Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Itabidi tuzuwie wa watu wa nchi nyingi duniani wasije, kwani corona kwa sasa hayupo China pekee.

Wacha waje tu. Kifo nini kifo tu iwe cha Corona au Malaria au Ukimwi au kingine chochote kile. Zote ni sababu tu.

Rudini kwa Allah mjisalimishe kwake, kifo tunatembea nacho, usikiogope. Kama si leo, kesho.
Njoo tupange nikukanyage na gari langu siku zako zifike uende kwa allah
 
Naunga mkono hoja, but it's very unfortunately, beggars can not be chooses!.
when your too poor na kazi yako kubwa is just to beg, wewe you just beg and you can't say no to anything however how small or risky it is, to you its money first, even just a small change, you can't say mo, you just say yes to everything!. Hizi ndizo gharama za umasikini.
P
Acha tu mkuu!

Umasikini ni laana.
 
wewe wa shule ya kata , wapo sana wasomi humu. Nawewe umekengeuka juzi , (ulikuwa msomi), kama walivyo wengi ukimwondoa Zito na Mbowe and some few others,
JF ni social forum, tukakata tuu issues, professional ya mtu na usomi wa mtu sio issue humu, issue humu ni hoja tuu, kuna wasomi tena wa Ph.D na wanamwaga pumba, na ma darasa la saba tuu lakini wanamwaga nondo.

Mfano mzuri mwangalie huyu jamaa,

Ni darasa la Saba tuu,

Halafu waangalie hawa ma professors na uprofesa wao, hapa wamefanya nini

Mwisho wa siku, rais wetu Magufuli alidanganywa, na waliomdanganya sio darasa la Saba, ni ma professors!.

Hivyo usomi sio issue kabisa, issue humu ni hoja tuu.

P
 
Pascal Mayalla,
Huwezi kuwa darasa la saba ukawa na issue, labda useme hizo issue unazitolea kwa wajinga, mazuzu wenzako na wanaziona za maana kwa vile reasoning yao imeishia hapo! kama lilivyo bunge la ndugai. Wote mle ni wajinga, mazuzuz etc! Kama ulisikiliza debate za impeachment ya Trump ndiyo utaona tofauti ya wasomi na wajinga kama nyie!
 
Itabidi tuzuwie wa watu wa nchi nyingi duniani wasije, kwani corona kwa sasa hayupo China pekee.

Wacha waje tu. Kifo nini kifo tu iwe cha Corona au Malaria au Ukimwi au kingine chochote kile. Zote ni sababu tu.

Rudini kwa Allah mjisalimishe kwake, kifo tunatembea nacho, usikiogope. Kama si leo, kesho.
Hata kama kifo ni kifo uislam unazingatia na tahadhari pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo hii Corona virus limekuwa janga la dunia. Ugonjwa huu sasa hivi umeshaingia kila bara isipokuwa bara la Antactica peke yake.

Inasikitisha sana sisi kama nchi serikali yetu tangu kutokea kwa ugonjwa huu imeendelea kupokea watalii kutoka China wakati ikijua kuwa hali ya China kwa sasa ni mbaya.

Watalii wanaingia nchini, wafanyakazi wetu airport huko KIA na Dar hawana vifaa kazi vya kujikinga na ugonjwa huo.

Serikali inajua kuwa ugonjwa huo unaweza kuambukizwa na mtu ambaye ana virusi lakini haonyeshi dalili.

Na serikali yetu inajua kuwa kuna mamilioni ya wachina walikuwa wametoka katika mji wa Wuhan kwenda kwenye majimbo mengine kwa ajili ya sikukuuu yao ya mwaka mpya wa kichina, Wachina hawa hawawezi kurudi tena Wuhan kwa sababu mji umefungwa, hakuna kuingia wala kutoka. Na wachina hawa baadhi yao wenye pesa ndiyo wanasafiri duniani ili kusubiria huko kwao kuwe vizuri, hawa wanasambaza maradhi.

Najiuliza katika kipindi hiki kigumu unawezaje kuruhusu watu kutoka Taifa hilo kuingia kwa wingi nsmna hiyo kwa kisingizio cha utalii?

HIVI SISI TUNAJITAMBUA KWELI?

Nilishangaa kuona clip ya mfanyakazi wa KIA akieleza jinsi idadi ya watalii nchini kutoka China ilivyoongezeka kipindi hiki cha Corona. Nataka niambie serikali, miongoni mwa hao kuna wakimbizi wa Corona huko kwao siyo watalii.

Kiukweli namna ambavyo serikali yetu inachukulia poa hili suala, namna ambavyo inalichukulia kwa mtindo wa business as usual ni namna ya kuogoesha na kusikitisha.

Kiufupi ninasema kama hili balaa litapiga nchini mwetu basi Rais Magufuli hatokwepa lawama kwa sababu alikuwa na muda wa kutosha kuchukua hatua ya kuilinda nchi dhidi ya wageni wanaoingia lakini yeye na serikali yake wakaamua kufumba macho ili tu kupata fedha za utalii. Kiufupi tumeweka mbele maslahi ya fedha chache za kipindi kifupi badala ya mustakbali wa afya na maisha ya watu milion 50 nchini.

Linapokuja suala la maradhi hakuna cha urafiki wala undugu wa nchi kwa nchi, hilo halipo, huu ugonjwa ungetokea kwetu, Wachina wasingeruhusu Mtanzania hata mmoja kuingia kwao.

Hivi sisi tunajitambua kweli?
 
Huwezi kuwa darasa la saba ukawa na issue, labda useme hizo issue unazitolea kwa wajinga, mazuzu wenzako na wanaziona za maana kwa vile reasoning yao imeishia hapo! kama lilivyo bunge la ndugai. Wote mle ni wajinga, mazuzuz etc! Kama ulisikiliza debate za impeachment ya Trump ndiyo utaona tofauti ya wasomi na wajinga kama nyie!
Mkuu paskali amekua mtumwa siku nyingi sana.asikusumbue kichwa.hapo anataka ujinga uone ni kitu cha maana
 
Hizi ni statement za watu ambao hawakusoma science at advanced/college lvel!
It's true, mimi science niliagana nayo O level.
Ila hii statement is true, uhai umeumbwa na kifo pia kimeumbwa, kama ilivyo kwa kila lenye mwanzo, pia lina mwisho, kuzaliwa ndio mwanzo wa maisha, na kifo ndio mwisho wa maisha hivyo wote tutakufa tuu siku yetu ikifika.

P
 
Pascal mkuu, awamu hii ndiyo tatizo japokuwa wewe ni mtetezi no1 wa hii awamu.

Ingalikuwa awamu zilizopita Jambo Hili hata bungeni lingejadiriwa na kuishauri serikali Nini Cha kufanya,lakini spika ndugai ni mlamba miguu tu.

Waziri wa afya nae ndiyo hovyo kabisa.
Nilimsikia akipinga bungeni hoja ya sugu kuwa hospital za serikali zinazuwia maiti mpaka ndugu walipe gharama za matibabu.
Siku iliyofuata nikamwona luningani akitoa tamko kuwa hakuna kuzuwia maiti.

Corona itatumaliza,Kama wachina tunaowategemea kifedha wanahaha kupata Tiba na chanjo hawajapata, je sisi tutapataje kupona?
AWAMU HII NI SHIDA,NI JANGA
Naunga mkono hoja, but it's very unfortunately, beggars can not be chooses!.
when your too poor na kazi yako kubwa is just to beg, wewe you just beg and you can't say no to anything however how small or risky it is, to you its money first, even just a small change, you can't say mo, you just say yes to everything!. Hizi ndizo gharama za umasikini.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajivunjia heshima uliyojijengea miaka mingi na inawezekana kwa gharama kubwa.
Uhai umeumbwa, na kifo pia kimeumbwa tena uliisha andikiwa ile siku unazaliwa, hivyo kama uliandikiwa utakufa kwa Corona, utakufa kwa Corona na huwezi kuzuia kifo.

Hebu acheni hao Wachina na wengine wote waje kutuletea hizo forex tunazo hitaji sana.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom