#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Niliwahi sema hivi hapa JF:

Gharama ya watu kupuuza siasa katika nchi si tu ni kubwa mno,bali hakuna hata tajiri anaeweza kuimudu.

Mkuu una hoja ya msingi sana.

Lazima tuwe na pa kuanzia. Suala la kutelekezewa gonjwa halina chama.

Hawa ni wa kuvaana nao head-on sasa.

Bottom line, hatukubali kutelekezewa gonjwa hali kodi wanachukua.
 
Nadhani muda wa kulalamika umeshakwisha sasa maana Jiwe hawezi kutoka hadharani na kuongea tena. Sasa hivi keshawaachia hiyo kazi kina Dorothy Gwajima

Tunapaswa sasa kuwa tunapost nini kifanyike tukionyesha na success stories kutoka kwingineko.

Msemaji wa Serikali (Dr. Abas) amesema Serikali haijawahi kukataa kwamba Corona ipo na akasema kwamba Serikali haitacopy blindly mbinu wanazotumia nchi nyingine
 
Niliwahi sema hivi hapa JF:

Gharama ya watu kupuuza siasa katika nchi si tu ni kubwa mno na hailipki kwa masikini na matajiri,bali hakuna hata tajiri anaeweza kuimudu.

Mfano, leo hii hata matajiri wakiwemo kina MO, wameonja adha ya siasa na wanasiasa baada ya kutekwa.

Na sasa changamoto ya upumuaji na madhara yake inayochangiwa na maamuzi mabovu ya wanasiasa wetu hata matajiri hawako salama.
... uko sahihi sana Mkuu. Siasa ndio kila kitu; ndio inatawala na kuamua mustakabali wa maisha yetu; wengi hatujui hilo tunaichukulia kimizaha sana. Twendeni tukajiandikishe tupige kura tuchague viongozi wanaofaa; visingizio kibao - niko safarini, sina muda, hayatuhusu sisi vijana, n.k.

Twendeni kwenye kampeni tukasikilize sera na kuwahoji wahusika; hatuna muda, mambo ya wazee. Wachache tuliojiandikisha twendeni tukapige kura - hatuna muda. Matokeo yake zaidi ya 25m wanaodaiwa kujiandikisha, waliopiga kura ni around 10m halafu leo tunalalamika. Pamoja na COVID-19, nchi nzima nyumba na mabanda yote yanapigwa chapa watu wote waanze kulipa kodi.
 
... uko sahihi sana Mkuu. Siasa ndio kila kitu; ndio inatawala na kuamua mustakabali wa maisha yetu; wengi hatujui hilo tunaichukulia kimizaha sana. Twendeni tukajiandikishe tupige kura tuchague viongozi wanaofaa; visingizio kibao - niko safarini, sina muda, hayatuhusu sisi vijana, n.k.

Twendeni kwenye kampeni tukasikilize sera na kuwahoji wahusika; hatuna muda, mambo ya wazee. Wachache tuliojiandikisha twendeni tukapige kura - hatuna muda. Matokeo yake zaidi ya 25m wanaodaiwa kujiandikisha, waliopiga kura ni around 10m halafu leo tunalalamika. Pamoja na COVID-19, nchi nzima nyumba na mabanda yote yanapigwa chapa watu wote waanze kulipa kodi.
Na uzuri wa hili la sasa la changamoto ya upumuaji madhara yake yanagusa hata wale wanaowalinda hao wanasiasa kwa mitutu ya bunduki,virungu, ving'ora na n.k.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huna haki ya kuishi kwa sababu wakati wahuni na mabumunda wanachukua nchi kwa njia za hila na za kihuni wewe uliishia kukenua meno!Sasa hivi ni wakati wako wewe kulipa uzembe uliofanya,na utalipa kupitia kifo.
 
Kwani kuna mtu kasema huna haki ya kuishi?

Mbona unvaongea kama umekatwa kichwa?

Tangulini akufukuzaye akakwambia Toka?

Yaliyomo humu ni kweli:


Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mjinga yeyote anamawazo kama yako, unapo aminisha watu hakuna tatizo unawafanya wasichukue tahadhari yeyote hivyo kama ilibidi wafe 10 basi watakufa 30 lakini ukiwapa tahadhari wangekufa 10 wengine wangepona kwa sababu wamechukua tahadhari

Hizo nchi unazo zisema yawezekana hivyo vifo kwao vimekuwa vichache kwa sababu ya tahadhari inayo endelea kutiliwa mkazo huenda kinyume na hapo ingekuwa mara tatu ya hivyo unavyo sikia

Pia wenzetu hawana ujinga ujinga wa kuficha ficha takwimu kwenye mambo sensitive , yawezekana tanzania tunakufa mara tatu ya wao ila ukweli unakwepeshwa kwa maslahi ya mtu mmoja pekee.
Yawezekana... Huenda...

hata wewe huna hakika ya hoja zako.

Kitu ambacho Magufuli hataki kukifanya Ni kutangaza hali ya hatari hivyo kudhibiti taharuki.

sasa kama yeye alishasema kuna corona ya ajabu ajabu imekuja. Akasisitiza watu wajikinge. MoH imetoa palative, unataka nini tena?
 
Yawezekana... Huenda...

hata wewe huna hakika ya hoja zako.

