Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Hii Nchi inataka mtu makini kama Rostam awe Waziri Mkuu.
 
PENDEKEZO KWA MAMLAKA ZOTE, WADAU PAMOJA NA IDARA YA MIPANGO MIJI HALMASHAURI YA KIGAMBONI

Miradi hii iliyotelekezwa ipo dunia nzima, na ni chamgamoto. NSSF, wadau wake na serikali watulie wasikurupuke wajifunze wengine walijikwamua vipi kutoka changamoto hii.

Mfano Sarot Group ya Turkey wameajiri wapiga mnada wanaoogea lugha zaidi ya nne za kimataifa kuweza kuwafikia wanunuzi wa kimataifa pia wanashirikiana na manispaa kuhakikisha maeneo ya jirani yapangike ki mpango mji.

Hii itavutia wanunuzi na ujenzi wa majumba mengine katika eneo kubwa jirani mfano Dege Kigamboni manispaa iandae mpango mji kupatikane eneo kubwa kuliko la Upanga jijini Dar huko Kigamboni utakaobeba Dege Eco Village na eneo la mji mpya la Upanga ya Kigamboni badala ya Dege Eco Village kuzungukwa na vibanda vya uswahilini siku za usoni hii itavutia uwekezaji mkubwa wa maghorofa eneo hilo la Kigamboni.



Amid a real estate crisis in Turkey, nearly 1,000 construction companies have gone bankrupt in less than a year. Before the start of the economic downturn, millions of dollars had been pumped into luxury housing projects across the country. In the western Anatolia region lies a stark symbol of this crisis: a ghost town with hundreds of abandoned Renaissance-style villas. Our colleagues from France 2 report, with FRANCE 24's Maud Jullien.
Source : France 24
 
Purchasing power ya Wa Tanzania ni ndogo sn especially kwenye really Estate kupata muwekezaji DEGE ni ndoto ya asubuhi wewe Tazama tu palm village wanavyo hangaika kuuza apartments zao ndio utajua soko lipoje Tz mifano ipo mingi tizama yale majengo ya PSPF asilimia kubwa yapo wazi Tena City center huko ni Mji kama umekufa kabisa.
Hizi nyumba zisiuzwe kiholela kuna hatari ya kumaliziwa chini ya viwango.
Huu mradi ni muhimu kwa kuupendezesha Dar-es-salaam.
TPDC,City Council, NHC,TIB,TPA,washirikiane kuujenga na kuendesha mradi huu kwa maslahi ya umma.
 
2017 Real Madrid Football Player Visit to Dege Eco Village

 
View attachment 2398070

Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.

Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.

“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.

Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.

Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:
00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.

View attachment 2398094

Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Inauma sana kuona jinsi pesa za wastaafu zilivyoteketezwa hapo. Ni matrilioni ya pesa. Hii ndiyo chanzo cha wastaafu wa Tanzania kulipwa pensheni ndogo sana ukilinganisha na nchi zingine za East Africa. Tunapitwa hadi na Burundi kwa kuwa na kikokotoo kisichokidhi maisha ya wastaafu. Pesa itakayopatikana kwenye uuzaji huo iende kuboresha pensheni ya wastaafu.

Serikali ihakikishe NSSF na taasisi zingine za serikali zinajikita kwenye kazi zake za msingi zilizobainishwa kwenye uanzishwaji wake. NHIF imefilisika kwa sababu hizi hizi za kujikita kwenye miradi ya ujenzi badala ya kulipia gharama za matibabu za wanachama wake. Imebidi kuanzishwe mfuko mwingine wa bima ya afya kwa wote ambao mjadala wake hadi sasa ni pasua kichwa kwani nao unaweza kuja kujikita kwenye maujenzi! Kila mtu anajua kuwa kwenye maujenzi ndiko kwenye upigaji mwingi.
 
Hizi nyumba zisiuzwe kiholela kuna hatari ya kumaliziwa chini ya viwango.
Huu mradi ni muhimu kwa kuupendezesha Dar-es-salaam.
TPDC,City Council, NHC,TIB,TPA,washirikiane kuujenga na kuendesha mradi huu kwa maslahi ya umma.
Naoana umielewa tofauti sijasema ziuzwe kiholela nilicho kisema uwezo wa WATANZANIA wa kununua upo chini sn kununua nyumba ambazo tayari zimeshajengwa hii miradi ya aina hii imefeli vibaya hapa TANZANIA.

