Hii serikali imezoea kudanganya, wakishitukiwa wanaanza kukunja mkia kama mbwa aliyebambwa akiiba mayai.
Hata hizi million 6253 ni namba tu, wakiminywa zaidi sio ajabu wakabadili tena.
Haiingii akilini eti akosee aliyeandika, aliyeikagua asione, raisi mwenyewe wakati anaipitia kabla hajaisoma naye asione😳
Halafu eti waliofanya kosa kubwa hivyo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Pia miye nina wasiwasi maana hali ya akiba 2020 ilikuwa USD 4.8 bn chini ya John Pombe Magufuli, sasa hii nyongeza ya karibia dola USD 2bn inahitaji ufafanuzi kwa mwaka 2021 :
“Akiba ya fedha za kigeni imebaki katika viwango vya kuridhisha na kufikia USD Bil 4.8 mwishoni mwa December, 2020, hii inatosha kulipia uagizaji bidhaa
Source :
https://www.bot.go.tz/PressRelease?lang=sw
Toka maktaba kabla ya gonjwa la covid-19 kuyumbisha uchumi, malipo kwa miradi mikubwa ya Stiegler's Gorge Rufiji kwa Egypt , SGR reli wa Turkey tena kwa USD hela za kigeni na wala hatujataja vita kubwa ya kiuchumi ya mabeberu hali ilisomeka hivi :
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 akiba ya fedha
za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kukidhi mahitaji ya
kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hadi Aprili 2020, akiba ya
fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 5.3. Kiasi hiki
kinatosheleza mahitaji ya fedha za kigeni za kuagiza bidhaa na
huduma nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 6.1 ikilinganishwa na dola
za Marekani bilioni 4.4 kilichotosheleza mahitaji ya fedha za kigeni
za kuagiza bidhaa na huduma kwa kipindi cha miezi 4.3 kwa kipindi
kama hicho mwaka 2015. Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka
kwa uwekezaji wa kigeni na mauzo ya bidhaa na huduma nje ya
nchi. Aidha, kiwango cha akiba ya fedha za kigeni kilichofikiwa ni
zaidi ya lengo la kuwa na akiba ya kutosha kuagiza bidhaa na
huduma nje ya nchi kwa muda wa miezi 4.0 na pia ni juu ya lengo
la miezi 4.5 lililowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki na lengo la miezi isiyopungua 6.0 kwa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC.