Shaka Hamidu Shaka, mrithi wa Polepole nafasi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

Uchunguzi ulitoa majibu gani? Je alikuwa bado amesimamishwa kabla ya uteuzi huu!!
 
Mama safisha taka mpaka chini ya kapeti. Vunjavunja vipuri vyote vya Udikteta. Tunakupenda saana
Kule saccos mnaanza lini kisafisha, au mzee wa faru John kashawasafisha nyote?.
 
Shaka Hamdu wewe utakuwa umepata fundisho kutoka kwa mtangulizi wako,Polepole alijitengenezea maadui kwa sababu ya maneno ya kejeli na vitisho kwa watu.
Jifunze kwa Januari Makamba na ikibidi mfanye awe rafiki yako,utavuna busara nyingi kabla hujafungua kinywa.

Nakutakia kika la kheri.
 
Ila yatima hadi mnatia huruma bado mnaota labda kuna siku baba atarudi, mlijaa viburi sana mkiongozwa na chakubanga na bashiru, ila Mungu ni fundi sana.
Kwa hiyo point yako ni nini sasa?

Lisu na chadema waekuwa Rais?
 
Kule saccos mnaanza lini kisafisha, au mzee wa faru John kashawasafisha nyote?.
Yaani kika anayemkubali Mh. Samia ni CHADEMA? Kwa taarifa yako nina kadi ya chama miaka mingi kabla hujazaliwa wewe. Na kuwa mwana CCM siyo tiketi ya kukubali kila uozo wa chama. Toka zile enzi za wizi wa EPA, ESROW na akaingia tena Dikteta sikuafikiana na upuuzi ule. Na haimaanishi kuwa kama sikubaliani na nikipinga basi ni Mpinzani.

Mimi nililelewa kwenye familia yenye maadili sana na niko makini kwenye kila kitu. Siwezi kushabikia maovu hasa uuaji wa binadamu. Kamwe hata uwe mzuri kiutendaji kakini ukikatili basi siwezi kukushabikia.

Hivyo Elewa niko home kabisa na sitegemei kuondoka home ila wakiharibu nitasema. Na msiniunganishe na Wapinzani.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu na siku zote Kweli itatuweka huru.
 
Hwa jamaa walijiona kwamba wao ndio ccm yenyewe na ambao wanaweza kufanya jambo lolote wakt wowote bila bughdha ya mtu yoyote, toka popote pale.
walifanyaje, ebu nipe matukio hata mawili tu
 
CCM ni ileile toka enzi ya Baba wa Taifa! Wala usiumize sana kichwa chako,hata Mama nae muda ukifika mtaanza kuona hafai na mtatamani Jiwe arudi tena!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…