Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Mkuu Pascal Mayalla Majibu ya haya maswali ni rahisi mno.. Nimependa hitimisho..
Kwanza ni kweli baada ya kugundua wanafuatiliwa Ilikua ni Salama zaidi kuelekea nyumbani, Sababu getini kuna Walinzi, CCTV na ni Ulinzi wa saa 24,hivyo lilikua wazo sahihi.

Kwanini dereva hajadhurika ni Rahisi tu..Mlengwa alikua Lissu.. Angedhurika kama angekua na Silaha ya kuwajibu..

Watu kushuka na Bunduki za Kivita..
Kwanza kabisa Mkuu Pasco Viongozi wote wa upinzani wanapoenda kukamatwa huwa Polisi Wanazibeba hizi Silaha .. Hivyo haikuwa jambo jipya..
Hata Rais hivi sasa Walinzi wake wanatembea na Silaha za Kivita.

Kwanini anafichwa.. Hizi ni Siasa tu.. Hakuna Mtu anayeweza kufichwa Hospital..
Ok wanasema Dereva amefichwa hivyo wanashindwa kumuhoji, Lissu je!
Kafichwa na nani?
 

Sasa Paschal rejea maelezo ya Tundu kwenye video na hata maandishi yake...kuona wanafuatwa mara nyingi amesema walikuwa tayari wameshaingia ndani ya uzio...sasa je hizo options unazotoa wangezitekeleza vipi? Imagine umeingia ndani ya eneo la nyumbani na kuna kuta za fensi pande zote ...mara paap gari waiona gari inakuja nyuma.

Nafikiri waulize kwanza wanaohusika na usalama wa nchi hii:
  1. Je, Lissu alivotoa taarifa za kuwa kuna watu wamekuwa wanamfuata na gari mara kwa mara walifanya nini?
  2. Je, iweje kiongozi Lissu ashambuliwe kwa risasi 30+ eneo lenye walinzi ndani na nje kwa ajili ya viongozi wa serikali? Vipi walinzi walienda likizo siku hiyo? Je, kama walikuwepo hadi gari zinaingia ndani hawakuziona achilia kumwaga risasi 30 wapo tu!! Au walisepa baada ya kusikia milio ya risasi maana wao walibeba toys!! Hata siamini hilo.
  3. Inasemekana ni kawaida kuwepo kwa surveillance camera ktk eneo linalozunguka nyumba tukio lilipotokea, je siku zilikwenda wapi?
  4. Inasemekana baada ya tukio polisi walifika lisaa baada ya tukio kutokea, je kuna umbali gani kutoka central police hadi Area D? Au magari hayakuwa na mafuta siku hiyo, au yalikuwa karakana. Cha ajabu Mange Kimambi akikohoa tu barabara za miji na majiji zinapambwa na gari za doria.
  5. Ikiwa dereva aliweza kumlaza chini kumkinga na risasi, je kama anahisiwa kumuua kwa nini hakumlengesha sehemu nzuri? Hapa hao wasiojulikana wasingepoteza risasi nyingi hivyo.
 
Tumekusikia, ni mpango wa Mungu Lissu kupona, na Mpango wa shetani unaendelea mpaka sasa kutoka kwa waliojaribu kumuua, sawa umemhusisha dereva wake kuhusika, lakini katika maswali yako mbona haujajiuliza kwanini dereva huyu alimzuia Lissu kushuka kwenye Gari karibia nusu saa? na kwanini hujajiuliza hawa washambuliaji kuingia ndani ya makazi ya viongozi? yaani wauwaji namshambulia kiongozo ndani ya makazi yenye ulinzi hujiulizi kaka, Kamela kufunguliwa eneo la tukio hujiulizi kaka,

Sawa Mungu kwasabu ni wenu sio wa wengine mtashinda uovu huu.
 
Tuanze tu hapa. Unafahamu kidogo kuhusu mambo ya jeshi? Je unafahamu range inafanyikaje? Je ushawai tumia bunduki?
Haya mambo kama hufahamu kamwe huwezi nielewa kwa kweliii!! Kiufupi tu ni hivi walengaji walikuwa na papala katika kupga gari, pia mpgaji hakukaa angle nzuri hivyo hakuona vizuri nini kinaendelea kwenye gari LA lisu,pia tambua kwamba dereva wa lisu ashapitia baadhi ya mafunzo ya awali hivyo inaonyesha alijianda baada tu yakuona tayari washakuwa targeted!!!
Mwishooo namalizia kwa kusema hivi hao waliofeli hiyo mission now wako katika mateso makubwa kwa kufeli kutimiza kazi wako wapi na nin kinafanyika juu yao hapa si mahala pake
 
Ukigonga msumari kwenye bati sehemu ulipoingilia na unapotokea huwa na shape tofauti. Sehemu ulipoingilia panakuwa na shape ya kubonyea, na sehemu ulipotokea hupanda juu!

