Ila wabongo ni wabishi mnoo..... Sasa kama dunia nzima kuna corona kipi cha ajabu TZ ikiwepo? Kwani sisi ni special sana kuliko mataifa mengine au tumefunga mipaka kwamba hawawezi kuteletea?

Na ndio maana mtoa mada kasema kwakuwa kuna doubts ni vzuri serikali either ikanushe au ikubali ili watu wachukue hatua stahiki. It's that simple kuliko kukaa kimya wakati rumours za second wave zipo kitaani
 
MAISHA YAKO NI JUKUMU LAKO, USINGOJE KUAMBIWA.
WHOSE LIFE IS IT ANYWAY.
 
Umeandika maelezo mengi ila nimekuelewa kidogo lengo lako,
Sasa unataka uelezwe kuhusu corona je umeomba kujuabna kuhusu mareria au ugonjwa wa moyo au kansa?
Kama hujauliza hayo mengine kwa nini uhangaike na corona wakati kuna hayo magonjwa pia ni hatati kuzidi corona?
Kuweka ndoo za maji na kuvaa barakoa hakujapigwa marufuku je wewe unavifanya hivyo kwa ajiri ya afya yako au mpaka urazimishwe?

Ukipenda corona iwepo ugua uone kama hutapata huduma.
 
Umeandika point tupu
 
Usiwe mbinafsi, wakati wewe una uelewa kuhusu Korona, linganisha na Watanzania wenzako ambao uwezo wa ufahamu wa haya mambo ni mdogo!
Inahitajika intervention ya serikali kuwaweka aware wananchi wanaoamini kuwa corona haipo waelewe hali halisi ili wachukue hatua!
 
Hapo mkuu, umetuacha kwenye mataa! Swali ni,je,ulipima COVID-19 au hapana?

Niliwahi kusoma chapisho fulani la kitabibu ambapo madkitari wa kichina walisema wakati mwingine tumbo kuchafuka na kuharisha, kushikwa homa na kikoozi kijavu na wakati mwingine macho kuwa mekundu ni dalili za corona.

Tuchukue tahadhali ugonjwa huu haukuhama nchi by 100%.
 
Wewe kama huna imani ya kumwamini Mungu kuwa aliiponya nchi,nenda kakae wanakovaa barakoa,sisi tuachie Magufuli wetu na imani yetu.
haya maneno ulitakiwa umwambie Lissu alipokuwa akijaza watu yeye mwenyewe bila kuvaa barakoa.
 
Mkuu umehesabu hadi vifo vya ajali nini?maana mwisho mwa mwaka ajali nyingi.
Endelee ni tu Kuamini na Kuaminishwa kuwa Deportivo la Corona haipo nchini Tanzania, ila tunaoishi na Madaktari 24/7 tunajua nini Kinaendelea.
 
Mungu yupo .....apige moja takatifu wale top 5 cpwaa tupumzike
 
Serikali inafanya nini katika janga hili mkuu? Huoni iko kimya garama za kipimo cha Corona ili uende nje ya nchi zimepanda?
 
Issue sio Tz kuwa na corona au kwamba napinga kuwa Tz hakuwezi kuwa na corona. Kama dunia nzima kuna corona sio sababu ya mtu kuja humu na kusema Tz watu wanakufa sana na corona bila ushahidi,mtu hajui sababu ya kifo cha mtu ila anakimbilia kusema kuna mtu kafa na dalili kama za corona mara sijui kawekewa mashine ya kusaidia kupumua,vifo vya watu maarufu hivi karibuni vimekuwa vinahusishwa moja kwa moja corona.

Sasa hayo mambo ndio naona si sawa hata kama serikali ingekuwa imetangaza kuwa kuna corona bado hayo mambo yasingekuwa na uhalali kuyafanya. Kinachofanyika hapa ni kama inatumika nguvu kuwatisha watu na corona.
 
Endelee ni tu Kuamini na Kuaminishwa kuwa Deportivo la Corona haipo nchini Tanzania, ila tunaoishi na Madaktari 24/7 tunajua nini Kinaendelea.
Kama unajua ni nini kinaendelea ndio ueleze humu watu nao waelewe na sio kutaka kuwaaminisha watu vitu kisa unaishi na madaktari utakuwa huna tofauti na waliyowaaminisha watu kuwa hakuna corona.

Kabla ya kuwepo corona tunajua mwisho wa mwaka huwa kuna ajali nyingi hutokea na husababisha vifo,sasa wewe unakuja kusema tu vifo vimeongezeka bila kueleza kwa kina wakati unajua kuna vifo vya ajali pia ambavyo havihusiani na maradhi ya corona.
 
Watu kutokuchukua hatua inaonyesha kiwango cha elimu walichonacho kwa kuamini koona inagopa mipaka ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…