#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
'Mamlaka' inasema hiyo kitu haipo macho makavuuuu,
mimi ni nani niseme vinginevyo?
wewe nani unipinge?
Sikuelewi ujue.
Kikwete alishawai ongea kwamba "za kumbiwa changanya na zako"
Hivyo hata serikali ikisema hakuna ugonjwa, wewe watakiwa kujiongeza kwa kuthibitisha.
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.

Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.

Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.

Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.

Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna hiyo kwa serikali sio sawa.
Sisi raia tumemwajir rais. Anawatendaji na vitendeakazi vyote vinavyohitajika. Anapaswa aongoze taifa kwa nuia iliyo sahihi. Unataka tutoe ushauri gani? Mimi kwa mfano sio daktari, sio mchumi lakini ni mlipa kodi. Nikiona vifo vinavyotokea na magonjwa yanayosumbua jamii nina haki ya kuhoji na kupewa majibu sahihi toka kwa serikali ambayo ndio yenye wajibu wa kudhibiti hali hiyo.
 
Katika hizo hoja zako naungana nawe kabisa, kuna haja serikali kutoa kauli kuhusu mustakabali wa wananchi na huu ugonjwa
Mimi nasema kipimo cha korona kiwe bure, na takwimu zitolewe mbona za ukimwi na marelia tunapewa takwimu why korona tunaogopa kutoa?
 
We mjomba umeeleza watu wametoa ushauri na waendelee kutoa ushauri, huo uliotolewa awali umefanyiwa kazi? Au wameishia kuwakejeli tu?
 
...Atoe amri, vyombo vya usafiri wa umma, turudi kwenye level seats.
Kinyume na hapo atakuwa anafanya genocide
IMG-20210218-WA0075.jpg
Pia kuvaa BARAKOA iwe LAZIMA kwenye mikusanyiko, daladala, nk
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.

Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.

Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.

Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.

Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna hiyo kwa serikali sio sawa.
Tatizo mnaficha vifo hamtaki watu wajue kuwa wanakufa kwa corona. Sasa kama mnaficha na mnasema corona hakuna unategemea ushauti atoe nani wakati hamtaki kukubali kwamba tatizo lipo? Kubalini ukweli na watu watatoa ushauri unaousema
 
Naunga Mkono Hoja
Msema Kweli Ni Mpenzi Wa Mungu
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Sisi raia tumemwajir rais. Anawatendaji na vitendeakazi vyote vinavyohitajika. Anapaswa aongoze taifa kwa nuia iliyo sahihi. Unataka tutoe ushauri gani? Mimi kwa mfano sio daktari, sio mchumi lakini ni mlipa kodi. Nikiona vifo vinavyotokea na magonjwa yanayosumbua jamii nina haki ya kuhoji na kupewa majibu sahihi toka kwa serikali ambayo ndio yenye wajibu wa kudhibiti hali hiyo.
Uko sahihi kwa namna moja,
ila kwa namna nyingine unaweza ukawa sio mtalam wa fani yeyote ila kwa uzoefu kutokana na kuona, kusikia au kusoma kuhusu Corona ukawa na mawazo ya kushauri serikali, ijulikane huu ni ugonjwa mpya hivyo tukiwa na mawazo mengi toka kwa watu tofauti tunaweza tukafanikiwa.
 
Utatoa ushauri gani kwa Magufuli?
Ushauri sio kwa Magufuli peke yake, inawezekana ukatoa ushauri kwa raia wa kawaida namna ya kujikinga, ukatoa ushauri kwa watu walio hatarini zaidi n.k.
Huu ugonjwa ni mpya kwa hiyo inahitajika elimu kubwa kadiri iwezekanavyo
 
Mimi nasema kipimo cha korona kiwe bure, na takwimu zitolewe mbona za ukimwi na marelia tunapewa takwimu why korona tunaogopa kutoa?
Huo ndio ushauri unaohitajika na nakupongeza kwa hilo.
Umetoa ushauri na maoni bila matusi wala kejeli kwa Serikali ni vyema zaidi sababu inapelekea kujenga mshikamano baina ya serikali na wananchi.
Matusi, kejeli, mashinikizo n.k mara nyingi havijengi
 
Watanzania wanamuamini kiongozi wao, ndiyo maana hata wasomi kama katibu mkuu kiongozi huku wakijua kabisa kuwa korona ipo ila walisimamia imani ya boss wao.

Uliona jana kijana amesimama mbele ya jeneza la Kijazi pengine ni mwanae, yupo hana barakoa, sasa si muwaambie wavae, au mnapenda kuzika.

Waambieni watu wajikinge wanangojea kauli za nyie mliowaaminisha kuwa korona ni kwa mapapai mbuzi na mafenesi.
 
We mjomba umeeleza watu wametoa ushauri na waendelee kutoa ushauri, huo uliotolewa awali umefanyiwa kazi? Au wameishia kuwakejeli tu?
Ushauri unatakiwa kuwa mwingi kadiri iwezekananyo, na ushauri isiwe kwenda serikali tu bali iwe hata kwa wananchi wenzetu wa kawaida kwa kuelimishina nini cha kufanya na nini cha kuacha ili kujikinga.
Izingatiwe huu ni ugonjwa mpya hivyo elimu yake inahitajika sana
 
Back
Top Bottom