#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
IMG_8788.JPG
 
Ikiwa ziliundwa mechanisms nyingi za kuwezesha kunawa mikono kwa maji tiririka na kuwekwa kila kona, inakuwaje hadi sasa hakuna company yeyote iliyotathmiwa na kuona ingeweza kutengeneza barakoa za ubora wa kukubarika? Je hatuwezi kuwa na technolojia rafiki ya kutengeneza mitungi ya gesi ya oxygeni ili kusambazwa ktk maeneo yenye wagonjwa wengi wenye shida ya kupumua kama yale ya mijini? Au ni kuzarau tu?
 
Kwa kuwa umeweka na picha embu mwangalie Mhe utuambie Ni kitu gani alichonacho hapo ambacho si Cha kununua dukani (kuletewa kutoka kwa mabeberu?)...Anza miwani, nguo, Mike, kalamu nk. Ni kipi hakitoki kwa mzungu?!!! mswaki alotumia, Colgate, sabuni, Taulo nk. Hivi mzungu akitaka kutulisha sumu Ni mpaka atumie barakoa kweli?!!! Mtu mwenye uwezo wa kupeleka chombo Hadi sayari ya mars na anakiendesha kutokea huku duniani hivi mtu Kama huyo akiamua kutufanyizia umafia Ni Hadi atumie barakoa?!!

Msaidieni huyu mzee acheni uoga wa kulinda matumbo yenu, Ni maangamizi kwa Taifa. Ameshakiri kosa; si lazima atangaze mimbarini.
 
Vita vya kiuchumi ndio Nini hasa?

Ni ya pili duniani vivutio vya utalii tunahitaji wazungu waje ili tupate fedha.

Madini na gesi tunawabembeleza waje na mitaji na technolojia yao hatuna cha kufanyia

Tuna bahari hatuwezi hata kuvua tunahitaji watuuzie meli na hao samaki wakipatikana tutaomba EU waruhusu tuwahuzie!
Tuache kuaminishana vya hovyo.
 
Nimeona jamaa wakishauri kuwa "kwa kuwa Rais ana mwamini sana Mungu ndo maana haoni hata ya watu kuvaa barakoa basi imani ile ile aliyo nayo ndo atumie kukataa kuwa na walinzi maana yupo Mungu Mlinzi mkuu"

Ninyi watu mna nia gani? Kwenye suala la Ulinzi wa mwili hapo Mungu sidhani kama ataweza maana kama ingewezekana najua kwa imani aliyo nayo Rais angesema hata walinzi hataki amemwachia Mungu. Maana atakaye ikoa nafsi yake ataipoteza.

Mi nadhani tuungane naye kwa kuwa na imani katika suala la Corona tu Ulinzi mwingine huu....mmmh mmh...tusimjaribu. ila kwa suala la ulinzi dhidi ya Corona watanzania tusiwe na hofu. Hilo tuungane naye.tuwe na imani pia.
 
Kwa kweli lazima nikiri kuwa mimi mmoja wa wana JF tuliomshambulia sana Rais wetu juu ya msimamo wake juu ya covid19.

Lakini leo nimetiwa imani kuwa Rais Magufuli.

Hili la kuliweka hadharani kuwa covid ipo, na tujikinge, na kuwa serikali haikuzuia watu kuvaa barakoa.

Hayo ni mambo ya msingi kabisa.

Hiyo ni kukubali kuwa licha ya kupungua maambukizi mwaka jana, wimbi la maambukizi sasa ni kali na limeshaua watu wengi ikiwemo viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla.

Tamko la Rais KANISANI pale St Peter Msasani ni pamoja na kukiri ukweli wa hali halisi.
Kwa hilo nampongeza sana.

Tulifika mahali si pazuri, pale hata viongozi wa dini, tunaofikiri wako karibu zaidi na upako wa Mungu, wakipinga msimamo wa serikali hadharani, hususan kuvaa au kutovaa barakoa.

Wanasayansi wetu na madaktari bingwa vile vile wapewe heshima yao na kuja na mikakati ya Public Health jinsi ya KUZUIA ugonjwa huu wa civid katika mazingira tuliyomo. Kuvaa barakoa ni mojawapo.

Na hizo barakoa za kutoka nje zenye matatizo, je wataalam wetu wako wapi kuzichunguza na kuja na suluhisho?

Zaidi ya yote, ugonjwa wa covid lazima kupambana nao kisayansi kugundua strain, maambukizi concentration na jinsi ya kuzuia.

Kwa hatua ya leo namuunga mkono Rais Magufuli.
 
Vibaraka wa mabeberu hao, Wana hasira kali, wanamsagia meno lakini amewapa za uso: Huko wanakojua zaidi kuvaa barakoa na kufanya lockdown huko ndiko yametokea madhara makubwa kwa maana ya vifo na kiasi cha maambukizi kuliko kwetu tulioamua kumtanguliza Mungu mbele kwanza kabla ya tahadhari (siyo bila ya tahadhari).
 
Vibaraka wa mabeberu hao, Wana hasira kali, wanamsagia meno lakini amewapa za uso: Huko wanakojua zaidi kuvaa barakoa na kufanya lockdown huko ndiko yametokea madhara makubwa kwa maana ya vifo na kiasi cha maambukizi kuliko kwetu tulioamua kumtanguliza Mungu mbele kwanza kabla ya tahadhari ( siyo bila ya tahadhari).
Hivi umemwelewa mtoa Uzi? Au ndo nyie kila kitu kudandia.
 
... at relativistic speeds one 60 minute hour could shrink into a 30 minute hour making an earthly day a 48 hour day!
WE'RE ON THE RIGHT TRACK INDEED!
👊 😅✌️💥
 
Vibaraka wa mabeberu hao, Wana hasira kali, wanamsagia meno lakini amewapa za uso: Huko wanakojua zaidi kuvaa barakoa na kufanya lockdown huko ndiko yametokea madhara makubwa kwa maana ya vifo na kiasi cha maambukizi kuliko kwetu tulioamua kumtanguliza Mungu mbele kwanza kabla ya tahadhari ( siyo bila ya tahadhari).
Wewe data zako za maambukizi ziko wapi?

Msiwe wajinga wajinga!
 
Toka uchaguzi umalizike kichwa chake hakijakaa vizuri. Nahisi kuna mambo aliyatarajia baada ya kupukutisha wapinzani kwanguvu, kajikuta mpweke hana la kufanya.

Wasaidizi wake wapo kama bendera tu. Anajiona mpweke na anaongea vitu rahisi mno kwa hadhi yake ya urais. Uwepo wa upunzani ulikuwa unasaidia kupasha moto brain yake.
 
Back
Top Bottom