Nenda AVIC TOWN wana mradi kama huu sijui kama hata asilimia 20% ya nyumba wameuza nyumba zipo wazi nyingi na ndio Kabla ya YANGA ipo huko , NHC umeitaja hapo wenyewe kama shirika tu wanapumulia mashine unataka uwape mzigo mwingine siwatakufa kabisa.
 
Purchasing power ya Wa Tanzania ni ndogo sn especially kwenye really Estate kupata muwekezaji DEGE ni ndoto ya asubuhi wewe Tazama tu palm village wanavyo hangaika kuuza apartments zao ndio utajua soko lipoje Tz mifano ipo mingi tizama yale majengo ya PSPF asilimia kubwa yapo wazi Tena City center huko ni Mji kama umekufa kabisa.
Kweli tupu, mtu anaona bora akanunue kiwanja aanze kujenga na kama wanapesa ndio watahamia nyumba ikiisha, wenye uwezo mdogo anahamia kwenye nyumba bado haijaisha.

Nyumba za miradi ni gharama halafu zina riba inayotisha kuisikia tu masikioni mtu anaogopa
 
Kwa hiyo alishindwa kuwashughulikia kwa miaka 5 yote.
Majengo yalitelekezwa hadi nilipokuwa nikipita nashangaa inakuaje mradi umeshatumia mamilion ya pesa umefika pale halafu majumba yanaachwa tu

Sio tu kutekelezwa, yaani vifaa vyote mule kama magari, sijui vifaa vya ujenzi nk vimeibiwa karibia vyote
Wajenzi walikua waturuki, mwendazake kawatimua
Sasa Sijui watawarudisha au watatafuta mkandarasi mwingine
Bifu zao Binafsi zinaumiza wengine
 
Sielewi elewi hapa. Sisi wakazi wa kigamboni tunajua huo ni mradi wa mwarabu mmoja anaitwa Akbar, alikuwa anaujenga huo mradi. Inasemekana aliutekeleza mara baada ya Magu kuingia madarakani sababu ulikuwa wa michongo michongo ming na huyo mwarabu alishawahi kukwaruzana na magu wakati akiwa waziri. Leo hii ndio tunshangaa kuambiwa kuwa ni wa serikali mweh
 
11 December 2014

Jakaya Kikwete afafanua ukubwa wa mradi huu

Watu 28,000 wanaweza kuishi katika maghorofa haya ya Dege Eco Village ...


Source : Dege Eco Village
 
Muda mrefu huku majengo yanaoza na kushuka thamani? Muda mrefu kiasi gani? Maana hata aliunda mahakama lakini hakuna fisadi lolote tuliwahi kusikia limepelekwa huko kwa miaka yote 5.
Nyie si ndo wale mnayemuona seth na rugemalira mashujaa baada yakutoka gerezani.
 
Acha porojo wewe...

Yaani since 2016 hadi 2020 bado tu "alitaka kuwashughulikia"?!

Btw, kama ambavyo aliwahi "kumshughulikia" mnene yupi serikalini na taasisi zake?!

Na kama alitaka kuwashughulikia kwavile aliona kuna ufisadi, ilikuaje tena DG wa NSSF akampa Ubalozi na kumpeleka Malaysia?!

Hivi mtaendelea kudanganyana hadi lini?!

Magu HAKUWA na guts za kushughulikia watu wazito... yeye aliishia ku-deal na civil servants tu tena wale ambao hawajafikia ministerial level.

Ukiondoa hao, gut yake nyingine ilikuwa kwa BAADHI tu ya Wafanyabiashara manake watu kama Rostam Azizi aliendelea kugonga nao cheers kama kawaida!!
Tatizo huo mradi siasa iliingia kati,, walianza chadema wakaupiga vita sana hadi kuulegeza, alipokuja jpm akawa kawasikiliza wapinzani kama alivyosikiliza suala la wapinzani juu ya babu seya, gesi mtwara, PAP, etc,, mradi ukadoda,,
Hakuna mtu anakubali kuwekeza mahali kusiko na stability🤗
 
Back
Top Bottom