo kwenye mkondo wa chanjo, hata mkikata saahv ni suala la muda tu miaka michache ijayo chanjo hii hii itakuja kuwa ni lazima na tutachanjwa tu mgomo wa mpito tu huu

Sasa kila mtu akae upande wake mnaopinga serikali jinsi inavyodeal na covid toeni suluhisho nini kifanyike na nyie mnaosapoti serikali toeni mikakati yenu ambayo mnaamini itamaliza hili tatizo permanently


Tukate mzizi wa fitina sasa
 
Ihamasishe kila mtu achukue tahadhari ya kujilinda yeye mwenyewe na kuwalinda wengine, ni hilo tuu. Sasa hivi msaramgambo kuna wanaouchukua tahadhari na wengine wanapuuza hivyo kuhatarisha wengine
 
Wawaachie wataalam wa afya watoe elimu juu ya ugonjwa ,dalili zake ,jinsi ya kujikinga ndio iwe msisitizo na matibabu yake .Kuna watu wanakufa kizembe sana bila kujua kwani muda anaopelekwa hospital tayari mapafu yamekuwa kama ya mvuta sugar na sometimes nothing they can do kwa hiyo stage.Elimu ikiwa ni kuhalikisha wananawa mikono ,wanachukua tahadhari wakiwa na suspected case etc
 
Umeongea point sana mkuu
 
Mara corona ipo mara haipo ni uzushi tu wa mitandaoni, mara chanjo ni feki, mara tutumie dawa za mitishamba, mara tujikinge tusifanye mchezo, mara Mungu ashatuokoa tusiogope...sasa tushike lipi??? Mnatuchanganya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…