Shaka Hamdu Shaka: Tumepunguza ada ya usajili wa "Online TV" kwa 95% kutoka TZS 1M hadi shilingi Elfu 50

Mbio za Panya

Wafuasi wa Lumumba mm hapo ndio huwa siwaelewi... Yaani tozo ya awali mliweka nyie(Mkashangilia),,Leo tena nyie wenyewe mmeifuta(Mnashangilia)... as if kuna kitu kipya mmeongeza..

Mnatengeneza tatizo,, halafu mnalitatua.. then mnajiona Wakombozi...

Mtazamo tu...
 
Unaona ni mbaya kuwa elfu 50?
 
Online Tv hizi hizi ambazo hazina content ya maana kila mda ngono tu au kuna nyinginezo zenye maadili?
Hebu fikiria mtangazaji anamuuliza mtu eti,
•unafanya mapenzi mara ngapi kwa wiki?
•Je una mchepuko?
•unapenda kufanya mapenzi muda gani?
Rubbish!! Waandishi hawana ethics kabisa na wengine wanaandika vichwa vya ovyo ovyo kama;
•mtoto wa magufuli acharuka asema nchi inaongozwa tofauti na baba pia asema waliomuua baba yake. Au
•Tazama wabunge wapigana bungeni samia atia neno.
Ukiingia ndani amna kitu kabisa yani kinachoandikwa hakiendani na kichwa cha habari, kiukweli nilitegemea usajili uwe ata 5 milion na mtu awe kasomea kabisa mambo ya habari.
 
Online Tv hizi hizi ambazo hazina content ya maana kila mda ngono tu au kuna kuna nyinginezo zenye maadili?
Hebu fikiria mtangazaji anamuuliza mtu eti,
•unafanya mapenzi mara ngapi kwa wiki?
•Je una mchepuko?
•unapenda kufanya mapenzi muda gani?
Rubbish!! Waandishi hawana ethics kabisa na wengine wanaandika vichwa vya ovyo ovyo kama;
•mtoto wa magufuli acharuka asema nchi inaongozwa tofauti na baba pia asema waliomuua baba yake. Au
•Tazama wabunge wapigana bungeni samia atia neno.
Ukiingia ndani amna kitu kabisa yani kinachoandikwa hakiendani na kichwa cha habari, kiukweli nilitegemea usajili uwe ata 5 milion na mtu awe kasomea kabisa mambo ya habari.
😀😀😀😀
 
Hivi wameanza kutoa leseni za biashara kwa biashara za mtandao?

Nina bonge la mchongo. Nahitaji moja.
 
Hiyo hatua ni nzuri mno Serikali imefanya kupunguza gharama za leseni za online TV itafanya vijana wengi waanze kupiga kazi online kusaka pesa

Online business ni eneo linaloongoza kwa sasa duniani kwa kuzalisha mabilionea wakubwa duniani nafasi nyingi za juu

Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani aweza kulipa

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako online , pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.Sisi tunapiga kelele ohh vijana wanatumia simu na komputa kuangalia picha za ngono na movie tu tofauti na wakenya sasa tusipowasaidia kujua kuwa waweza fanya kitu na kupitia PayPal wakapata pesa wataendelea na matumizi mabaya

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake i tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.

Sio vizuri Serikali kuwaza tu kupata mipesa ya kigeni kupitia korosho,pamba ,kahawa nk online business ni eneo moja kubwa sana la kuingiza pesa za kigeni

Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga waanze kufundisha practical online business kama somo linalojitegemea
 
Unaona ni mbaya kuwa elfu 50?

Hapana Mkuu,, hakuna ubaya wowote kwa kilichofanyika....

Nilichosema ni kwamba aliyeweka watu walipe Millioni Moja,, ndio leo aliyetoa na kubaki Elfu hamsini..

Nani wa kusifiwa hapo na ni nani wa kumchukia..???
 
Hiyo hatua ni nzuri mno Serikali imefanya kupunguza gharama za leseni za online TV itafanya vijana wengi waanze kupiga kazi online kusaka pesa

Online ni eneo linaloongoza kwa sasa duniani kwa kuzalisha mabilionea wakubwa duniani nafasi nyingi za juu

Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani aweza kulipa

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako online , pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.Sisi tunapiga kelele ohh vijana wanatumia simu na komputa kuangalia picha za ngono na movie tu tofauti na wakenya sasa tusipowasaidia kujua kuwa waweza fanya kitu na kupitia PayPal wakapata pesa wataendelea na matumizi mabaya

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake i tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.

Sio vizuri Serikali kuwaza tu kupata mipesa ya kigeni kupitia korosho,pamba ,kahawa nk online business ni eneo moja kubwa sana la kuingiza pesa za kigeni

Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga waanze kufundisha practical online business kama somo linalojitegemea
Hii ni comment ya maana sana aise,

YEHODAYA 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom