OSEFUKANY
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 2,437
- 3,896
Mzee HIMARS vp, umeshamaliza ya Urussi sasa unataka kuja kuteketeza mashule huku nyumbani? Hahahaaa 😃 😃 😃 😀Wataje shule na walimu ili zibaki magofu
BTW hili suala limekuzwa na kutiliwa chumvi mno zaidi ya ukweli ulivyo. Watu wamelishabikia sana jambo ambalo ni Fununu/Tetesi kana kwamba wamefanya uchunguzi na kujiridhisha pasi na shaka kabisa kwamba watoto (wanafunzi) wanafundishwa mambo hayo ya kulawitiana. Mathalani kama inavyoonekana ktk picha iliyoambatanishwa: LGBT ni ufupisho wa Lesbian, Gay, Bisexual, and Transgender . Hiyo habari ya kufundishwa kulawitiana inatoka wapi? Je, si Haki ya mwanafunzi ajue na atambue kuna hali hizo katika jamii anamoishi na walioko miongoni mwa makundi hayo asiwanyanyapae (Stigmatize) ni watu kama yeye na wana Haki zao Kulindwa, Kuishi, n.k. halafu ajiepushe na Ushawishi wowote kujiunga au kujiingiza huko kwenye makundi hayo na akatae ushawishi wa namna hiyo ??. Mara nyingi tunavuna tulichopanda halafu baadaye tunaanza kulia-lia. Kwa mfano ulio wazi kabisa - Wazazi hawawaambii watoto wao mtoto anapatikanaje -wanawadanganya (wanaambia uongo) eti tumeenda kuomba kwa bibi, tumenunua Hospitali n.k. Baadaye Mtoto huyo-huyo anapocheza na wenzake au akiwa shuleni huko ndipo anapopata habari (ZA UKWELI) kuhusu dukuduku zake nyingi ambazo alifichwa na wazazi wake. (Samahani kama nitakuwa nimewakwaza baadhi ya wazazi, lakini ninaamini Waalimu (esp.Primary level) watanielewa)
Kwa msomaji yoyote atakayebahatika kupitia commenti yangu hii:- Niwaombe tu kwa roho nyeupe kabisa na kwa msisitizo, Jamani tuache UNAFIKI narudia tena TUACHE UNAFIKI kwani tukatae -tukubali hayo makundi tajwa hapo juu YAPO na YATAENDELEA kuwepo na labda YATAONGEZEKA muda tunavyoendelea. Kwani nyie mnaoyazungumza hayo mliyajuaje na hata mmefikia mahali pa kuwatambua tena kwa majina na mahali wanapoishi?. Umshukuru Mungu wako kwamba wewe sio miongoni mwao na mwanao pia hajajiunga huko. Lakini usiwanyooshee kidole, Kuwabeza, Kuwahukumu au Kuwalaani waliomo humo.
Shida iliyopo kwa sasa hapa e.g. Tz ni kwamba makundi hayo hayajatambulika na Serikali au Kurasimishwa (kitu ambacho kitapelekea Kuwekwa Sheria ya Kuwalinda na Kuwahifadhi) japo Yapo lakini kwa KIFICHO.
Nipo hapa jamani ni Ruksa kunikosoa ila niombe tu matusi na jazba zisiwepo. Nitajitahidi kukujibu kadri nitakavyojaliwa. Haya kazi kwenu. Asanteni