Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii Nchi inataka mtu makini kama Rostam awe Waziri Mkuu.
Vingine vyakucha, huu mradi umesimama kitambo sanaMradi wameufisadi hadi umewashinda. Duh hii awamu in balaaa
bahati mbaya ? unauhakika?Hapana.jpm alitaka kuwashughulikia walioufisadi bahati mbaya akatutoka.kwa sasa mafisadi wamerudi na wanataka wajiuzie wao ili waendeleze kunufaika hao mafisadi
Mkuu Prince Kunta , siku hizi ni mambo ya online, kila kitu ni hapo ulipo na simu janja yako!.Ndugu mkurugenzi, PPR ikiingia kwenye real estate naomba usiniache katika ufalme wako
Hizi nyumba zisiuzwe kiholela kuna hatari ya kumaliziwa chini ya viwango.Purchasing power ya Wa Tanzania ni ndogo sn especially kwenye really Estate kupata muwekezaji DEGE ni ndoto ya asubuhi wewe Tazama tu palm village wanavyo hangaika kuuza apartments zao ndio utajua soko lipoje Tz mifano ipo mingi tizama yale majengo ya PSPF asilimia kubwa yapo wazi Tena City center huko ni Mji kama umekufa kabisa.
Tukumbushe kidogo, hizo spana zilikuwaje?JK. JPM (rest in eternal peace) ndo alikuja kugundua ufisadi akapiga spana.
View attachment 2398070
Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.
Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.
Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.
“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.
Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.
Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:
Inauma sana kuona jinsi pesa za wastaafu zilivyoteketezwa hapo. Ni matrilioni ya pesa. Hii ndiyo chanzo cha wastaafu wa Tanzania kulipwa pensheni ndogo sana ukilinganisha na nchi zingine za East Africa. Tunapitwa hadi na Burundi kwa kuwa na kikokotoo kisichokidhi maisha ya wastaafu. Pesa itakayopatikana kwenye uuzaji huo iende kuboresha pensheni ya wastaafu.00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.
View attachment 2398094
Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Naoana umielewa tofauti sijasema ziuzwe kiholela nilicho kisema uwezo wa WATANZANIA wa kununua upo chini sn kununua nyumba ambazo tayari zimeshajengwa hii miradi ya aina hii imefeli vibaya hapa TANZANIA.Hizi nyumba zisiuzwe kiholela kuna hatari ya kumaliziwa chini ya viwango.
Huu mradi ni muhimu kwa kuupendezesha Dar-es-salaam.
TPDC,City Council, NHC,TIB,TPA,washirikiane kuujenga na kuendesha mradi huu kwa maslahi ya umma.
Anaweza akapita nalo hiliHii Nchi inataka mtu makini kama Rostam awe Waziri Mkuu.
Kweli tupu, mtu anaona bora akanunue kiwanja aanze kujenga na kama wanapesa ndio watahamia nyumba ikiisha, wenye uwezo mdogo anahamia kwenye nyumba bado haijaisha.Purchasing power ya Wa Tanzania ni ndogo sn especially kwenye really Estate kupata muwekezaji DEGE ni ndoto ya asubuhi wewe Tazama tu palm village wanavyo hangaika kuuza apartments zao ndio utajua soko lipoje Tz mifano ipo mingi tizama yale majengo ya PSPF asilimia kubwa yapo wazi Tena City center huko ni Mji kama umekufa kabisa.
Kwa hiyo alishindwa kuwashughulikia kwa miaka 5 yote.
Majengo yalitelekezwa hadi nilipokuwa nikipita nashangaa inakuaje mradi umeshatumia mamilion ya pesa umefika pale halafu majumba yanaachwa tu
Wajenzi walikua waturuki, mwendazake kawatimuaSio tu kutekelezwa, yaani vifaa vyote mule kama magari, sijui vifaa vya ujenzi nk vimeibiwa karibia vyote
Watu ambao mlipambana na magufuri akawashinda mnawakati mgumu sana aiseee.Ni awamu ya mwendazake sio hii
Ongezea neno "mentality" hapo mkuu.Rich Daddy, Poor Daddy
Nyie si ndo wale mnayemuona seth na rugemalira mashujaa baada yakutoka gerezani.Muda mrefu huku majengo yanaoza na kushuka thamani? Muda mrefu kiasi gani? Maana hata aliunda mahakama lakini hakuna fisadi lolote tuliwahi kusikia limepelekwa huko kwa miaka yote 5.
Tatizo huo mradi siasa iliingia kati,, walianza chadema wakaupiga vita sana hadi kuulegeza, alipokuja jpm akawa kawasikiliza wapinzani kama alivyosikiliza suala la wapinzani juu ya babu seya, gesi mtwara, PAP, etc,, mradi ukadoda,,Acha porojo wewe...
Yaani since 2016 hadi 2020 bado tu "alitaka kuwashughulikia"?!
Btw, kama ambavyo aliwahi "kumshughulikia" mnene yupi serikalini na taasisi zake?!
Na kama alitaka kuwashughulikia kwavile aliona kuna ufisadi, ilikuaje tena DG wa NSSF akampa Ubalozi na kumpeleka Malaysia?!
Hivi mtaendelea kudanganyana hadi lini?!
Magu HAKUWA na guts za kushughulikia watu wazito... yeye aliishia ku-deal na civil servants tu tena wale ambao hawajafikia ministerial level.
Ukiondoa hao, gut yake nyingine ilikuwa kwa BAADHI tu ya Wafanyabiashara manake watu kama Rostam Azizi aliendelea kugonga nao cheers kama kawaida!!