Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.

1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.!

2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.!

3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.!

4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!

Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?

Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?

Mbona Zito Kabwe na Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa hawakupewa nafasi ya kuomba radhi na kurudishiwa uanachama wao?

Hapa kuna sinema inachezwa na ndani ya siku 30 tutaona matokeo yake, kama mtu alikuwa tayari kutengeneza igizo la kuangushwa na konyagi na kisha kusingizia wasiojulikana, hapa kuna mengi yanakuja.

mi-CCM kwa nini kufukuzwa hawa imewauma hivi?

Mpaka mnatia huruma!
 
Kila mwananchi aliyefurahishwa na kamati kuu, hebu tupia japo ubeti mmoja hapa kuonyesha furaha yako!

Malenga wa malenga nami naongezea huu, kwani malaya wa kisiasa hawana nafasi CHADEMA:

CHADEMA ina wenyewe, siyo hawa domo kaya,
Ni Supika au jiwe, yamekuwa yenu haya?
Ni haki yetu wenyewe, kuwafurusha malaya!
Hongereni sana Mbowe, wewe ni mtu makini!

Cc: Team 666
 
Wanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..

Hahaaahaa ha haa. Uliowataja mmoja ana influence TSIS tangu akiwa uvcmc. Yeye ni kipandikizi. Arudi tu nyumbani.

Walirudi mamvi na kina zirro sembuse huyu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] akileta ubeti ni tag mkuu

Usipate shaka jombi kuku tag ni wajibu. Huu uliuona?

IMG_20201129_173640_152.jpg
 
Naomba kuongeza beti 2 tu:

Hakika Wewe makini, Mwamba wetu Chadema,
Umewahoji Wahuni, Maswali yenye hekima,
Orodha kawapa nani, Mahera anakoroma,
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini.

Hawa Covidi kumi tisa, mbali sana timulia,
Ni virusi wana visa, tamaa waikimbilia,
Hatuwataki kwa sasa, Chama watatuulia,
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini.

Cc: Team 666
 
CCM wanatumia pesa za walipa kodi kuwanunua covid 19 wanandungai kwa gharama kubwa badala ya maendeleo ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
Nanyi chadema mmezidi umalaya toka muanze kujiuza hamjapata mtaji tuu mfanye mambo yenu?
Mlianza wabunge, mkajiuza
Wakaja madiwani, mkajiuza wee Hadi kichefuchefu
Sasa mmekuja jiuza covid 19!
Mtakwisha na ukimwi endeleeni kujiuza tuu.
 
Huyo si mwamba ni kamba,ukweli wajulikana
Yote hayo anaimba,mwisho atapatikana
Samahani ataomba,mkweli kujulikana
Ni mwamba aliyeshindwa,majeruhi toka Hai.

Sina budi kukujibu, we Lumumba buku saba,
Kubumba bumba sababu, hasa zile za mahaba,
Mazezeta mambumbumbu, ni fursa haswa Lumumba!
Sifia Mzee Baba, ukavune buku Saba.



Cc: Team 666
 
Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!

Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
HONGERA NA PONGEZI[emoji120][emoji120]
 
Sina budi kukujibu, we Lumumba buku saba,
Kubumba bumba sababu, hasa zile za mahaba,
Mazezeta mambumbumbu, ni fursa haswa Lumumba!
Sifia Mzee Baba, ukavune buku Saba.



Cc: Team 666
Wala hapo huna jibu,ni lugha zilizopinda
Siasa za kujaribu,mwisho wake zinadunda,
Buku saba si sababu,Zezeta amekushinda
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM
 
Wanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
Mademu bomba wapo wengi. Hatutaki wadangaji
 
Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!

Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Picha ndiyo kwanza limeanza ujiandae na kuandika shairi lingine .Manake mapigo Yajayo ya upande wa pili Ni hatari ya kufa mtu usimuone Kobe kainama ujue anatunga Sheria. Watu watajuta na kulaumiana kwa yote waliyoamua.Mgawanyiko utanzia kamati kuu yao,Bawacha,Bavicha mpaka ngazi ya chini Mkoa kwa Mkoa,wilaya kwa wilaya,kata kwa kata,mtaa kwa mtaa,Kijiji kwa Kijiji,kitongoji kwa kitongoji.
 
Wala hapo huna jibu,ni lugha zilizopinda
Siasa za kujaribu,mwisho wake zinadunda,
Buku saba si sababu,Zezeta amekushinda
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM

Kulikoni buku saba, ubeti umetungiwa?
Ulolipwa kwenye saba, itabaki ukigawa?
Wekeza japo akiba, ona nusu imeliwa!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!

Uliambiwa ni ligi, au watoka Namungo?
Ati zezeta ni Kingi, wa pimbi kwenye mapango?
Pambeni mpake rangi, utajitenga urongo!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!

Cc: Team 666
 
Mkuu Team 666 nadhani nimejitolea ya kutosha kuku tag kama ulivyoomba.

Wa huku kujitolea ni wajibu. Huku wa kubebwa kwenye malori au kulazimishwa kuhudhuria hawapo.
 
Kulikoni buku saba, ubeti umetungiwa?
Ulolipwa kwenye saba, itabaki ukigawa?
Wekeza japo akiba, ona nusu imeliwa!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!

Uliambiwa ni ligi, au watoka Namungo?
Ati zezeta ni Kingi, wa pimbi kwenye mapango?
Pambeni mpake rangi, utajitenga urongo!
Kama nusu imekwenda, subiri kuliwa wewe!

Cc: Team 666
Brazaj huna hoja,kazi yenu kulalama
Siri kwetu ni umoja,huko kwenu uhasama
Hata mje kwa pamoja,Lumumba itawazima
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM.
 
Brazaj huna hoja,kazi yenu kulalama
Siri kwetu ni umoja,huko kwenu uhasama
Hata mje kwa pamoja,Lumumba itawazima
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM.

Hoja si kubumba bumba, bali ni kudadavua,
Kusifia kama Luba, lije jua au mvua?
Huo waitwa uzoba, nani asiye ujua?
Nusu tena imekwenda, subiri sasa kuliwa!
 
Brazaj umechoka,ujualo ni kubumba
Vina vimekukauka,na sera zenu sambamba
Malenga watakucheka,na kukuona mshamba
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM
 
Wanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
Ulisikia wapi?hakuna mkubwa zaidi ya Chadema ref Lowassa,Slaa.Kabwe nk nk
 
Brazaj umechoka,ujualo ni kubumba
Vina vimekukauka,na sera zenu sambamba
Malenga watakucheka,na kukuona mshamba
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM

Nusu mbili zimekwisha, rasmi sasa u punga,
Vina unasahihisha, kwa 'scheme' ya kuvunga?
Kama ndiko kujishasha, ni sawia na kudanga!
Buku saba yote kwisha, sasa washindwe wenyewe!
 
Back
Top Bottom