Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mhudumu wa uwanja wa KIA amesema katika kipindi hiki ambapo ugonjwa wa Corona Virus umepiga sana China, idadi ya watalii kutoka China imeongezeka maradufu kuja nchini.

Wachina wenyewe wakihojiwa wamesema pamoja na utalii wamekuja kutafuta sehemu salama kukimbia ugonjwa huo kwao.

Hii hali ininatisha sana haswa ukizingatia mgonjwa wa kwanza kufa huko ulaya yaani Ufaransa ni mzee aliyekuwa ameenda kutalii.

Swali la kujiuliza ni, kwanini katika hali critical namna hii serikali inaendelea kutoa viza kwa wingi na kuwaruhusu Wachina kuingia kwa wingi namna hii?

Hebu tujiulize laiti nchi yetu ingekuwa imepigwa na Ebola au Corona wangeturuhusu kukimbilia kwao?

Hii hali ni ya ajabu sana, wakati serikali hii inasuasua kuwarudisha watoto wetu walioko Wuhan (sababu mojawapo ni kuhofia hao watoto kuleta maradhi nchini), hii ni double standard kubwa, iba maana tunaweka mbele pesa za kitalii kuliko usalama wa taifa letu?

Wenzetu Wakenya wamesitisha safari za ndege zao China kuepuka kuleta maradhi nyumbani lakini sisi tumefumba macho kwa sababu ya kuogopa kuwaudhi wachina.

Mashirika makubwa ya ndege kama vile British Airways nao wamesitisha safari za China na kuna nchi kama vile zimesitisha kupokea watalii wa Kichina, sisi tunakwama wapi?

Shirika la Ethiopian Airline ndo limekuwa mchawi zaidi, lenyewe linaweka mbele maslahi ya fedha na hivyo kuhatarisha bara zima la Afrika, limeshutumiwa sana kuendelea kufanya biashara katika kipindi hiki cha hatari.

Hapa chini nimeweka video ikionyesha dege la Ethiopia Airline likishusha mamia ya Wachina huko KIA.

---





Pia soma
> Utalii: Wachina 600 kutua Tanzania wiki ijayo
> Serikali yatenga maeneo maalumu kwa watu watakaogundulika kuwa na Virusi vya Corona Tanzania

Your browser is not able to display this video.
 

Serikali hii inatishia usalama wa nchi kwa kuruhusu watalii wa kichina kuingia nchini katika kipindi hiki hatari.

Wamewatekelekeza watoto wetu huko Wuhan lakini wanaruhusu wachina kutsfuta Ukimbizi wa Afya nchini kwa kisingizio cha utalii
 
Inamaana bado wanakuja,

Dah yani huu ni upuuzi sana,hata kama kuwaogopa basi viongozi wetu hawatufanyii haki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani serikali yetu inatuogopa au kutuheshimu sisi wananchi?

Serikali yetu inasikiliza tu pale ikiambiwa kitu na EU, China na Marekani, sisi inatuona kama sisimizi tusiokuwa na chochote mbele yake

Sasa ona wanavyohatarisha maisha ya wananchi kwa sababu ya kuogopa wachina
 
Kipindi ninatetea wale wanafunzi wa Kitanzania warudishwe nyumbani nilipokea matusi na kejeli!! Sasa ndo mpembue mliokuwa mnapinga. Wachina wanapata usafiri wa kuja huku ikiwa wao ndio wahanga wakubwa wa COVID-19 na mnawakataa watanzania wenzenu!

Ilipaswa uwekwe utaratibu wa kuwapokea hao wanafunzi lkn badala yake wanaingia wachina kwa wingi!! Huku ndo kuruka majivu na kukanyaga moto.. time will tell
 

Ni aibu kubwa sana kaka
Tunawapotezea watu wetu wenyewe
Tunaruhusu wachina waje wakati wa kipindi hiki corona
 
Ni aibu kubwa sana kaka
Tunawapotezea watu wetu wenyewe
Tunaruhusu wachina waje wakati wa kipindi hiki corona
Wapuuzi walikuwa wanafikiri kuna njia moja tu ya huo ugonjwa kuja hapa ati kwa kuwaleta hao wanafunzi!! .
Bora zimwi ulijualo unaweza ukaliepuka kuliko usilolojua!!

Tunafahamu kabisa wale wanafunzi wanaweza kuwa na maambukizi hivyo utaratibu wao wa kuwapokea unakuwa yakinifu wa hali ya juu na wanatengewa eneo maalum wakiwa chini ya uangalizi yakinifu wa madaktari kwa muda hata wa mwezi.. kinachotokea hivi sasa ni kupokea zimwi ambalo hatulijui.
 

Tatizo tuna watu wenye inferiority complex wamejaa kwenye sehemu za maamuzi.
 
Umenikumbusha jana mchana,niliingia sehemu kwenye restaurant moja katikati ya mji,nikakuta rundo la wachina kama nane hivi, kwakweli nilitamani nitoke mbio, ila sikujua hata ujasiri wa kuendelea kukaa pale niliutoa wapi,ingawa niliposhiba ndio nikawa najiuliza hivi kilichonifanya nisiondoke ni nini,tuombe mwenyezi Mungu atunusuru na hili janga.
 
Kibaya zaidi huenda hawa watalii wanatoka au wanafanya kazi katika miji iliyowekwa quarantine kama vile Wuhan, ambao walifanikiwa kutoka kabla ya quarantine kutangazwa, wengi waliondoka Wuhan kwa ajili kusherehekea mwaka mpya wa kichina na hao ndo wamesambaza maradhi katika majimbo mbalimbali ya china na hata nchi nyingine, Kutokana na wao kutoweza kurudi huko Wuhan baada ya siku kuu zao za kichina kuisha pengine ndiyo maana wanakuja huku Africa kungoja quarantine iondolewe. Lakini Je serikali yetu inaelewa inachokifanya katika kuhatarisha usalama wa nchi namna hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…