Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.
Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.
Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.
Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.
Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna hiyo kwa serikali sio sawa.