Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Bora hata wangefuta topic ya circle kwenye maths, the earth as a sphere. Nilikuwa sizielewi. Tena bora hiyo sphere, circle sijawahi ielewa
Ni nyepesi Sana hizo mkuu, na zinakuwa applied Sana huku kwenye course za science hasa engineering.
 
Bado shida ipo kubwa. Serikali ina uwezo wa kufanya chochote ikiamua.

Mashoga wanajulikana hivi serikali ikiweka adhabu ya yeyote anaejitangaza mahusiani ya jinsia moja miaka 30 kifungo hili swala si lina weza kupungua sana?

Serikali ona mitandaoni mtu anajitangaza yeye ana mahusiano ya jinsia moja na hamsemi chochote?

Sawa hivo vitabu tunawashukuru kuzuia lakini hamjagusa sehemu ambayo ndo kichochezi cha upuuzi.

Mashoga na wasagaji washughulikiwe kwa vitendo sio kuweka tu sheria ambayo haina vitendo. Mtu akifungua acount kwenye social media ifungwe lakini pia wamiliki wa mtandao huo wapewe utaratibu kwamba mtu akiruhusiwa na mtandao wenu kufungua acount ya kuhamasisha upuuzi huo mtandao tunaufungia Tz.

Hivi hii haiwezekani? Tatizo hii nchi tegemezi sana. Ila mimi nadhani serikali ina uwezo wa kuwinda hawa wapuuzi na ikafanikiwa.

Mfano mzuri juzi kombe la dunia mbona waliweza kuzuia mashoga kuingia? Serikali mjitahidi nyinyi mna nguvu. Kizazi cha mashoga kina kuwa kwa kasi jamani eti nao wanafanyaga sherehe zao huko si ndo pa kuwawinda na kuwasweka ndani?
 
Hii vita viongozi njaa wa Tz hawaiwezi,hayo nimaigizo matupu,ushoga bongo hawawezi kuugusa,alishindwa jpm ataweza huyu mtembeza bakuli.
 
Wangeanza kwenye majamvi.

Wapunguze taarifa za Upotoshaji pia.

Kuna mijamaa humuhumu ningeyafungia, manake sumu zao ni kali na hasi sana. Yaani wako kinyume na Tamaduni na Maadili ya Kitanzania na Kiafrika kwa Ujumla...lugha mbofu mbofu/vu

Utanisamehe Usiyeonekana hali siyo nzuri hivyo humu.

Washirikiane na Makampuni kama JF, Twitter, Facebook Tiktok kuchuja maudhui hasi kwa Jamii.

Kazi iendelee

Naunga mkono Uamuzi.
 
Wanafuta vitabu watoto wanaangalia katubi zenye agenda ile ile.

Bado kuna movies na watoto hao hao kujua matumizi ya smartphone mapema.

It's more than that..

Hii ianzie katika ngazi ya familia kila mzazi asimame kikamilifu kwenye malezi ya watoto wake.
 
Wangeanza kwenye majamvi.

Wapunguze taarifa za Upotoshaji pia.

Kuna mijamaa humuhumu ningeyafungia, manake sumu zao ni kali na hasi sana. Yaani wako kinyume na Tamaduni na Maadili ya Kitanzania na Kiafrika kwa Ujumla...lugha mbofu mbofu/vu

Utanisamehe Usiyeonekana hali siyo nzuri hivyo humu.

Washirikiane na Makampuni kama JF, Twitter, Facebook Tiktok kuchuja maudhui hasi kwa Jamii.

Kazi iendelee

Naunga mkono Uamuzi.
Wewe huwezi kuchuja maudhui mwenyewe??
 
Wewe kama mzazi umechukua hatua gani kuwasaidia hao watoto? Au ulipo sikia umesikia unasubiria uje uulizwe halafu itasaidia nini?

Kumbe tunafanana na viongozi wetu,..... Vitabu viliruhusiwaje kuingia na kutumika bila kuangalia maudhui? Na alie ruhusu ni nani na anachukuliwa hatua gani kwa uharibifu aloufanya?
Umemaliza?
 
VITABU 16 VYAPIGWA MARUFUKU KUTUMIKA SHULENI, TAASISI ZA ELIMU

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye Shule na Taasisi zote za Elimu.

Vitabu hivyo vimepigwa marufuku na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 59 cha Sheria ya Elimu Sura ya 353.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Prof. Mkenda amesema kama taifa tuna mila na desturi za kufuata na katika kufundisha na kulea watoto na kwamba shule zina wajibu wa kuendana na taratibu hizo katika kuwaandaa watoto.

"Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,"amesema Profesa Mkenda

Amevitaja vitabu hivyo kuwa ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili. @ikulu_mawasiliano @ikulu_habari @wema.smz2020 @shuledirectkids @shuledirect @maelezonews @maelezozanzibar


USSR
 
Naona mjadala ni mkali sana. Lakini sijaona mahali mtu aliposhea mfano wa page kupitia vitabu vilivyotajwa hapo. Mfano kitabu namba fulani tajwa hapo juu ukifungua page yake ya 6 au 10 kina maudhui mabovu katika jamii.

Ni screenshot mbili nazo hazijaleta majibu sahihi.
 
SIvijui hivyo wimp kid ila 14,15 na 16 kweli walimu wanawafundishia wanafunzi? Like seriously??
 
Back
Top Bottom