Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Hii ni hatua nzuri na kubwa sana kwa watanganyika, inaonesha vile tukiamua kupigania jambo kwa umoja wetu, hayupo yeyote wa kutushinda.

Sasa kwa hatua hii, ndio inathibitisha bila shaka, ule mkataba kati ya serikali na DPW ni haramu, haufai kuachwa uendelee kuwepo kwasababu umevunja sheria zetu za ndani.

Natumai hatua ya mwisho itakuwa ni kuuvunjilia mbali ule mkataba haramu hii ni kazi ya serikali ya Samia, hata kama akiendelea kuziba masikio lazima auone na kuufanyia kazi ukweli, lazima serikali yake iheshimu sheria zetu za ndani.

Mwisho kabisa, kwa bunge kukataa kupitisha ile sheria, imeonesha mhimili wa bunge umeidharau mahakama kuu, ambayo ilitoa mapendekezo kwenye hukumu yake ikilitaka bunge likafanye marekebisho ya sheria ili kuendana na ubovu wa ule mkataba wa bandari.

Hii maana yake kwa upande mwingine ni kwamba, sasa inajulikana rasmi, mahakama kuu kanda ya Mbeya ilithibitisha kwenye hukumu yake kwamba ule mkataba wa bandari ni mbovu, na wapeleka maombi ndio walishinda ile kesi.

Pongezi ziende kwa wote waliopinga na wanaoendelea kuupinga ule mkataba wa hovyo wa bandari, likiwemo Kanisa Katoliki kupitia waraka wake, ambao sasa nguvu zake zinathibitika mpaka bungeni, wanasheria, na wengine wote wenye kuitakia mema Tanganyika yetu.
💪🏻💪🏻✅
 
Wasalaam ndugu zangu Watanzania!

Bunge leo limekataa kupitisha mabadiliko ya sheria 2 ambazo zilikuwa zinakinzana mkataba tata kati ya Tanzania na Dubai.

Binafsi niliwasilisha maoni yangu kwa kupinga mabadiliko haya ya sheria kwa kamati ya Bunge kupitia email yao.

- Nimewasilisha maoni yangu kupinga marekebisho ya sheria ya ulinzi wa rasimali za Taifa

Tukumbuke sheria hizi mbili zilitungwa 2017 baada ya migogoro mikubwa ya madini katika awamu ya 5.

Pia Kuna Rufaa inasubiliwa kusikilizwa rasmi na kutolewa uamuzi, ukiliangalia maamuzi ya Bunge leo unapata picha kabisa kuwa Mahakama Rufani itawapa ushindi mkubwa wananchi kwa kusema wazi kuwa Dubai haikuwa na hadhi ya kusaini IGA na Tanzania, pia itasisitiza kuwa mkataba ulikiuka sheria zetu na hivo mkataba huu batili na hivo kuipa nguvu Serikali ya kwenda kuvunja rasmi mkataba huu tata.

Watanzania wameshinda. Watanganyika tumeshinda.
Na Lord Dening alipeleka pia anasema.
 
Sasa hivi vinatuhenyesha mahakama ya mikata ya Kimataifa, au huelewi hilo? Mikataba ya magu na kabudi kibao ina kesi huko, na mengine tumeshaanza kuilipa. Na mengine ndege zilishashikw, mama kaipigania.

Msisifie ujinga.
Tunacholipia siyo mikataba bali ni fidia zilizotokana na kuvunja mikataba ya kihawayawani kama huu wa Dp world
 
Hapo ndipo Watanzania mnazidi kudhihirisha ujinga wenu. Kujifanya mnajuwa kumbe hamjuwi.

Hivi bandari toka lini ikawa ni mali asili? Bahari na vilivyomo baharini ndiyo mali asili, siyo bandari. Bandari iwe baharini iwe nchi kavu ni kitu kinachojengwa na watu.

Kujidai ku dramatize kumbe unaongelea vitu viwili tofauti, halafu hapo hapo umeshajifanya Jaji wa mahakama ya rufaa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Wewe bibi ndie mjinga usiye na akili kabisa.

Hujui maamuzi ya mahakama kuu kanda ya Mbeya yaliagiza bunge likafanye marekebisha ya hiyo sheria, ili isikinzane na vipengele kwenye ule mkataba haramu wa bandari ambavyo vilikuwa vinalalamikiwa kuvunja sheria zetu za ndani.

Nyie mmezoea kuimba tu kumbe hata mnavyovipigia debe hamvijui, sasa kwa taarifa yako, hii hatua ya bunge ndio imethibitisha bila shaka kwamba ule mkataba kati ya serikali na bandari ni haramu, hapa ndipo utaitambua nguvu ya TEC.
 