Kitu ambacho Magufuli hataki kukifanya Ni kutangaza hali ya hatari hivyo kudhibiti taharuki.

sasa kama yeye alishasema kuna corona ya ajabu ajabu imekuja. Akasisitiza watu wajikinge. MoH imetoa palative, unataka nini tena?
Ndio maana nikasema huo ni ujinga kwa sababu unafikiri upande mmoja na kuuacha mwingine

Yawezekana kweli hataki kuweka taharuki lakini hii inawafanya watu kuishi bila tahadhari hivyo kuzid kuongeza tatizo na litakapo kuja kulipuka hata kukabiliana nalo haitawezekana au itakuwa kwa gharama kubwa zaid na utaona bora wangeambiwa ili wachukue tahadhari tatizo lisiwe kubwa
 
Mkuu mie nakuelewa vizuri sana. Siangalii serikali katika negative pekee ( katika yale iliyo shindwa ), naangalia pia katika yale iliyoweza kuyafanya pia na yakawa na faida kwa jamii. Swala la afya nchi nyingi za africa zimekuwa nyuma, na zimekuwa zinategemea zaidi misaada katika sector ya afya hata katika janga la corona nchi nyingi hazina uwezo wa kukabiliana nalo wenyewe hadi pale ambapo wame wezeshwa misaada. Kwa nchi yetu imepata fund ya kutosha ?

Mkuu haihitaji funds kuifahamisha jamii kuwa kuna janga la ugonjwa huu, kuwa tahadhari kabla ya hatari inahitajika.

Haihitaji funds kuitaka jamii kuzingatia umuhimu wa kuvaa mabarakoa na kupunguza mikusanyiko inayoweza kudhibitiwa.

Haihitaji funds kutambua wananchi wanaolipa kodi wameathirika mno na janga hili kiasi cha badala ya kuona wanapunguziwa mzigo huo, wewe wawaongezea hata kwa kuleta kodi mpya sasa kama hizi za mazishi.

Upo mkuluro wa haihitaji funds ..

Au niendelee?
 
Huyu Lema atulie, akili za kuchanganua mambo hana.
Status yake ya ukimbizi haimruhusu kufanya siasa ngoja tutapelekea immigration Canada wamfutie ukimbizi kwa kukiuka masharti tunampa onyo la mwisho
 
Zaidi ya ubishi na ujinga sioni kama Lema ana kitu kingine kichwani

Arusha alikua ameigawa vibaya sana kikabila.
 
Badala ya kusubiri Serikali Kwanini sisi wananchi tusianze kuonyesha tunachohitaji? Kwanini wananchi tusijitolee kusaidia Hospitali ambazo tayari zipo uwezo wa kutoa huduma? Kwanini kila kitu tusubiri serikali?

Nini kinatakiwa kwenye hili la kupambana na huu ugonjwa kwa hapa tulipo ni moja tu na kila mtu analijua. Yaani mkiwamo wewe na hata serikali nzima:

"Kuwaachia wataalamu wa afya kushika hatamu za uongozi wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu ambao ni tatizo la kiafya wala si tatizo la kisiasa wala kiusalama kama mnavyotaka kuwa hadaa wengine."

Kuwataka wananchi kuchangia ni yale yale ya kutaka kuitafutia serikali uhalali wa kutowajibika katika wajibu wake ulio wa msingi zaidi.

Wakati wa serikali kurejesha kodi tunazolipa ni sasa kwa kutuhami na janga hili. Si wakati wa kuitisha michango na kodi zaidi kutoka kwetu?

Hivi mnaifahamu hali ya uchumi ya mnaodhani waendelee kuchangia na pia kulipa kodi zilizoboreshwa zaidi na zaidi?

Yale yale ya chako chako changu pia chako?

Kwanini miradi mikubwa kama hii ya ununuzi wa madege kwa cash, ma SGR, ma stiggler's gorge nk isisimamishwe kwanza kuikabili dharura hii?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nadhani muda wa kulalamika umeshakwisha sasa maana Jiwe hawezi kutoka hadharani na kuongea tena. Sasa hivi keshawaachia hiyo kazi kina Dorothy Gwajima

Tunapaswa sasa kuwa tunapost nini kifanyike tukionyesha na success stories kutoka kwingineko.

Msemaji wa Serikali (Dr. Abas) amesema Serikali haijawahi kukataa kwamba Corona ipo na akasema kwamba Serikali haitacopy blindly mbinu wanazotumia nchi nyingine

Kwamba serikali haita copy blindly mbinu wanazotumia nchi nyingine ndiyo kusema je jombi?

Mbinu zipi basi wanazotumia takribani mwaka sasa tangu janga hili kuingia nchini?

Au ni hii kuwaongezea wananchi mzigo wa kodi na kuwatelekeza walio hatarini kujifia kibudu yaani wa kufa na wafe wa kupona na wapone?

Hizo ndizo unazoziita kuwa ni mbinu?
 
Mbona rumours has it yule Waziri wa mambo ya Nje wa China alikuja na madaktari wao na chanjo kwaajili ya top layer.
Wapinzani wa Magufuli kwa maneno ya kanga amjambo, Waziri mwenyewe alikuwa amevaa baracoa masaa 24 amekuja kuvua baada ya kuona kwa Magufuli na cabinets yake baracoa sio insue,kama chanjo inazuia corona mbona wanaendelea kuvaa baracoa na kujifungia ndani.Magufuri ni mwanaume wa shoka atishiki kwa maneno,anajua kufa kupo tu akuna mwanadamu awezae kukikimbia kifo kikija
 
Mungu mbariki Lema
Lema awezi pata baraka, maana kajipereka utumwani mwenyewe na kizazi chake,hiyo raana ya kujifanya mkimbizi ili apate msaada itamtafuna yeye na kizazi chake chote mpaka kizazi cha nne.Mwaume akimbii matatizo anakabiliana nayo.
 
Back
Top Bottom