Ugonjwa huu unapoendelea kuenea kote duniani (isipokuwa China kwa sasa) uwezo wa kuukomesha ugonjwa huu sasa ungali mikononi mwetu.
Tulipokuwa hatuna mgonjwa hata mmoja miito ilikuwa mingi kuzuia:
1. Ndege zote kutoka nchi zilizoathirika nao kuingia nchini
2. Kufunga mipaka yote ya nchi.
3. Kuwaweka wageni wote wanaotaka kuingia nchini chini ya uangalizi kwa siku 14 kabla ya kuwaruhusu watu kuingia nchini.
Tungezingatia haya ugonjwa huu usingeingia kabisa wala tusingekuwa tumefikia katika hali tete tuliyo nayo sasa.
Hatukuzingatia sasa tunalipa kutozingatia huko. Tutaendelea kulipa zaidi kwa kutoendelea kuzingatia hayo.
Kila siku inayopita bila kufanya maamuzi haya itatugharimu zaidi. Huu ndiyo ukweli wa wazi.
Tulianza na mgonjwa 1 sasa tunao 3.
Vivo hivyo Afrika Kusini walianza na mmoja hadi jana walikuwa nao 116. Rwanda walianza na 1 leo wana 8.
Italia walianza na mmoja hadi jana wanakufa 465 kwa siku.
Ni hatari zaidi kujifariji bure kama tulivyofanya hapo awali wakati tulipokuwa hatukuwa na mgonjwa hata mmoja.
Ni jambo la pongezi kuwa jitihada za kuondoa mikusanyiko hatimaye umeandika lakini bado haitoshi.
Kenya zaidi ya mashuleni hata misikiti na makanisa vyote vimefungwa.
Pamoja na hatua zile tatizo pale juu, ni muhimu tukasimamisha shughuli zote sasa. Watu wote wakasalia majumbani.
Kwa hatua hii mikusanyiko kwenye madaladala na masokoni itakwisha. Huu ugonjwa ni wa muda ufupi tutaweza kuudhibiti.
Total lock down siku 14 - 30. Huu ugonjwa utakoma.
Kwa wenzetu wanaelekea huku:
Senator Ledama wants landlords to suspend rent payment for three months over coronavirus scare
Chelewa yetu kuchukua maamuzi thabiti kwa wakati tujue itatugharimu zaidi.
Wahenga wanasema "chelewa chelewa utakuta mwana si wako".