Inshort inafikirisha cos hakukuwa na mjadala zaidi spika kasema tunapinga marekebisho ya sheria yaliyowasilishwa na Serikali, wanaohafiki waseme ndiyo ikajibiwa ndiyo! kilichopo hapa Spika alikuja na hoja hiyo toka huko alikokuwa.
Maana yake Spika alikuja na maelekezo toka juu. Kuna igizo wanafanya hawa
 
Sasa hivi vipengele ulivyoweka vinamaanisha nini kwa uelewa wako?
Wewe chawa nimethibitisha ni mjinga usiyejitambua, hujui hata kile kilichozuiwa na bunge kina madhara gani kwenye ule mkataba wa hovyo wa bandari uliozoea kuupigia debe, hii hatua ya bunge leo ndio imekupoteza kabisa, imeonesha kelele ulizozoea kupiga hazina maana.
 
Sasa hivi vipengele ulivyoweka vinamaanisha nini kwa uelewa wako?
Kama umesoma hivo vingere ukaelewa na ukasoma ule mkataba ukaelewa na ukarejea maamuzi ya Mahakama Kuu kanda ya Mbeya kuwa ni kweli IGA inakiuka sheria yetu ya ulinzi wa rasimali za Taifa ila hatuwezi kubatilisha Mkataba huu sababu kuna nafasi ya kufanyia marekebisho basi we utakuwa kilaza.
 
Wewe chawa nimethibitisha ni mjinga usiyejitambua, hujui hata kile kilichozuiwa na bunge kina madhara gani kwenye ule mkataba wa hovyo wa bandari uliozoea kuupigia debe, hii hatua ya bunge leo ndio imekupoteza kabisa, imeonesha kelele ulizozoea kupiga hazina maana.
Ngoja nikuthibitishie ulivyo mjinga

Niambie tangu lini uwekezaji kwenye Bandari ukawa suala la maliasili?
 
Ngoja nikuthibitishie ulivyo mjinga

Niambie tangu lini uwekezaji kwenye Bandari ukawa suala la maliasili?
Hili swali la kitoto kawaulize wale majaji wa mahakama kuu Mbeya kwanini waliliagiza bunge likafanye marekebisho ya hiyo sheria, huku mpuuzi wewe ukishangilia kwamba serikali ilishinda ile kesi.

Chawa hujawahi kuwa na akili.
 
Hili swali la kitoto kawaulize wale majaji wa mahakama kuu Mbeya kwanini waliliagiza bunge likafanye marekebisho ya hiyo sheria, huku mpuuzi wewe ukiahangilia kwamba serikali ilishibda ile kesi.
Umejiona ulivyo mjinga?
Ndo ujue mimi sio level zako!
Wapi Majaji walisema Bunge likafanye marekebisho ya Sheria ya Maliasilia?
 
Leo bungeni serikali imefuta marekebisho yote iliyopendekeza ya sheria ya maliasili za Taifa ambayo yangewezesha IGA baina ya Tanzania na Dubai kuanza kuendesha bandari zetu.

Hakika nguvu ya umma dhidi ya serikali dhalimu imeshinda na mapambano yaendelee kuhakikisha hata IGA yenyewe inafutwa!
 
Wasalaam ndugu zangu Watanzania!

Bunge leo limekataa kupitisha mabadiliko ya sheria 2 ambazo zilikuwa zinakinzana mkataba tata kati ya Tanzania na Dubai.

Binafsi niliwasilisha maoni yangu kwa kupinga mabadiliko haya ya sheria kwa kamati ya Bunge kupitia email yao.

- Nimewasilisha maoni yangu kupinga marekebisho ya sheria ya ulinzi wa rasimali za Taifa

Tukumbuke sheria hizi mbili zilitungwa 2017 baada ya migogoro mikubwa ya madini katika awamu ya 5.

Pia Kuna Rufaa inasubiliwa kusikilizwa rasmi na kutolewa uamuzi, ukiliangalia maamuzi ya Bunge leo unapata picha kabisa kuwa Mahakama Rufani itawapa ushindi mkubwa wananchi kwa kusema wazi kuwa Dubai haikuwa na hadhi ya kusaini IGA na Tanzania, pia itasisitiza kuwa mkataba ulikiuka sheria zetu na hivo mkataba huu batili na hivo kuipa nguvu Serikali ya kwenda kuvunja rasmi mkataba huu tata.

Watanzania wameshinda. Watanganyika tumeshinda.
Bravo Kwa watanganyika wote
 
Back
Top Bottom