Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Kwa sasa wacha wazuie pale wanapoweza huku wakitafuta njia mbadala ya kudhibiti huko kwenye blogs and websites.
At least wameanza kuchukua hatua
Hivyo vitabu havina chochote cha kufanya serikali izuie, wameona fake version zilizowekwa mitandaoni tu.

Hili jambo linaifanya Wizara ya Elimu iende kuwa kichekesho cha dunia.

Watanzania wengi, pamoja na Wizara yao ya Elimu, ni wepesi sana wa kuhukumu mambo kabla ya kuyachunguza.

Mmeshindwa kuzuia watoto wasicheze Singeli na vigodoro Uswahilini, mnakuja kushadadia vitabu ambavyo hata hamjavisoma?
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 59 cha sheria ya Elimu, Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada kutumika katika shule za umma na binafsi nchini.

Prof. Mkenda ameyasema hayo jijini Dodoma ambapo amevitaja vitabu hivyo kuwa ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

"Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
 
Kwani wewe wasema je? Hivyo vitabu viwachwe? Wewe hujui mamlaka na wajibu wa wizara ya elimu au unabisha kwabb unamiliki simu janja.
nataka katazo lenye nguvu ya kisheria, sio tamko la desturi na utamaduni wa waziri.

wapo watu wamefukuzwa kwenye taasisi zao kwa sababu walipofuata taratibu za kikatiba kujaribu kumuondoa kiongozi waliyeona hafai tena waliambiwa wamekiuka mila, desturi na tamaduni za taasisi. Ambazo hazijaandikwa mahala.
 
Serikali ya Tanzania imeingia mkenge kukubali fake news ya "Diary of a Wimpy Kid" kilichobadilishwa na wahafidhina na kusambazwa Whatsapp...
Wizara Ina muda wa kufanya uhakiki? hapo ni kukurupuka tu na kupiga marufuku kabla Mambo hayajawa sio Mambo.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini...
Safi kabisa, wamagharibi wanatumia nguvu kubwa mno kwa kushirikiana na vibaraka wao kupandikiza "mbegu mbaya" kwa watoto wa kiafrika. Tusipokuwa makini tutakuja kuwa na jamii ya ovyo sana baadae.

Wazazi tujitahidi kukagua vitabu na madaftari ya watoto wetu kila tupatapo nafasi.
 
Vinatolewa bure na mashirika ya magharibu hususani kutoka Marekani, wengi kujifanya watumishi wa kikuristo wanatoa kama msaada, kagueni ma begi yawatoto wenu, wasiengie kwenye hilo dimbwi la ushoga
Acha upumbavu wewe, Mtumishi yupi wa kikristo aliyewahi kukupa au kumpa mwanao msaada wa kitabu cha ushoga!? Hao waarabu wanaofukunyua mitaro ya dada zenu walipewa vitabu na nani!? Chuki ikizidi huzaa ujinga.
 
Vinatolewa bure na mashirika ya magharibu hususani kutoka Marekani, wengi kujifanya watumishi wa kikuristo wanatoa kama msaada, kagueni ma begi yawatoto wenu, wasiengie kwenye hilo dimbwi la ushoga
Series pia mzifungie, premier league pia wasiangalie maana Ina support LGBT, pia wasiangalie cartoon za nje, pia miziki wasiangalie, kiufupi huwezi zuia kitabu ukaachia series, miziki, na google!!

Badala wafundishe watoto ubaya wa mambo wao wanaficha taarifa kabisa mwisho wa siku watoto Wanaenda tafuta uncontrolled knowledge huko Mitandaoni!!
 
Safi kabisa, wamagharibi wanatumia nguvu kubwa mno kwa kushirikiana na vibaraka wao kupandikiza "mbegu mbaya" kwa watoto wa kiafrika. Tusipokuwa makini tutakuja kuwa na jamii ya ovyo sana baadae.
Wazazi tujitahidi kukagua vitabu na madaftari ya watoto wetu kila tupatapo nafasi.
Mtoto Gani anasoma vitabu Tanzania? Mbona google hawafungii au premier league wanaopromote kabla ya Kila mechi? Double standards haiwezi tusaidia kitu.
 
Series pia mzifungie, premier league pia wasiangalie maana Ina support LGBT, pia wasiangalie cartoon za nje, pia miziki wasiangalie, kiufupi huwezi zuia kitabu ukaachia series, miziki, na google!!

Badala wafundishe watoto ubaya wa mambo wao wanaficha taarifa kabisa mwisho wa siku watoto Wanaenda tafuta uncontrolled knowledge huko Mitandaoni!!
Hivyo vitabu ukitafuta hutakuta hayo maudhui maana nimejaribu google sana ila sijayaona.

Wizara ilitakiwa ioneshe hivyo vitabu na picha zilizomo
 
Mtoto Gani anasoma vitabu Tanzania? Mbona google hawafungii au premier league wanaopromote kabla ya Kila mechi? Double standards haiwezi tusaidia kitu.
Kwa kuvizuia hivyo vitabu angalau serikali imeonesha kuwajibika, hatuwezi kuacha huo uchafu uingizwe kwenye mfumo wa elimu ya watoto wetu eti kwakuwa google na EPL umeruhusiwa!

