SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400


Tuwekee kwenye mtindo wa bango kitita (table). Kwa maelezo hayo hatuwezi kuelewa kwa urahisi.
 
Niliona wanazungumzia kutakua na chakula, ndo kwenye hizo gharama au vipi?
 
Sio kweli ulaya treni ya mwendo kasi ya umeme nauli yake kubwa kuliko mabasi ya safari ndefu .
 
[emoji81][emoji81][emoji81]mbongo iki zidi ata 200 tzsh ana enda kwenye pungufu
 
mmesahau kuwa jamaa wanafanya makusudi ili shirika life turudi kwenyo mabasi na maroli. Yaani n makusudi mazima kabisaaa.
 
Itaen
Itaenda kupata hasara kama Air Tanzania.
Hiv wakiweka 15k kwenda Moro na 30k kwenda Dodoma watapungukiwa Nini.?
 
Serikali ikiendeshwa na wafanyabiashara neno HUDUMA huwa ni uhaini

Tutaendelea kupanda mabasi maana ndivyo TRC wanavyotaka. Nchi imejaa wapumbavu wengi kwenye nafasi za maamuzi
 
Mkuu issue ni muda utakaotumika kwa kusafiri na sgr na muda wakusafiri na abood.
Bado kwa kutumia bus unawahi mkuu, hilo dubwasha litatumia almost 2hrs au zaidi tupo hapa, kunbuka bus likijaa ni no stop so kuweka umakini wenye mabasi watabadirika ili sgr ikose abilia. -Tunza hii risiti.
 
Tuwekee kwenye mtindo wa bango kitita (table). Kwa maelezo hayo hatuwezi kuelewa kwa urahisi.
Dar-Morogoro
daraja la tatu
24,794/- kwa mtu mzima,
12,397/- kwa watoto.

Kwa Daraja la Uchumi,
29,752/- mtu mzima
14,876/- kwa watoto.

Daraja la tatu:
Dar es Salaam-Dodoma.
59,494/- mtu mzima.
29,747/- watoto.

Daraja la Uchumi
71,392/- mtu mzima.
35,696/- watoto.

Dar - Pugu.
Daraja la tatu.
4,694/- mtu mzima.
2,347/- watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…