Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Aliyetuloga alishakufa na kaburi lake halijulikani lilipo tungeenda kulilia kuomba toba!
 
Hao ni wakimbizi dhidi ya corona viruses, weupe wote wanakimbia kwenda western countries,

safari hii hawatakiwi ajili ya hili gonjwa baya... Ingekuwa ni vita nchini mwa wasingekimbilia huku.

Magonjwa,kuchuma mali na mambo hatari yote ukimbizi ni Africa,
 
Umefikia KIA baada ya mlipuko wa ugonjwa wa CORONA? Mimi nimepita na wahudumu wote wamevaa Mask ila DAR ndio sikuwaona na MASK
 
Mask sio issue kumbuka hata Madaktari wanao watibu wagonjwa huvaa Mask na bado wanakufa we unazani hizo mask watavaa siku zote hao wachina wakifika huku watavaa siku zote? Ulisha wahi kuwaza kwa mfani ile nyomi ya kkoo kama ugonjwa ukilipuka nn kitatokea?
Umefikia KIA baada ya mlipuko wa ugonjwa wa CORONA? Mimi nimepita na wahudumu wote wamevaa Mask ila DAR ndio sikuwaona na MASK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mask sio issue kumbuka hata Madaktari wanao watibu wagonjwa huvaa Mask na bado wanakufa we unazani hizo mask watavaa siku zote hao wachina wakifika huku watavaa siku zote? Ulisha wahi kuwaza kwa mfani ile nyomi ya kkoo kama ugonjwa ukilipuka nn kitatokea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri hasa kwa upande wa AIRPORT zetu ni nini?
 
Tumeshazoea kuchukua hatua baada ya kushambuliwa kwanza na majanga.
Kwahili serikali haitaepuka hasira ya wananchi. Ni jambo ambayo linaweza kupelekea uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali.
Serikali uichukue hatua mapema
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana hivi kweli tunakubali hii hali? gharama yake itakua kubwa kuliko hivo visenti wanavyoleta hao wachina
 
Ni picha ya leo,Pope aliahirisha misa juu alikua na tatizo dogo la kiafya
pamoja na nia njema, lkn ni hatari sana kuwapokea , kuna andishi linasema on average incubation period ya hao virus ni siku 14 lkn imegundulika kuwa inaweza kwenda hadi siku 24 , hivyo mtu anaweza pimwa leo akaonekana hana lkn baada ya 10 days ikaibuka
 
Ina uma Sana ndugu Zanguni

Imagine Mwanao yupo China amekataliwa kuja Tanzania Wakati huo huo Nchi inapokea Watalii kutoka kutoka huko huko China

Mbona Mnatufanyia hivi Serikali ya Awamu ya Tano ??

Mnataka tufe Kama kuku waliovamiwa na Mdondo ??
 
Ikiwa jambo kubwa kama kuhiji lakini saudia ikapiga marufuku watu kuingia nchini mwao ili kuudhibiti ugonjwa sisi tamaa tumeweka mbele tunakaribisha mamia ya wachina ukilipuka hapa sijui tutakimbilia wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa wa Corona umezidi kusambaa kwa kasi na kuingia kwenye nchi nyingi duniani licha ya tahadhari kubwa na teknolojia ya hali ya juu ya kuchuja wageni





Baada ya kuona ugon jwa huu haudhibitiki kirahisi sasa imepelekea nchi nyingi kukata mawasiliano kabisa na nchi zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huu kama China, Iran, Italia, Japan na Korea

Hata hivyo Tanzania haina habari, Tanzania imezidi kupokea watalii kutoka China huku ikijidai kuwa haijali raia anatokea wapi kwa kuwa ipo vizuri kwenye kujilinda

Hiki ni kichekesho ukizingatia facilities na teknolojia za Tanzania ukizilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zimefunga kabisa usafiri na nchi athirika kwa hofu ya kuenea ugonjwa huu,

nchi kama Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa China imepiga marufuku raia wote kutoka China sababu ya ugonjwa huu ambao aambukizi yake hayaonekani mpaka zipite siku 14, nchi nyingine zilizopiga marufuku kabisa raia wa China ni Australia, Singapore, Iran, Ufilipino, New Zealand n.k

Nchi nyingine zimefika mbali zaidi kwa kupiga marufuku kabisa hata raia wa nchi nyingine ambaye aliwahi kwenda China siku za karibuni

Nchi kama Saudi Arabia imesitisha ibada za Hijja ndogo kutokana na hofu ya maambukizi haya, na inaweza kupiga hata marufuku ya Hijja kubwa

Nchi nyingi za kiarabu pia zimekatisha kabisa safari zake na Iran ambayo ina waathirika ambao hawafiki hata 300 kwa hofu ya ugonjwa huu, lakini Tanzania inaruhusu watalii kutoka China kwenye maambukizi ya takribani 80,000





Kwani hujui kuna mtu ana dawa ya Corona huko Arusha? Achana na Tanzania tuko juu sana!
 
Back
Top Bottom