Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Mila, desturi na tamaduni za Tanzania sio sheria.

Marufuku ya Waziri pia sio sheria.

Nchi inapaswa kuongozwa na utawala wa sheria.

Tunataka sheria.
Angukia katiba mpya moja kwa moja ndiyo utaeleweka kiurahisi.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

View attachment 2516384

Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda”

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
Kwa upande wa wazazi wa bongo ambao watoto wao wanagegedana vichochoroni majumbani mwao sidhani kama watahangaika na hili.
 
Hizo ndizo fake version nilizosema.

Watu wamelinganisha na vitabu halisi wakakuta hakuna vitu kama hivyo.

Kwa hiyo tumepiga marufuku vitabu kwa kuangalia fake news za Whatsapp?
Sorry mkuu. Hebu tuwekee ukurasa halisi
 
Hao watoto vitu wanavyojua hawajavisoma popote ila wanajua.

Tuulizeni na sisi wa vi tuition tuwaambie watoto wanayoyaongea
Wewe kama mzazi umechukua hatua gani kuwasaidia hao watoto? Au ulipo sikia umesikia unasubiria uje uulizwe halafu itasaidia nini?

Kumbe tunafanana na viongozi wetu,..... Vitabu viliruhusiwaje kuingia na kutumika bila kuangalia maudhui? Na alie ruhusu ni nani na anachukuliwa hatua gani kwa uharibifu aloufanya?
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

View attachment 2516384

Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda”

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
Hivyo vitabu vimeshawaharibu watoto wangapi
 
Inaumiza Sana.
Screenshot_20230214-051351.jpg

Watoto wanafundishwa uhuni tu
 
Prof. Mkenda anaweza kujitahidi sana kwa nafasi yake ila Taifa kama Taifa ikaruhusu huu Ushetani kwa kupitia Masharti ya Misaada

Ninakumbuka vizuri ile barua ya serikali kukanusha kupinga haya mambo baada ya Makonda kupinga tena serikali ilisema ule ulikuwa ni msimamo wa Makonda tu na sio wa serikali...UNAFIKI HUU

Serikali hasaa ndio ilipaswa ianze kupinga huu Ushetani na wote watakaoonesha kuasisi au kusupport wachukuliwe hatua kali.
 
Back
Top Bottom