Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

mbona tunahangaika sana....covid 19 haipaswi kuratewa kwa hali hii huku malaria ikiwa juu kwa vifo...tropical disease ni malaria corona ni Sub tropical so kila mtu ashinde mechi zake.
Aisee wataalam wa JF. Kwa hiyo haya maoni yako yanapaswa kuwapa watu matumaini?
Usi-misled watu. Corona ni pandemic. Ni tatizo kubwa na la hatari.
Watu wengi wanaoishi kwenye maeneo yenye malaria hawaugui ugonjwa huo mara kwa mara kwa sababu ya ile immunity wanapata kwa kuumwa na mbu mara kwa mara.
Hakuna vaccination wala dawa ya Corona. Halafu binadamu wengi hawajahi kuugua huo ugonjwa kwa hiyo ni vigumu kuwa na herd immunity.
Sasa endelea ku downplay issue serious. Kuna siku utajua hujui.
 
Serikali ya awamu ya tano ina watawala wa hovyo haijawahi kutokea.
 
Bahati mbaya sana umemuonea Ummy mwalimu kwa kosa ambalo sio lake yeye kama yeye hana mamlaka ya kufunga viwanja vya ndege huyo uliyemsifia kwa kuchukua uamuzi yeye na mwenzake (nadhani unamfahamu) ummy yeye ni mtu wa kutoa ushauri tu wenye maamuzi wapo ndio wa kulaumiwa
Angalau Ummy ameonyesha kuwatoa hofu watanzania maana watu wamepata hofu kubwa wakati afrika nzima rate na maa.bukizi yapo chini sana 0.006 huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi nyingi zilizoathirika na virusi vya Corona (COVID-2019) tayari zimefunga mipaka yake angalu kwa siku 30 ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo kwenye hizo nchi. Ukiacha mbali nchi za Ulaya, pia Africa ziko nchi zimeweka restrictions kwenye mipaka yake.

Sisi Tanzania tunakwama wapi? Au tunsubiri nini? Hivi kweli kama yule mama wa Arusha mlimpima na hakugundulika ni wangapi wa aina hiyo wanapita kwenye mipaka na airport?

Mie nadhani kazi kubwa ikifanyika mipakani huku kwenye jamii itapunguza taharuki.

Screenshot_20200318-232429.png

Rwanda tayari wametoa tamko. Uganda na Kenya nazo zimeweka restrictions kwa wageni. Mamlaka ya Tanzania hebu liangalieni hili swala. Wananchi tunawaangalia nyie.
 
Ukiachilia mapungufu atakayokuwa nayo, yani Museveni anaitambua Thamani ya maisha ya wananchi wake!
Katika hili nampongeza sana, Kwetu Tanzania ni Uzembe mkubwa sana. Deal na source kwanza, fungeni mipaka na wekeni restriction kweli kweli.
 
Tunahitaji watalii tuongeze pesa za kigeni
Kufunga mipaka ni kuwahukumu wasio na maambukizi sababu ya wachache wenye maambukizi

Hata hivyo covid 19 .........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa huu unapoendelea kuenea kote duniani (isipokuwa China kwa sasa) uwezo wa kuukomesha ugonjwa huu sasa ungali mikononi mwetu.

Tulipokuwa hatuna mgonjwa hata mmoja miito ilikuwa mingi kuzuia:

1. Ndege zote kutoka nchi zilizoathirika nao kuingia nchini
2. Kufunga mipaka yote ya nchi.
3. Kuwaweka wageni wote wanaotaka kuingia nchini chini ya uangalizi kwa siku 14 kabla ya kuwaruhusu watu kuingia nchini.

Tungezingatia haya ugonjwa huu usingeingia kabisa wala tusingekuwa tumefikia katika hali tete tuliyo nayo sasa.

Hatukuzingatia sasa tunalipa kutozingatia huko. Tutaendelea kulipa zaidi kwa kutoendelea kuzingatia hayo.

Kila siku inayopita bila kufanya maamuzi haya itatugharimu zaidi. Huu ndiyo ukweli wa wazi.

Tulianza na mgonjwa 1 sasa tunao 3.

Vivo hivyo Afrika Kusini walianza na mmoja hadi jana walikuwa nao 116. Rwanda walianza na 1 leo wana 8.

Italia walianza na mmoja hadi jana wanakufa 465 kwa siku.

Ni hatari zaidi kujifariji bure kama tulivyofanya hapo awali wakati tulipokuwa hatukuwa na mgonjwa hata mmoja.

Ni jambo la pongezi kuwa jitihada za kuondoa mikusanyiko hatimaye umeandika lakini bado haitoshi.

Kenya zaidi ya mashuleni hata misikiti na makanisa vyote vimefungwa.

Pamoja na hatua zile tatizo pale juu, ni muhimu tukasimamisha shughuli zote sasa. Watu wote wakasalia majumbani.

Kwa hatua hii mikusanyiko kwenye madaladala na masokoni itakwisha. Huu ugonjwa ni wa muda ufupi tutaweza kuudhibiti.

Total lock down siku 14 - 30. Huu ugonjwa utakoma.

Kwa wenzetu wanaelekea huku:

Senator Ledama wants landlords to suspend rent payment for three months over coronavirus scare

Chelewa yetu kuchukua maamuzi thabiti kwa wakati tujue itatugharimu zaidi.

Wahenga wanasema "chelewa chelewa utakuta mwana si wako".
 
Tunahitaji watalii tuongeze pesa za kigeni
Kufunga mipaka ni kuwahukumu wasio na maambukizi sababu ya wachache wenye maambukizi

Hata hivyo covid 19 .........

Sent using Jamii Forums mobile app
do you think Tanzania is more clever than all countries that has restricted its borders inlcuding airports ?
hata sanitizer ndio kwanza zinaaagizwa
 
Nchi nyingi zilizoathirika na virusi vya Corona (COVID-2019) tayari zimefunga mipaka yake angalu kwa siku 30 ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo kwenye hizo nchi. Ukiacha mbali nchi za Ulaya, pia Africa ziko nchi zimeweka restrictions kwenye mipaka yake.

Sisi Tanzania tunakwama wapi? Au tunsubiri nini? Hivi kweli kama yule mama wa Arusha mlimpima na hakugundulika ni wangapi wa aina hiyo wanapita kwenye mipaka na airport?

Mie nadhani kazi kubwa ikifanyika mipakani huku kwenye jamii itapunguza taharuki.

View attachment 1392445
Rwanda tayari wametoa tamko. Uganda na Kenya nazo zimeweka restrictions kwa wageni. Mamlaka ya Tanzania hebu liangalieni hili swala. Wananchi tunawaangalia nyie.
Nchi yetu ni ya kijamaa. Hatuwezi kufanya huo ubaguzi
 
Back
Top Bottom