Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Mbona wameruhusu mabasi saa nane na nusu usiku na hakuna tatizo. Ally's na Katarama walipokiuka masharti walifungiwa.
 
Mabasi ya Arusha-Kigoma yajiandae kutekwa kwenye msitu wa malagarasi.

Alafu Kampuni za Coast Line na Kiazi Kitamu mnakabidhi Basi kwa dereva mmoja kuendesha umbali mrefu kiasi hicho, tujiandae kuona mengi.
Utaratibu utatolewa kesho ya namna ya kusafiri. Halafu sio kila basi litasafiri usiku. Ni Kama Sasa Kuna mabasi yameruhisiwa kuondoka kuanzia saa tisa usiku. Ila siyo yote.
 
Tatizo watu hawafuatilii, wenyewe wanawaza ajali. Kuna mabasi yanatoka Mwanza mpaka Mbeya yanasafiri usiku kucha.
 
Ila watanzania tupo very negative. Tunawaza mabaya tu. Mbona mabasi yameruhisiwa kusafiri saa tisa usiku na hakuna shida. Tuangalir mambo chanya sio hasi pekee.
Kifo mkono bro nishawahi panda gari kutoka Kilimanjaro mpaka Iringa ile Gari tulienda kuzuiwa Mikumi tusiendelee na Safari tukalala pale Ila Gari yenyewe spana MKONONI matengenezo kila baada ya kilometers tulifika tumechoka balaa alafu vituko njiani vilikua vingi balaa, usije ukadhani unabishana na mtu ambae hasafiri usiku usiku una Mambo meusi meusi
mengi yaan Gari inabidi lioshwe na Holly water kabla ya Safari
 
Nakuelewa mkuu, pole Sana. Ila kwa utaratibu wa Sasa basi Kama Hilo halitasafiri usiku.
 

Mbona hapo Rwanda huwa tunasafiri usiku, kwanini iwe shida kwa Tanzania. Hapo Kenya tangu 1990 wanasafiri usiku mpaka Leo. Nadhani tuangalie uhitaji kuliko madhara. Halafu sio kila basi litasafiri usiku, ni baadhi tu.
 
Hii ni try n error inafanyiwa kazi hapa, come Dec utasikia wanasitisha coz ajali zimekuwa nyingi.

Mbona mabasi mengi yalianza safari za usiku. Kwa mfano Kuna mabasi yalianA safari kutoka Dar saa tisa usiku.
 
Nchi nyingi duniani usafiri wa umma ni 24hrs, sisi tuna nini cha tofauti na wengine!? Hata majirani zetu (Kenya & Uganda) usafiri ni 24hrs na bado tunawazidi kwa idadi ya matukio ya ajali! Toka nje ya box.

Nimegundua watanzania ni waoga Sana. Serikali imeruhusu usafiri wa masaa ishirini na nne, lakini watu wanawaza ajali.
 
Yaan unataka kusema Barabara za KE hazina utofauti na Barabara za TZ?

Basi subiria takwimu si zitaandikwa hapa hapa JF tu
Tujitahidi kutembea.
Kenya na Ug kama una passport yako nauli ni ya kawaida sana.
Huo ugonjwa wa kujichukulia poa na kudharau miundombinu yetu ni kwasababu hatutembei, tumejifungia ndani so tunahisi tuko nyuma kwa kila kitu!
Kwa taarifa yako EA hakuna nchi yenye miundombinu bora (barabara za kuunganisha mikoa) kama Tz.
 

Barabara za Tanzania ni nyembamba
 

Kesho LATRA watatoka utaratibu. Halafu kusafiri usiku itakuwa sio kila basi. Ni Kama Kilimanjaro Express yeye kaanza kusafiri usiku muda, rutinza Mbeya na Mwanza mabasi yanaondoka saa tisa kamili na hakuna ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…