Serikali: Siku za Kigogo wa Twitter zinahesabika na hana siku nyingi

Serikali: Siku za Kigogo wa Twitter zinahesabika na hana siku nyingi

CANARY TRAP strategy ilifanya kazi na hana muda mrefu...

Ila serikali ya Tanzania bado imelala sana, ingebidi itangaze dau waziwazi kama milioni 250 kwa mtu atakaye fanikisha kufanikisha kutoa habari zitakazoweza kumpata kigogo na hakika hata wiki haitaisha anakamatwa mapema...

Hawa washauri wa serikali sijui huwa wanawaza nini?? vichwa vyao viko tupu 100%, na hakika kuna watu wanamjua kigogo fika, sema hawawezi mchoma katika mamlaka husika burebure, hapa serikali iingie BOT ichote fedha iweke mezani tuone kama huyo kigogo atachukua round...

Mbinu za kutumia wadada zilikuwa za zama hizo miaka ya 80 (kwa hii mbinu ni ngumu kumkamata kigogo maana ni mjanja kwelikweli), miaka ya hivi karibuni ni fedha tu inaongea.

Hawaoni wenzao Marekani wanachofanya kwa magaidi wanatangaza dau kubwa, waarabu uvumilivu unawashida wanaishia kuwachoa magaidi waliotikisa dunia...
Mkuu wabongo hua hawawezi kusema tumeshindwa mbele ya hela. Kiufupi mbongo hawezi kuruhusu pesa impite kiboya boya tu eti kisa unachokitaka yeye hana

Kwenye pesa aisee kila mtu ni masai ukimdhamini tu umekwisha, we kila ukiangalia unadhani mtu yupo kumbe ni shuka ye mwenyewe kasepa kitambo


hata ukienda kununua simu kariakoo ukifika dukani usipoiona simu unayoitaka hawata kuruhusu uondoke na hela utaambiwa simu unayoitaka wewe kwa hapa haipo ila nisubiri nikakuchukulie kwenye store yangu. Lakini sio kweli kua simu inaenda kuchukuliwa kwenye store yake, bali kwenye duka lingine ilimradi tu apate hata 10k ya udalali kuliko kuruhusu pesa impite kabisa
 
Mbona mnamuongelea kigogo kama mtu haramia, wakati ni mnyetishaji wataarifa muhimu kwa uma
 
Forget it. Kigogo is a phenomenon not a personality.
Walisema hivyo hivyo kuhusu Osama! Lugola akimshindwa Kigogo 2014 ndani ya siku 31 itabidi ajiondoe kwenye nafasi ya uwaziri. Naanza leo kuhesabu
 
Do you remember the issue of JK on "The Utamu"? The guy was in UK but mkono wa.serikali reached him!!
Propaganda huyo Male Lusinde wala hakukamatwa ulikuwa uzushi tu serikali hii kwa uongo!
 
Kigogo2014 yupo kuunga bando la mwezi wa siku 31
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema mtu anayejiita Kigogo2014 siku zake zinahesabika na atatiwa mbaroni muda si mrefu kwani hata mwezi una siku zisizozidi 31

Mh Lugola amesisitiza kuwa yeye leo hana maneno mengi ila ujumbe huo umfikie huyo kigogo2014 popote pale alipo.
Kuna vitu huwa havitangazwi
tapatalk_1572617323774.jpeg
 
Wakishamdaka iweje? Au wanamtafuta wakamlishe yule chatu wao wa kigamboni? Eti wawatumie wahuni wa kimataifa kunsaka mtu anayeandika tu mawazo yake na Kisha wawalipe! Kama watatumia mishahara yao kuwalipa ni sawa but sio fedha za umma!
Kuzushia viongozi vifo ndiyo mawazo? Huo upotoshaji wa kulete taharuki ndo mawazo?

Awazushie vifo wazazi wake uone kama kuna mtu atakuwa hata na muda naye basi.

You peep your nose in other people's affairs, you pay the price,hii ni duniani kote.

Tena huyo kwa kuwa ni anonymous akidakwa ni hakuna cha press wala mahakamani,mtaona kimya tu.
 
kigogo kwa mawazo yangu sio mtu 1 ni kundi la watu (tena wataalamu sana) kuna siku niliona akisema 'walimdukua wakachemka" unaweza pata picha jamaa ni wa moto kiasi gani?

hii kudanganyana sijui mtego wa kuumwa maggu sijui nini ni porojo
Ila Magu alikuwa anaumwa kweli diyo uongo
 
Kigogo 2014 (asiyejulikana) anaisakama serikali ya awamu hii hasa maovu yake anatafutwa kwa kuambiwa siku zake zinahesabika. Bahati nzuri katoa hadi namba ya simu yake (kigogo) apigiwe. Mie nauona ni ujinga na kuhamisha mjadala wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Na kwa lugola kaona ni ajenda kubwa sana.

Musiba huyu anajupikana kanyamaziwa kimyaa wala sijasikia tena akiitwa kuhojiwa wala kuripoti polisi. Huyu bila shaka Lugola kakwaa kisiki.

Uchaguzi serikali za mitaa. Hapa ndio serikali ya ccm kama inavyojiita imekaa kimya dhidi ya madhira wanayofanyiwa upinzani huku watendaji wakiwa watekelezaji wakuu wa madhira hayo huku wakisimamiwa na ccm na jeshi la polisi.

Walinzani wanaonekana kama wahaini wa nchi hii na wahalifu huku serikali ikiwa kimyaa ila itokee ccm kapigwa au mtendaji kafanyiwa kama wanavyofanyiwa upinzani utaona tv, magazeti na lugola wakitoka mafichoni na kuwaita magaidi na wamwaga damu. Ila kwa kuwa ni wao hayo majina huyasikii wala kukemea wala kuchukua hatua yoyote.

Bila shaka naona lugola katoka na katumwa kuja kubadiri hali ya upepo watu wasizungumzie maisha yao na mustakabari wa miaka 5 ijayo bali wabaki na habari za umbea wa Kigogo 2014
 
Back
Top Bottom