mgen
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 23,169
- 9,054
Khutba hiyo peleka Kwa kidile kwenye Watu kama we ukazawadiwe takbirrrr ✊Niaje waungwana
Baada ya Israel, Marekani, Uingereza na washirika wao wengine kujipanga kwa zaidi ya mwezi mmoja na kitu ili kufanya shambulizi la kuiangamiza Iran kushindwa.
Sasa tumeona wenyewe jinsi Iran ilivyo imara kwa air defence yao hadi kupelekea shambulio la ndege 100 za Israel kushindwa kupiga hata kituo kimoja cha polisi. Maandalizi yalikuwa makubwa mno lakini mashambulizi yalikuwa madogo mno. Ndege 100 ambazo hata hivyo hazikuingia ndani ya anga la Iran ni kama vile zilienda kuzurura tu kwa wenzao.
Gharama kubwa za maandalizi ya shambulizi, mafuta na propaganda halaf zinafika kwenye mpaka adui na kutoka bila kuacha hasara ni aibu na fedheha kubwa kwao.
Sasa baada ya kuona wameshindwa kufanya chochote cha maana. Kuna kundi la wayahudi wetu wa bonyokwa na wale wa tel aviv ya Tandale wamekuwa wakikusanya kusanya vipicha picha na video za vile vishambulio vya Gaza na kuviunganisha hapa kwenye tukio la leo ili kuwahadaa wajinga wenzao kuwa shambulio la Israel lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa kitu ambacho sio kweli.
Shambulio lao lilikuwa la hovyo sana ndomaana dunia haijui kinachoendelea huko Iran. Hii ni tofauti na mashambulio ya Iran ambayo huwa na uzito na kuifanya dunia karibia yote ikiiongozwa na nchi za magharibi kulaani shambulio la Iran nchini Israel. Siku zote mtemi mwenye nguvu akimpiga mnyonge, watu husema na kupiga kelele. Lakini mnyonge akijitutumua kumpiga mtemi watu huwa hawaoni wala kulalamika, maana hakuna madhara ambayo mwenye nguvu anaweza pata.
Tuombe Mungu Ayatollah asitoe kauli kuhusu kashambulio hako. Maana akitoa tu kauli, basi Netanyahu na genge lake watalazimika kuwakimbiza wanajeshi wao na familia zao shimoni mapema (handakini) kabla kiyama kingine hakijawakuta wakiwa juu ya ardhi wakitembea. Ayatollah huwa hatanii na kauli yake haibadilishwi na mtu yoyote hapa ulimwenguni.
Kwa aibu hii ya leo, kushindwa vita na hezbulah, ukijumlisha nyumba ya Netanyahu kushambuliwa huku THAAD na Iron Dome zikiiangalia. Netanyahu angekuwa mzalendo wa kweli angejiuzulu. Lakini kwa tamaa zake anataka mpaka afie uongozini. Yani hata hayati mzee Mwinyi amemshinda uadilifu.
"Israel strikes multiple targets across Iran in retaliatory strikes - The Jerusalem Post" 'Days of Repentance': Israel strikes multiple targets across Iran in retaliatory strikes