Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Umenena vyema, akanunue chakula cha kutosha aihifadhi msiwapangie wakulima pakuuza mazao yao. Km watamaliza mazao yao itakula kwao. Huwezi kumsimamia mtu mzima mwenye akili yake. Tuishia km wazungu wajibika kwa uzembe wako we ni mtu mzima jiwekee akiba. Mara mama fungua mipaka leo funga mipaka hamuoni hata aibu? Rais ana mambo mengi ya kufanya siyo kuwawekeeni akiba. Mkulimwa hajawahi kuwapangia namna au sehemu ya kutumia mishahara yenu au mapato yenu ya biashara msiwapangie soko la kuuzia mazao yao. Watakaouza mazao yote shauri yao.
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao

Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati

imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya

Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa

mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula

CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda

tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui

Sawa bwana
wacha yauzwe bei juu wanashindwa kusema yapunguwe mana wanajuwa walivyoacha mbolea kupanda bei.
 
Tulishauri mwaka huu mavuno ni kidogo wafunge mipaka kwani hata soko la ndani tu linatosha wakashupaza vichwa vyao, mavuno yakiwa mengi watu wauze nje ni sawa lakini mwaka wenye mavuno kidogo nao wauze nje kipindi chote hapana, Burundi kuuza mahindi, maharage, mtama na muhogo ni uhujumu uchumi kwa sasa, uganda kazuia hakuna kuuza chochote nje isipokua ni ruhusa kununua, na kuingiza ndani, Rwanda kazuia kabisa hakuna kutoa hata kiazi, wizara ya kilimo ipo ipo tu imekalia siasa, hakuna usalama kama nchi haina chakula cha kutosha na mkumbuke dunia nzima mavuno kwa mwaka ulioisha yalikua hafifu sana, viongozi hawachukui maamuzi simply sababu wao na familia zao njaa haitowakumba.
Mipaka ifungwe ili wakulima wauze mazao yao kwa bei rahisi ??! Kwani huwa wanasaidiwa na Nani kulima ??! Kila mtu ashinde mechi zake !!! Na kazi iendelee !
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida.

Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Nani kakwambia mkulima ndiye anayenufaika na biashara hii ya chakula kupelekwa nnje ya nchi?

Njoo huku Kusini (Mtwara na Lindi) uone jinsi tunavyonunua ufuta kilo moja tsh 1100 - 2000 kutoka kwa mkulima na sisi tunauza tsh 3190 kwa kilo.

Mkulima ananufaikaje na bei hiyo ya 3190 kwa kilo!!??
Mnapenda kuongea vitu ambavyo hamvifahamu.
Wakulima wanaonufaika na bei kubwa ya mazao ni wakulima wakubwa tuu.

Wanufaika wakubwa wa kupanda kwa bei ya mazao ni watu wa kati (madalali) ma wafanyabiashara wa mazao.
Nikupe mfano mmoja,kuna kijiji ambacho wakazi wake walilima ufuta na kupata mavuno mazuri lakini changamoto yao ni kuwa umbali wa kutoka hapo kijijini mpaka kwenye mnada wa ufuta ni km 29.

Hakuna usafiri wa mabasi.
Mimi nimeenda huko nikawaambia nanunua ufuta kwa tsh 1200 kwa kilo,wamekubali kuliko kusubiri kwenda mnada ambao watauza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani itakayowachukua wiki kupata fedha yao.

Umeona mkulima anavyoteseka hapo sasa!?
 
Wanaouza mazao wakati huu wala mkulima hahusiki kabisa tena ni mapesa toka nje yaliyoingia kununua mazao na kuweka stock mazao kwa mfano kijiji cha gwarama kule kakonko.

Wanyarwanda wamejenga magodown kupitia wafanyabiashara wa pale na kila mwaka huweka tani nyingi mno za mazao wakati kama huu husafirisha, haya pale nyakanazi kuna tajiri wa burundi anaitwa kamangaza ana magodown pale kupitia wazawa na hununua mahindi mengi sana na mtama, na huanza kusafirisha kwenye uadimu hali kadhalika.

Wafanyabiashara wakenya huingiza pesa nyingi sana kule chunya na songea nakuweka store tani nyingi sana za mazao, kwahiyo tunaposema mfunge mipaka tunamaana mnufaika kwa sasa sio mkulima kama mnavojidanganya, mavuno yangekua mengi ni sawa lakini mnakaza vichwa huko serikalini wakati hamna hata taarifa za kutosha.
 
Kuna mbunge wa kanda ya ziwa huitwa nassor huyu hununua mahindi ya mabilioni kila mwaka na yuko share na wakenya pia, huweka stock za kutosha, mkulima wa Tanzania wa jembe la mkono wa Tanzania aliuza mazao yake mwezi wa nne sababu ya umaskini hakuna mkulima anaeweka stock mazao ninyi mko ofisini hamuwezi kuelewa kitu, tungekua tumevuna sana sahihi kabisa kuachia mipaka
 
Haya kijiji cha kasuga mkoani kigoma mashamba makubwa ya zao la muhogo yanamilikiwa na Warundi ambao huwatumia wenyeji kama wasimamizi na wakivuna wanasubiri either kusafirisha kwenda kwao au kuuza Tanzania kulingana na bei ilivo
 
Hii nchi bwana, wakati wakulima tunalalamika bei ya mbolea na pembejeo hakuna aliyelia na sisi. Leo tunauza mazao bei juu ili kufidia gharama za uzalishaji na kipato kidogo tulichovuna kutokana na mbua inakuwa nongwa.

