Serikali yatoa ufafanuzi wa akiba ya Fedha za Kigeni, makosa yalifanyika

Serikali inatoa taarifa kwa kila robo
 
Ikulu ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu akiba ya fedha za kigeni ambapo imesema Tanzania ina akiba ya fedha za kigeni Dola za Marekani Milioni 6,253 na sio Dola za Marekani Bilioni 6,253 "akiba hii inatosheleza kununua bidhaa na huduma kwa muda wa miezi 7

 
haya topic imeisha, tuanze topic nyingine sasa...cc Behaviourist .... tuendelea kuenjoy demokrasia..
Serikali kutoa ufafanuzi kuwa kuna makosa yalifanyika haiwezi kuisafisha ikulu kuwa imeoza.

Makosa yaliyofanyika yanaweza kuwa na maana moja kati ya maana hizi mbili.Kwanza inawezekana hotuba hii alieiandika hakuihariri kabisa na pia alipopewa Rais nae hakuihariri kabisa hadi anapanda hewani,kitu ambacho ni ngumu kuamini.

Lakini maana ya pili inawezekana kuwa wote wawili, yaani Rais pamoja na alieandika hotuba hii katika suala zima la kusoma na kutafsiri namba iliwapiga chenga.Yaani alieandika hotuba namba zilimchanganya akasema iende hivyo hivyo tuuu na Rais nae namba zikamchanganya akasema iende hivyo hivyo tuu.Hii inaleta maana zaidi kwa sababu kwa point ya kwanza ni ngumu Rais kusoma hotuba ambayo yeye mwenyewe hajaipitia.

Kwa sababu point ya pili inaleta maana zaidi,hii maana yake ni kwamba Rais pamoja na wasaidizi wake hawajui kusoma na kuandika.Yaani tunaongozwa na mbumbumbu.
 
Hii serikali imezoea kudanganya, wakishitukiwa wanaanza kukunja mkia kama mbwa aliyebambwa akiiba mayai.

Hata hizi million 6253 ni namba tu, wakiminywa zaidi sio ajabu wakabadili tena.

Haiingii akilini eti akosee aliyeandika, aliyeikagua asione, raisi mwenyewe wakati anaipitia kabla hajaisoma naye asione😳

Halafu eti waliofanya kosa kubwa hivyo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
 
Mkuu ulikomaa Sana nikakwambia ni dola mil.6250 bado ukawa huelewi.Nadhani sasa umeelewa.
Wewe ni mgumu kuelewa, raisi alikosea kutoa zile figure. Sisi ndio tukawa tunahoji inawezekana vipi tukawa na fedha kiasi hiko.
Leo ikulu kutoa ufafanuzi ni kuwa wamekubaliana na raisi alikosea kwenye hotuba yake, japo yeye mwenyewe mama Samia aliwahi kusema raisi hakosei
 
Na sio mara ya kwanza haya makosa kwenye hotuba za mama, hata ile hotuba ya siku ya Uhuru alikosea kosea sana.
Hawapaswi kuishia kutoa ufafanuzi Bali kujua kwa nini makosa yapo kila hotuba
 
Inawezekana mwandishi na msomaji wote walikimbia namba (HKL).
 
Kwani mimi nilibisha? Si nilisahihisha? Rejea mijadala yetu.
 
Milioni 6253 kwa maneno inaandikwa: Milioni elfu Sita mia mbili Hamsini na Tatu tu. hilo neno "na" liondolewe.
 
Kubalini hamjui mnachofanya! Yaani mwandishi na mwandikiwa wote hawaeleweki!
 
Naomba watujibu Sinema ya Royal Tour iligharimu kiasi gani miez zaidi ya 6 sasa hakuna jibu
 
Bora kuliko ile ya nileteeni Gwajima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…