Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

Naunga mkono hii, kwenda chuo tena mambo mengi, bora waangalie anapataje mafunzo maalumu ili alisimamie hilo, sio tena kumpeleka chuoni.
 
hivi yule majaliwa mkombozi wa wahanga wa ajali ya ndege ziwa victoria yuko wapi kwasasa
 
Sipingani na wewe,,,, nadhan hujanielewa nilichokua nakimaanisha....ni vizuri kama serikali imetambua mchango wake kwenye hilo...lakini pia inatakiwa waangalie namna ambavyo wanaweza wakaokoa maisha ya watoto wengine zaidi kupitia yeye,, kwa mfano wanaweza wakatangaza fursa kwa wamama wengine wengi zaidi wakapimwa afya zao ili kuepuka magonjwa ambukizi na kuwapa training fupi ya namna nzuri ya kutunza hao watoto njiti...kupitia hiyo tutaokoa maisha ya watoto wengi na kuwapa fursa pia wamama wenye mioyo ya kujitolea kama yeye....hope umenielewa vizuri sana😊🤗...na kingne wanasema changamoto ni vitanda vipo vichache na incubators zipo chache pia, wanaweza wakaanza na hivyo kwanza
 
NI kweli kabisa huko sahihi na hiyo njia imetumika tangu miaka ya 80 huko na mpk sasa nina ushahidi ya watoto wawili niliwaona kwa macho yangu wawili wengine aliwazaa wote njiti lkn kipindi hicho milokuwa mdogo sina akili
Nikisema tangu miaka ya 80
7bu huyo mama mtoto wa kwanza alimzaa 85 njiti wa pili 88 njiti watatu 95 njiti wanne 99 njiti na watatu 2007 njiti
Sasa huyo wa 99 na 2007 niliwashihudia 7bu akili timamu nilikuwa nazo sasa

Hvyo dadaangu humu wengi hawana akili hawajui nino wanachangia hvyo kwa swala alokuwa analifanya huyo DADA ni zaidi ya USHUJAA 7bu niliwaambia hao wanaopinga kwanza hawaju mtoto NJITI yupoje kimuonekano na kiumbo kama wangejua nina uhakika wasingeongea ujinga wao huo

Jambo la ziada kwa sasa kwa SEKTA YA UZAZI serikali imepiga hatua sana katika lengo la kupunguza VIFO VYA WATOTO WACHANGA kwa kiasi fulani wameviepusha kwa 80%
Hatua hii imeongezeka zaidi baada ya KUJENGA WODI mpya hizi za kisasa kwa HOSPTARI ZA AMANA TEMEKE NA MWANANYAMALA sijajua hali ya MIKKOANI ipoje ila kwa DSM wamejitahidi sana
 
Hizo nguvu si wangewekeza kwenye kununua incubators za kutosha.

Wabongo wapo busy kutetea Dp kisa inatumia mashine lakini wapo busy tena kumpongeza Rais kwa kutoa pesa za kukumbatia watoto badala ya kushauri zinunuliwe mashine za kutosha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Itakuwa wanataka watanzania tujazane hospital tukakumbatie watoto.

Nchi ngumu hii[emoji1787]
Ili mradi tu wawatoe watu kwenye reli.
 
Naunga mkono hii, kwenda chuo tena mambo mengi, bora waangalie anapataje mafunzo maalumu ili alisimamie hilo, sio tena kumpeleka chuoni.
Nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Waziri akijiamulia baadae likatokea tatizo ataingia matatizoni. Kama binti ana miaka 25 asisite kwenda shule ili apate ajira kirahisi kwa sababu pia inaonekana hana ajira ndo maana kaweza kufanya hilo zoezi.
 
Safi. Tunapongeza panapostahili na kukosoa panapostahili.
Incubators ni vile tunaishi dunia ya usasa na changamoto nyingi ndani yake, lakini joto la mama ni zuri. Naamini wamechukua hatua stahiki upande wa afya ya mwanadada anayefanya zoezi hilo maana ndiyo la muhimu kwa afya ya watoto wasipate maambukizi yoyote yale kutoka kwake.
 
Kutumia mtu badala ya incubators
Halafu litakuja kutokea janga, wote watamruka watadai utaratibu haukufuatwa, kama yule muosha vifaa. Yaani ccm ni balaa kwa Tz!
 
Ni wachache sana watakuelewa!
Kwa kifupi mtoto njiti hajakomaa hii ni pamoja na kinga pia.
Sitaki kwenda mbali kuhusu tahadhari za kuzuia magonjwa kutoka kwa huyu mama kwenda kwa hao njiti kama zinafuatwa.
Anyway twende tu..
Kwamba amana hawajui Hilo Ila wewe mkulima wa pilipili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…