Huko nyuma; mbolea ilikuwa 28,000 SA na Urea 55,000. Leo SA 85,000 mpaka 90,000 na UREA 140,000. Bado madawa ya magugu, wadudu na virutubisho vingine. Hapo hujanunua mafuta kwa wale waliolazimika kutumia pampu kwa ajiri ya umwagiliaji. Wakulima tumelima kwa gharama kubwa sana mwaka huu na kipato kimekuwa kidogo sana, angalau tunaponea kwenye bei.

Ata hiyo mipaka ikifungwa tutaweka mazao yetu ghalani mpaka tukutane na bei itakayotupa uhakika wa kurejesha gharama zetu.
 
Wakulima wakubwa wa mpunga ifakara ni waganda ambao hukodi mashamba, na kuanza kulima baadae husafirisha mchele kuelekea kahama kwenda uganda ukitoa wasukuma hao wandamba na waluguru huko hawana kitu, inabidi tuwaeleze muelewe mavuno ni machache funga mipaka wanyarwanda na warundi wanaolima hadi binti manyanga kwenda kambi katoto chunya huko watauza chakula ndani hawatosafirisha kwenda kwao
 
Biashara ya mazao ni kitu cha aina yake waziri bashe kaa ofisini lakini nauhakika haujui lolote huku field nini kinaendelea maana hata uhakiki wa wakulima wenu hamjafanya ndio maana wageni hununua mashamba kama wazawa na kuanza kuchapa jembe kama kawaida lazima muwe na mipango ya kueleweka
 
Njaa kwa maana ya mtu unaenda sokoni na pesa yako halafu unakosa unga au mchele haiwezi tokea.

Wafanyabiashara wanavusha mazao kwa maana huko nje bei ni juu kuliko hapa.

Bei yetu ikipanda sawa na wanakopeleka,hawatapeleka nje tena.

Kwahiyo inabidi watu wakomae kutafuta pesa zaidi vyakula havitaisha sokoni mpaka msimu ujao.

NB:Hizi bei zinachangiwa na bei ya mafuta pia siyo uhaba wa mavuno pekee.
 
Serikali haihusiki,sema hali ya hewa imetuumiza sana...tumepata mazao Kwa kusua sua sana [emoji26]
Hakika, Hali ya hewa haikuwa poa na ilijulikana itatokea.
Ila Kwa Bei za mbolea, acha tu hata Gunia la mahindi lifike 200,000.
 
Mipaka ifungwe ili wakulima wauze mazao yao kwa bei rahisi ??! Kwani huwa wanasaidiwa na Nani kulima ??! Kila mtu ashinde mechi zake !!! Na kazi iendelee !

Mimi ni mkulima na biashara ya mazao naijui kuliko wewe, mwaka huu mavuno ni machache soko la ndani pekee halina mazao, siwezi kufurahia kuuza sudani kusini au Rwanda wao wapate chakula huku nchini kuna njaa, tungekua tumevuna sana ruksa kuuza nje lakini hali ya mvua uliiona ilivo leo hii tunapoongea mimi na wewe kigoma, rukwa, katavi, mbeya, morogoro hakuna tena mazao sasa mikoa ya uzalishaji kama hiyo ikikosa chakula unategemea nini? Hii ni mwezi wa saba ukumbuke usifurahie bei kupanda angalia mateso ya maskini huko vijijini kwetu ambao kula yao hadi sasa ni shida, MAVUNO NI KIDOGO MWAKA HUU SOKO LA NDANI TU HALINA KITU HAKUNA SABABU YA KUFUNGUA MIPAKA.
 
Kuhusu mbolea ni sera mbovu za wizara ndio maana ni rahisi sana kuingiza mbolea ya magendo aina ya Fomi toka burundi ikawa chini kuliko kununua ya Tanzania imekaa kiujanjaujanja sana
 
Hii serikali sidhani kama inajua implication ya hiki inachofanya kuruhusu chakula kusombwa na malori kwenda kenya. Au wanasubiri siku wananchi wakiandamana kwenda kwenye makazi ya rais kuomba msosi kama kule sri lanka ndo watajua hali imekuwa ngumu.
 
Wapo baadhi ya wakulima wamejanjaruka na wanafanya kila wawezalo ili kupata faida na kilimo chao. Serikali ikianza kufunga mipaka itawaumiza hata hao wachache.
Nani kakwambia mkulima ndiye anayenufaika na biashara hii ya chakula kupelekwa nnje ya nchi?!??
Njoo huku Kusini (Mtwara na Lindi) uone jinsi tunavyonunua ufuta kilo moja tsh 1100 - 2000 kutoka kwa mkulima na sisi tunauza tsh 3190 kwa kilo.
Mkulima ananufaikaje na bei hiyo ya 3190 kwa kilo!!??
Mnapenda kuongea vitu ambavyo hamvifahamu.
Wakulima wanaonufaika na bei kubwa ya mazao ni wakulima wakubwa tuu.
Wanufaika wakubwa wa kupanda kwa bei ya mazao ni watu wa kati (madalali) ma wafanyabiashara wa mazao.
Nikupe mfano mmoja,kuna kijiji ambacho wakazi wake walilima ufuta na kupata mavuno mazuri lakini changamoto yao ni kuwa umbali wa kutoka hapo kijijini mpaka kwenye mnada wa ufuta ni km 29.
Hakuna usafiri wa mabasi.
Mimi nimeenda huko nikawaambia nanunua ufuta kwa tsh 1200 kwa kilo,wamekubali kuliko kusubiri kwenda mnada ambao watauza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani itakayowachukua wiki kupata fedha yao.
Umeona mkulima anavyoteseka hapo sasa!!???
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao

Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati

imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya

Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa

mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula

CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda

tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui

Sawa bwana
CCM ni zaidi ya shetani asew
 
Back
Top Bottom