Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

vijana jitoleni kwa wingi serikali nyenyekevu itaweka mkono wake wacheni kulalama
 
@HIMARS
 
Muda atakaotumia kujiendeleza hataweza kuwakumbatia watoto, yeye hafanyi kazi ya unesi ila yeye ni inkyubeta ya muundo wa binaadamu, ni vigumu kuamini kuwa wote walioko serikalini ni wasomi, yeye aajiriwe kwenye mfumo wa kazi maalumu tu kwa kuwa mnamuhitaji kwani hakuomba kazi.
 
Anaweza kuwekewa utaratibu.
Siku 3 kwa wiki darasani na zingine awe na watoto.
Ijulikane sio lazima awakumbatie wote.
Target iwe angalau kwa wiki aokoe mtoto mmoja au hata mwezi kwani sio kila siku huzaliwa njiti
 
Kutumia mtu badala ya incubators
Mkuu DR mkuu mwenyewe ndo amezengumza
Kwanza amesema shida sio INCUBATOR na wala hazipo chache
Shida ni vitanda vya mama watoto NJITI kulala hapo na mtoto kuwa ni vichache hii inafanya changamoto ya mama kuja na kurudi HOSPTARI kila siku sasa wazazi wengine wakienda siku mbili tatu wanatekeleza watoto hilo tatizo moja wapo

Pili kwa mujibu wa DR kumbatio la binadamu(kangaluu) lina matokeo CHANYA ya haraka zaidi kwa 100/% kuliko INCUBATOR

3 7bu iliyopelekea mpk huyo mdada kufanya hivyo alifika HOSPITAL kumuona rafikiye aliyejifungua ndo akapata taarifa kuna mtoto alitekelezwa kama sikosei au aliokotwa yupo kwenye INCUBATOR zaidi ya miezi 4 haongezeki Uzito
wkt wa majadiliano ndipo nesi mmoja akasema endapo angetokea mtu akamkumbatia anauhakika ndani ya wiki angeongezeka uzito na akatoka hapo hosptari
Ndipo huyo dada akajitolea kufanya Hvyo kwa wiki nzima na mtoto akaongezeka uzito akafikia LENGO la madaktari wenyewe walivyohitaji
Sasa baada ya hapo akaendelea na mishe zake ila akawaambia ikitokea kuna Kesi nyingine kama hiyo wasisite kumpigia
Ndipo zikatokea kesi kama hizo mbili akaziandle kwa mtindo huo huo mpk juzi gazeti lamwananchi ilivyopublish ushujaa wake

Ajakulupuka tu kufanya hvyo MADAKTARI wana akili na wanajua wanachofanya walihakikisha yupo na AFYA njema ya kufanya jambo hilo ili isiwe na hathali zozote kwa mtoto

Zaidi pengine lina athari kwake 7bu haijulikani watoto wana magonjwa gani yeye alichofanya ni kujitolea

Sasa dr kasema kuna wazazi wanawatekeleza watoto wakishaona ni watoto NJITI kwa kushinda hiyo kazi ya kangaluu sasa huyo dada wala sio watoto wake ni moyoni anajitolea kufanya hvyo na wala halipwi chochote zaidi MADR au MANESI kumpa msosi na nauri tu
Je huoni kama ni ushujaa na alisatahili PONGEZI na motisha ili kurudisha IMANI kwa jamii kuwa
HUMANITY STILL EXIT

Kwanza ushawahi kumuona mtoto NJITI nina uhakika kwa moyo wako hata anagekuwa MWANAO usingewez kumkumbatia inahitaji MOYO na USTAMIILIVU ndo mana wengi hutekeleza hao watoto




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…