Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Acha uzushi Mzee,ikibidi njaa ikukumbe tuu la sivyo na wewe kalime..

Ukiona mtu anauza ujue anauza ziada..

Hiki ni kipindi cha wakulima kunufaika,ukitaka bei ya chini nenda shambani toka kucheza BAO huko mjini.
 
Hii serikali sidhani kama inajua implication ya hiki inachofanya kuruhusu chakula kusombwa na malori kwenda kenya. Au wanasubiri siku wananchi wakiandamana kwenda kwenye makazi ya rais kuomba msosi kama kule sri lanka ndo watajua hali imekuwa ngumu.
Alaa kwa hiyo chakula huwa kinasombwa tu, wewe hapo kiazi unajua implication yake?

Ni hivi ukitaka cha Bei rahisi nenda kalime.
 
Wapo baadhi ya wakulima wamejanjaruka na wanafanya kila wawezalo ili kupata faida na kilimo chao. Serikali ikianza kufunga mipaka itawaumiza hata hao wachache.
Waambie hao wapumbavu wakalime afu wakizalisha waiambie serikali ifunge mipaka..

Yalivyo mapumbavu yanashindwa kujua kwamba kilimo ni biashara kama biashara nyingine..

Mwaka ulioisha mchele umeleta pesa nyingi za kigeni kuliko zao lolote linaloitwa la biashara kama pamba,chai,kahawa na korosho.
 
unga kilo ni sh. 1300 acheni kupotosha.
mahindi huku namtumo songea bei chee kabisaa, Pia huku Galapo babati mahadi bei poa kabisaa.
Achana na wapumbavu tuu hao mkuu..

Mashineni Katavi mchele kilo ni 1700 tena supa na Michele imejaa..

Yanaropoka tuu bila hata Takwimu.
 
Masukuma gang na yule kichaa wao ndio waliharibu kilimo hapo katikati
 
VIONGOZI mmelala ngoja tuwape taarifa ambazo hata hamzijui enedeleeni kukaa kwenye viyoyozi lakini watu wakipata njaa kamwe hamtotawala vizuri jiongezeni mnaposhauriwa na watu waliopo ground
Njaa ipi hiyo? Kwamba chakula ni mchele na mahindi tuu au?

Kwamba watalima afu wauze chote waje kupata njaa au? Toa ujinga wako hapa Mzee.
 
Mkuu hawa wanaojifanya wakulima humu JF ni madalali na wafanyabiashara wa mazao ambao serikali ikibana usafirishaji wa mazao biashara yao ya kulangua mazao kutoka kwa wakulima kwa bei chee na kuuza kenya itakuwa imetumbukia nyongo. Lakini ulichoeleza ndiyo uhalisia, mkulima hajawahi kufaidika na bei ya mazao kuwa juu zaidi ya madalali na walanguzi wa mazao wanaojiita wafanyabiashara ambao wamekuwa wakibana mizani na kujaza lumbesa kuzidi kumnyonya mkulima.
 
Tunakujua chawa wa kutetea utopolo, kwa hiyo huwezi kushangaza yoyote humu.
Upumbavu wenu wasimulieni wake zenu..

Ukitaka bei rahisi kalime,au Lima harafu waambie serikali wafunge mipaka..

Ila kwetu awamu ya 6,kilimo ni biashara kama hardware and the likes..

Awamu ya 6 sio wapumbavu kama awamu ya 5,tumeingiza bil.954 hatuwezi acha zipotee tunataka zilete tija kwa kilimo kuchangia 10% ya Pato la Taifa..

Ushenzi wenu mtafanya mkijapata madaraka na kuwaongoza wajinga
 
Unaongelea kilimo biashara kwenye nchi ambayo raia wake wengi ni mafukara wa kipato, wakiwemo na watumishi wanaolipwa mishahara kiduchu.....wewe jamaa huu uzwazwa sijui unautoa wapi.
 
Unaongelea kilimo biashara kwenye nchi ambayo raia wake wengi ni mafukara wa kipato, wakiwemo na watumishi wanaolipwa mishahara kiduchu.....wewe jamaa huu uzwazwa sijui unautoa wapi.
Ndio tunawatoa huko kwenye ufukara mlikokuwa mumewafukia sasa na njia rahisi ni kuwahakikishia soko.
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Ona hii kenge...
 
Ndio tunawatoa huko kwenye ufukara mlikokuwa mumewafukia sasa na njia rahisi ni kuwahakikishia soko.
Aliyekwambia mkulima wa kawaida kule kijijini ananufaika na biashara ya mazao nani, mkulima amekuwa ni mtu wa kunyonywa na walanguzi na madalali kupitia lumbesa, kubana mizani na kupewa bei ndogo, jaribu kutumia akili kufikiri kwa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…