RuwaIkunda
Senior Member
- Nov 2, 2017
- 156
- 279
[emoji16][emoji16][emoji16]Nlitegemea jana angevamiwa na "POLISISIEMU" na kumzuia asiongee na vyombo vya habari.
CCM wanateseka sana na hivo viti maalum 19 vya chadema, si wangewapa Polisi na TISS hizo nafasi bungeni, au hata Magereza.
Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.
1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.!
2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.!
3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.!
4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!
Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?
Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?
Mbona Zito Kabwe na Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa hawakupewa nafasi ya kuomba radhi na kurudishiwa uanachama wao?
Hapa kuna sinema inachezwa na ndani ya siku 30 tutaona matokeo yake, kama mtu alikuwa tayari kutengeneza igizo la kuangushwa na konyagi na kisha kusingizia wasiojulikana, hapa kuna mengi yanakuja.
Kila mwananchi aliyefurahishwa na kamati kuu, hebu tupia japo ubeti mmoja hapa kuonyesha furaha yako!
Wanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
nafasi ya kusikilizwa wamepewa kwa barua na kwa public notice ila wakatoroka kikao.
Hao waasi ni wabunge wa gereji full stop.
[emoji23][emoji23][emoji23] akileta ubeti ni tag mkuu
Naomba kuongeza beti 2 tu:
Hakika Wewe makini, Mwamba wetu Chadema,
Umewahoji Wahuni, Maswali yenye hekima,
Orodha kawapa nani, Mahera anakoroma,
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini.
Hawa Covidi kumi tisa, mbali sana timulia,
Ni virusi wana visa, tamaa waikimbilia,
Hatuwataki kwa sasa, Chama watatuulia,
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini.
Nanyi chadema mmezidi umalaya toka muanze kujiuza hamjapata mtaji tuu mfanye mambo yenu?CCM wanatumia pesa za walipa kodi kuwanunua covid 19 wanandungai kwa gharama kubwa badala ya maendeleo ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
Huyo si mwamba ni kamba,ukweli wajulikana
Yote hayo anaimba,mwisho atapatikana
Samahani ataomba,mkweli kujulikana
Ni mwamba aliyeshindwa,majeruhi toka Hai.
HONGERA NA PONGEZI[emoji120][emoji120]Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!
Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Wala hapo huna jibu,ni lugha zilizopindaSina budi kukujibu, we Lumumba buku saba,
Kubumba bumba sababu, hasa zile za mahaba,
Mazezeta mambumbumbu, ni fursa haswa Lumumba!
Sifia Mzee Baba, ukavune buku Saba.
Cc: Team 666
Mademu bomba wapo wengi. Hatutaki wadangajiWanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
Picha ndiyo kwanza limeanza ujiandae na kuandika shairi lingine .Manake mapigo Yajayo ya upande wa pili Ni hatari ya kufa mtu usimuone Kobe kainama ujue anatunga Sheria. Watu watajuta na kulaumiana kwa yote waliyoamua.Mgawanyiko utanzia kamati kuu yao,Bawacha,Bavicha mpaka ngazi ya chini Mkoa kwa Mkoa,wilaya kwa wilaya,kata kwa kata,mtaa kwa mtaa,Kijiji kwa Kijiji,kitongoji kwa kitongoji.Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!
Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Wala hapo huna jibu,ni lugha zilizopinda
Siasa za kujaribu,mwisho wake zinadunda,
Buku saba si sababu,Zezeta amekushinda
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM
Brazaj huna hoja,kazi yenu kulalamaKulikoni buku saba, ubeti umetungiwa?
Ulolipwa kwenye saba, itabaki ukigawa?
Wekeza japo akiba, ona nusu imeliwa!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!
Uliambiwa ni ligi, au watoka Namungo?
Ati zezeta ni Kingi, wa pimbi kwenye mapango?
Pambeni mpake rangi, utajitenga urongo!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!
Cc: Team 666
Brazaj huna hoja,kazi yenu kulalama
Siri kwetu ni umoja,huko kwenu uhasama
Hata mje kwa pamoja,Lumumba itawazima
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM.
Ulisikia wapi?hakuna mkubwa zaidi ya Chadema ref Lowassa,Slaa.Kabwe nk nkWanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
Brazaj umechoka,ujualo ni kubumba
Vina vimekukauka,na sera zenu sambamba
Malenga watakucheka,na kukuona mshamba
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM