Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Yani bora hao wanafunzi warudi aisee
Kipindi ninatetea wale wanafunzi wa Kitanzania warudishwe nyumbani nilipokea matusi na kejeli!! Sasa ndo mpembue mliokuwa mnapinga. Wachina wanapata usafiri wa kuja huku ikiwa wao ndio wahanga wakubwa wa COVID-19 na mnawakataa watanzania wenzenu!

Ilipaswa uwekwe utaratibu wa kuwapokea hao wanafunzi lkn badala yake wanaingia wachina kwa wingi!! Huku ndo kuruka majivu na kukanyaga moto.. time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mji wa Beijing wenyewe umepitisha sheria ya kuwaweka karantini wachina wenzao wanaorejea kutoka huko mikoani kwa siku 14, lakini sisi serikali ya CCM inakenua meno inawapokea na kuwaacha wachanganyike immediately kwenye mitas yetu, mahoteli yetu etc. What do you expect?
Serikali hii hopeless kabisa!
 
Hii serikali inazidi kua tishio kwa wananchi, na bado tutaipa tena nafasi..dah! sijui wabongo tulikwama wapi asee
 
Katika hali ya kawaida tu, ni muhimu kuangalia jambo hili kwa umakini, haiwezekani kbs wakimbie kwao waje kupumzika huku, hiki ni kipindi hataree kwa nin wasizuiee, idara za serikali muhimu kuliangalia hili
 
Hapana hatupaswi kufanya unyanyapaa kwa mtindo wa kutenga kwa hili "isolation" haipaswi kueleweka kama "discrinination".Zipo njia nyingi za kuhakikisha tunajilinda lakini siyo kwa kuwanyanyapaa wengine.

Wachina hawakuomba kupatwa na Corona "wakati na bahati huwapata wote".Hatuwezi kuwazuia Wachina wote hata ambao wapo salama wasiingie Nchini kwa kigezo cha "Corona". Tunafahamu tutakufa pia lakini tusikwepe kusaidia wenzetu kwa kiasingizio cha kufa.."what saves life is life".
 
Na kwa vile nchi nyingi wamepigwa ban watamiminika huku wanakopokewa, waliofika watawajuilisha wenzao kuwa Tanzania ni free waje tu. Serikali haipo serious, nna wasiwasi pengine hu ugonjwa hawausikii habar zake
 
Wewe muanzisha uzi umetumwa na mabeberu kuharibu uhusiano wetu na china


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umenikumbusha jana mchana,niliingia sehemu kwenye restaurant moja katikati ya mji,nikakuta rundo la wachina kama nane hivi,kwakweli nilitamani nitoke mbio,ila sikujua hata ujasiri wa kuendelea kukaa pale niliutoa wapi,ingawa niliposhiba ndio nikawa najiuliza hivi kilichonifanya nisiondoke ni nini,tuombe mwenyezi Mungu atunusuru na hili janga....
Sasa wewe unatofauti gani na serikili ya CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aah wapi. Sisi waafrika hasa watanzania tunaishukuru serikali ya dakta magufuri kwa usugu mkubwa wa gonjwa corona. Ikija watakao kufa ni chadema ila wale wa mashati ya mboga mboga utadunda. Wacha wachina waingie ili kudhibitisha hili. Asante sana dakta magufur.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha jana mchana,niliingia sehemu kwenye restaurant moja katikati ya mji,nikakuta rundo la wachina kama nane hivi,kwakweli nilitamani nitoke mbio,ila sikujua hata ujasiri wa kuendelea kukaa pale niliutoa wapi,ingawa niliposhiba ndio nikawa najiuliza hivi kilichonifanya nisiondoke ni nini,tuombe mwenyezi Mungu atunusuru na hili janga....
Juzi kati kuna wafilipino wawili waliambatana na mchina mmoja, walikuja maeneo ya ofisini aisee nilihisi nywele zimenisimama ghafla, nilitamani kupotea kwa muda. Uoga huu😅
 
Back
Top Bottom