mkuu hoja yako ni ipi hapa? kwa hiyo kama kulitokea utata wa kifo cha wangwe na USA hawakutoa tamko je hilo liinahalalisha uwepo wa vifo vyenye utata leo na je inahalalisha USA isitoe tamko leo? kwa hiyo mkuu unaona yaliyotendeka ni sawa? mtajibu nini kwa Mungu Mkuu maana siku yaja na dunian ni mapito tu. hiv mkuu madaraka hayo ni ya miaka mingapi hata ukiyapata kwani utaishi nayo kwa mda gani? kitu cha kupita tu hapa duniani unahalalisha roho za binadamu wenzako kupotea?
siasa sa ghilba mkuu huwa hazidumu. jaribu kufikiria eti ili kumwangusha mpinzani wako unatumia pesa za walipa kodi unamnunua diwani mmoja ambaye yumkini amechaguliwa na watu 400. Hao 400 wote hujawanunua halafu eti unategemea utauua upinzani kwa kumnunua huyo mmoja tu na kuwaacha hao 400 wakiwa na hasira ya kusalitiwa na kiongozi wao.. sasa mkuu hiyo ni nini?!!!! badala ujenge chama kwa hoja na utekelezaji wa ilani wewe unakazania kununua binadamu?!!!!
Mkuu mimi nilikuuliza hayo kutokana na hoja yako hii.
watu wameshindiliwa risasi, maiti ndani ya viroba zimeokotwa ufukweni, watu wametekwa, wamepotezwa, wamefungwa, wamefilisiwa...kwa hiyo wanaokandamizwa wakae tu kimya waseme hewala baba?!!
Nilikuuliza yote hayo kwasababu kwanza nilitaka utambue kuwa matendo ya utekaji, risasi, mauaji n.k hapa nchini hayakuanza leo yalikuwepo tangu muda mrefu na si serikali hii tu yanatokea. Pili nilitaka tu tuweke kumbukumbu sawa sawa kuhusu hawa tunao waita
watetezi wa demokrasia na haki za binadamu
swali je wameanza kufanya utetezi wakati huu tu? kwasababu matukio maovu yapo tangu siku nyingi au hawakuwa wanayaona ama hayakuwa na maana kwao kunyooshea vidole na matamko Kama wanavyofanya sasa?
Haya matamko yao wanayo yatoa kila siku ni ya kinafiki yenye lengo fulani nyuma ya pazia huku wakijificha kwenye kivuli cha haki za binadamu.
Angalia hiyo tweet hapo eti ofisi ya CHADEMA imepigwa Bomu!! Hivi kweli kabisa ofisi ya CHADEMA tena ya Kanda ipigwe bomu, yani mtu kabisa abebe bomu akalipue ofisi ya CHADEMA ya Kanda? Vitu vya ajabu kabisa hivi.
Alafu hao ccm ni wapumbavu kiasi gani hadi wafanye matukio Kama hayo ambayo wanajua kabisa yatawachafua alafu wakafanye kwa makusudi kabisaa? Siamini Kama ni wajinga kiasi hiki, alafu mara mbili mfululizo tukio la Arusha bado halijapoa wanatupiwa zigo la lawana na kupakwa matope alafu leo tena waende kuchoma nyingine mbeya? Kama ni hivyo basi huyu anae ratibu haya matukio ni mpumbavu wa kiwango Cha lami.
Kwa haraka haraka tutasema kuna masilahi yao yameguswa ndio mana wamekuwa wepesi sana kutoa matamko.
1 Unakumbuka tamko lao kuhusu shambulio la kigaidi masaki bila hata kushirikisha vyombo vya ndani kana kwamba wao ndio watawala wa nchi hii?
2 Unakumbuka matamko yao wakilazimisha Tanzania Kuna Ebola tena wakataja na hospital ya temeke Kuna mtu kafa kwa Ebola?
3 Unakumbuka matamko lukuki wakati wa Corona?
Uhalali wa wao kufanya vitu kama hivi wanaupata wapi?
Upouliza kuwa tutajibu nini kwa MUNGU hapa maana yake ni kwamba unatoa tuhuma kuwa wauaji ni hawa walio madarakani.
Sasa hebu lete tukio moja lenye ushahidi usio shaka kuwa muuwaji ni fulani (namaanisha ushahidi na sio fulani alisema au alitoa tuhuma kuwa wauaji ni serikali), unaweza kuleta ushahidi wa angalau tukio moja?
Kama ni kweli hawa watawala ndio wanaua sasa wale polisi, wanachama wa ccm na viongozi wa serikali kule kibiti waliokuwa wakiuawa kila kukichwa nani alikuwa anawaua? Kama muuaji wetu ni serikali inamaana walikuwa wanauana wenyewe kwa wenyewe?
Kuna tamko lolote kutoka ccm lililohusisha au kutuhumu upinzani kuhusika na mauaji yale?
Kuhusu hoja yako ya kununua upinzani kwa pesa za walipa kodi, hili nalo pia ni jambo la kufikirika mkuu halina ushahidi, au una ushahidi wa mmoja wapo aliye nunuliwa utuwekee hapa?
Unadhani kwamba hawa watu hawawezi kuhama kwa utashi wao tu, kwanini hutaki kuamini kuwa huo ni uchaguzi wao binafsi?
Unataka kuniambia kuwa wote waliopo CHADEMA wameridhika kabisa na kila kitu na kwamba kamwe hawawezi kuhama kwa maamuzi yao?
Kwahiyo na hawa wanao hama kutoka ccm kwenda CHADEMA vipi nao wamenunuliwa au ni maamuzi yao tu kwa kuto ridhishwa ndani ya ccm?
Kuna watu wamehama kutoka CHADEMA kwenda ACT mfano ni yule mbunge wa ubungo vipi nae ACT walimnunua sh ngapi?