Serikali kutoa ufafanuzi kuwa kuna makosa yalifanyika haiwezi kuisafisha ikulu kuwa imeoza.
Makosa yaliyofanyika yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.
Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii katika suala zima la kusoma na kutafsiri namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.
Kwa sababu point ya pili inaleta maana zaidi,hii maana yake ni kwamba Rais pamoja na wasaidizi wake hawajui kusoma na kuandika.Yaani tunaongozwa na mbumbumbu.