Habarini wana JF popote mlipo.
Jana moja ya habari zilizotawala kwenye mitandao na vyombo vya habari ni juu ya kuondolewa kwa vitabu 16 ambavyo haviendani na maadili ya kiTanzania.
Ndugu waziri, nidiriki kusema kwamba mti umeukata ili hali bado shina na mizizi haijatolewa.
Kwanini?
Hapa naongelea hii alphabet R ambayo katika mashule mengi hapa nchini wanaitumia kuwakilisha huu upinde wa mvua, au kwa kimombo ni Rainbow.
Konsonanti hii R haijapotosha uwakilishi huo wa upinde wa mvua, bali maana iliyo huko duniani na inavyotumika ndio kinyume cha maadili na tamaduni zetu.
Sasa niweke wazi maana na uwakilishi wa upinde wa mvua kwa tafasiri ya huko duniani kulinganisha na suala la vitabu 16 ulivyokataza.
Upinde huu wa mvua unasimama kama alama ya jumuiya ya watu wa jinsia moja wanaoshirikiana kimapenzi, [yani mwanamme na mwaname, au mwanamke na mwanamke]
Pili, washiri wa mapenzi wa jinsia zaidi ya moja na kwa mtu zaidi ya mmoja.
Tatu, Watu waliobadili jinsia aidha alikua mwanamke akajibadili kuwa mwanamme, au kinyume chake.
Hii alama aligundua Gilbert Baker baada ya kuombwa kubuni alama kwa ajili ya washiriki wa kimapenzi wa jinsia moja, ambapo Harvey Milk anaesadikiwa kuwa mshiriki wa kwanza kujitangaza waziwazi kufanya ivo mnamo miaka ya 1970.
How Did the Rainbow Flag Become a Symbol of LGBTQ Pride?
Swali langu linakuja, baada ya kutoa hivi vijitabu, Je watoto wetu bado wapo salama?
Jibu ni
Hapana.
Hivyo basi ndugu Waziri mwenye dhamana, nikuombe umalizie hiki kisiki na mizizi yake ili kuondoa kabisa hili swala sio tu vichwani hata machoni ambapo ni njia ya kwanza ya mapokeo.
Naamini wewe ni kikngozi mweledi na mchapakazi, na hili sio jambo gumu kwako.