Je, yale matundu ya gari ya Lissu yakoje? Kama yametoka kuvutika nje probably risasi zitakuwa zilipigwa kutokea upande wa kulia wa dereva. Lakini Kama yalibonyea kuingia ndani probably yalipigwa kutokea nje upande alikuwa amekaa Lissu.

Matundu yale yanaonekana hayakupigwa kutokea kulia.

Je, ina maana dereva alishuka akaelekea upande wa Lissu na kumimina risasi? Vipi camera zilizoondolewa?
 
Na wewe ukiitwa kuulizwa maswali usije kulalamika popote pale.
Huyo dereva kajua alichotendwa.. asali mola amfungue kuyajua
 

Walikufanya nini uko bungeni? Siku hizi umepotoka sa. Ulianza kumtetea Makonda, baada ya siku mbili Rais akawaibisha kwa kusema alipe kodi.
Leo umekuja na hii, polisi wangetakiwa kumhoji dereva lakini polisi hawakwenda kumhoji.
Polisi walitakiwa kuwahoji walinzi wa area D lakini walitolewa kabla ya tukio.
Polisi walitakiwa kwenda kuchukua cctv footage kwa Kalimani, lakini ziliondolewa baada ya tukio.

Leo unakuja kujiabisha mbele ya hadhira kweli Paschal?
 
Mguu wa kulia umejeruhiwa vipi kuliko wa kushoto risasi zilipotokea?
 
Hahahahahah acha kuandika pumba wewe.Yani mtu aliyepewa AK 47 akaue hawez Fanya upuuzi unaoelezea hapo.risasi 38 ni nyingi mno kwa tukio serious. Kuna matukio mengi sana ya uvamizi,ni risasi 3 zimezidi na tukio lisilozid dk.Kwa maelezo yenu ni kwamba wauaji walipoingia ndani wakaanza kusubir kwanza wamuone lisu ndio wampige risasi na wakati huohuo Dereva anaangaika kulaza kiti kumficha lisu naye kushuka na kujificha chini ya gari.Yani baada ya dereva kumficha lisu naye kujificha ndo kumimina risasi kukaanza hahahahahah. Hii movie ya kichina ni noma sana. Tukio la kuvamiwa lisikie tu lkn sio kwa hizi porojo
 
Mm sijasemea sana serikali nimechukizwa tu Na jinsi watu wanavyoshambulia mtoa madam wanataka awe anaandika post za kuwafurahisha wao.
Hafu una ushahidi kua serikali ndio ilifanya hill tukio kwa lissu
 
Pascal Mayalla, aisee utamfanya akili fupi Lissu akufikire hata wewe kuhusika na kupigwa risasi yeye. Kwa kweli ume raise some valid points here ila inasikitisha kuona watanzania wengi hawana upeo wa kuona mbali wao wako tu hapa kupinga kila kitu. Wabongo mmehamshwa sasa, hamkeni.
 
Nafikiri mngeonekana mko rational ktk kufikiri kama mngesema dereva na waliotoa kamera wote wanahusika kumdhuru lisu.Hii kumtoa dereva kwa mgongo wa kamera hakuna logic yyt.Haiwezekani uone unafuatiliwa we unazd kwenda tu,mnafika geti wako nyuma nanyi mnaenda tu.unakuja na story za kujificha chini ya gar.
 
Hizo CCTV cameras zimehama lini kutoka kwa Kalemani na kwenda kwa Lisu mwenyewe?Nani alienda kuzitoa? Mnapoteana Sana
 
Paskali ( NJAA) amesahau kabisa jinsi meja general mstaafu serikali ilivyoshughulika,kama wanavyodai kwanini CCTV zilitolewa
 
Pengine hata huyu pascali pia alihusika. Lakini langu kubwa zaidi ni jinsi gani naweza kuzuia post za member mojawapo hapa jf nisizione maana kisaikolojia anawafanya watu wamtukane halafu mwishowe wale ban
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…