Kwani we unasemaje, viachwe viendelee kutumika?
 
Kwa kuvizuia hivyo vitabu angalau serikali imeonesha kuwajibika, hatuwezi kuacha huo uchafu uingizwe kwenye mfumo wa elimu ya watoto wetu eti kwakuwa google na EPL umeruhusiwa!
Kwani we unasemaje, viachwe viendelee kutumika!!??
Vitabu Gani vipo kwenye syllabus hapo? Nachosema kama mmeamua kuzuia content za magharibi basi muache vyote sio kuchagua Moja na kuacha njia zingine 10.

Mfano ukiskiliza bongo fleva 90% zinaimba kuchuma mchicha, kusafisha mtaro, Kwa mpalange n.k watoto wanaziimba bila kukosea verse unadhani ukiondoa vitabu pekee inasaidia?

Ushauri wangu ni kwamba watoto wafundishwe ubaya wa mambo hayo maana watayasikia tu at some point in life. Ila kuzuia haiwezekani maana mmeachia bongo fleva waimbe matusi hayo hayo mnayopinga kwa vitabu. And bongo fleva inasikilizwa zaidi kuliko vitabu kusomwa!!
 
Ondoa matopic magumu magumu au futa vitabu vyenye topic ngumu ngumu kama equlibrium, atoms, probability katika hesabu, cos, sin n.k

Vimepitwa na wakat havimsaidii mtu wala kijana wa sasa kumudu mazingira

Badala yake hizo topic lete vitabu vifuatavyo

1. Kilimo theory ichukue 10%

2. Kilimo practical 90%

3. Ufugaji theory 10%

4. Ufugaji practical 90%

5. Home decors

6. Welding, plumbing and irrigation system

7. Farm machineries Mechanics

8. Business practical (Biashara jwa vitendo)

9. Money ethics (Kanuni za fedha)

10. Self reliance (Elimu ya kujitegemea)

11. Nchi yako ni tajiri ulipo pana rasirimali nyingi sana Kuishi bila kutegemea Mikopo ya nje

Hicho cha 11 iwe core course kuanzia chekechea hadi PhD, Maana Ili tuendelee lazima mawazo ya utegemezi na utumwa yafutwe kwenye mind ya vizazi vyetu.
 
Habarini wana JF popote mlipo.

Jana moja ya habari zilizotawala kwenye mitandao na vyombo vya habari ni juu ya kuondolewa kwa vitabu 16 ambavyo haviendani na maadili ya kiTanzania.

Screenshot_20230214_015915_Instagram.jpg


Ndugu waziri, nidiriki kusema kwamba mti umeukata ili hali bado shina na mizizi haijatolewa.

Kwanini?
Hapa naongelea hii alphabet R ambayo katika mashule mengi hapa nchini wanaitumia kuwakilisha huu upinde wa mvua, au kwa kimombo ni Rainbow.

Konsonanti hii R haijapotosha uwakilishi huo wa upinde wa mvua, bali maana iliyo huko duniani na inavyotumika ndio kinyume cha maadili na tamaduni zetu.

images (1).jpeg

images (4).jpeg


Sasa niweke wazi maana na uwakilishi wa upinde wa mvua kwa tafasiri ya huko duniani kulinganisha na suala la vitabu 16 ulivyokataza.

Upinde huu wa mvua unasimama kama alama ya jumuiya ya watu wa jinsia moja wanaoshirikiana kimapenzi, [yani mwanamme na mwaname, au mwanamke na mwanamke]

Pili, washiri wa mapenzi wa jinsia zaidi ya moja na kwa mtu zaidi ya mmoja.

Tatu, Watu waliobadili jinsia aidha alikua mwanamke akajibadili kuwa mwanamme, au kinyume chake.
Hii alama aligundua Gilbert Baker baada ya kuombwa kubuni alama kwa ajili ya washiriki wa kimapenzi wa jinsia moja, ambapo Harvey Milk anaesadikiwa kuwa mshiriki wa kwanza kujitangaza waziwazi kufanya ivo mnamo miaka ya 1970.

Screenshot_20230214_015955_Instagram.jpg


How Did the Rainbow Flag Become a Symbol of LGBTQ Pride?

Swali langu linakuja, baada ya kutoa hivi vijitabu, Je watoto wetu bado wapo salama?
Jibu ni Hapana.

Hivyo basi ndugu Waziri mwenye dhamana, nikuombe umalizie hiki kisiki na mizizi yake ili kuondoa kabisa hili swala sio tu vichwani hata machoni ambapo ni njia ya kwanza ya mapokeo.

Naamini wewe ni kikngozi mweledi na mchapakazi, na hili sio jambo gumu kwako.
 
Hivyo vitabu havina chochote cha kufanya serikali izuie, wameona fake version zilizowekwa mitandaoni tu...
Binafsi naona hilo katazo ndio litasababisha vitabu hivyo kusomwa zaidi ili kujua nini tatizo lililosababisha vizuiwe.

Wangepita kwenye taasisi husika kutoa katazo kimykimya na kuwaelimisha sababu za katazo.
 
Back
Top Bottom