Kwa kweli lazima nikiri kuwa mimi mmoja wa wana JF tuliomshambulia sana Rais wetu juu ya msimamo wake juu ya covid19.
Lakini leo nimetiwa imani kuwa Rais Magufuli.
Hili la kuliweka hadharani kuwa covid ipo, na tujikinge, na kuwa serikali haikuzuia watu kuvaa barakoa.
Hayo ni mambo ya msingi kabisa.
Hiyo ni kukubali kuwa licha ya kupungua maambukizi mwaka jana, wimbi la maambukizi sasa ni kali na limeshaua watu wengi ikiwemo viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla.
Tamko la Rais KANISANI pale St Peter Msasani ni pamoja na kukiri ukweli wa hali halisi.
Kwa hilo nampongeza sana.
Tulifika mahali si pazuri, pale hata viongozi wa dini, tunaofikiri wako karibu zaidi na upako wa Mungu, wakipinga msimamo wa serikali hadharani, hususan kuvaa au kutovaa barakoa.
Wanasayansi wetu na madaktari bingwa vile vile wapewe heshima yao na kuja na mikakati ya Public Health jinsi ya KUZUIA ugonjwa huu wa civid katika mazingira tuliyomo. Kuvaa barakoa ni mojawapo.
Na hizo barakoa za kutoka nje zenye matatizo, je wataalam wetu wako wapi kuzichunguza na kuja na suluhisho?
Zaidi ya yote, ugonjwa wa covid lazima kupambana nao kisayansi kugundua strain, maambukizi concentration na jinsi ya kuzuia.
Kwa hatua ya leo namuunga mkono Rais Magufuli.