Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Mayala is very right in this regard.

Kwa yeyote mwenye kufikiria sawa sawa, asiyeegemea upande wowote kwenye fikra zake, lazima ataliona hilo kiurahisi sana.

Memories zangu pia zinanikumbusha sakata la Chacha wangwe na dereva wake, na kauli za mbowe na chadema yake, na ukweli uliokuja kufahamika baadae kuhusu dereva yule na ukaribu wake na mbowe na chadema yao kwa ujumla wake
 
Pascal hakuna tena.amebaki anatanga na njaa. Alafu na vijana wa lumumba tabia ya mtu anapohoji kitu mnakimbilia kusema n chadema sio kweli.wengine n wazalendo tu
 
Kweli urudi shule,yaani unamfananisha PM au Rais na Mbunge hahahahahah.
 
Pascal Mayalla siku hizi unajitia aibu. Ni bora ungekaa kimya kuliko kuleta huu mchanyato wa pumba na ujuha.
 
wewe uelewa wako ni mdogo kama hujamwelewa mayala alichoandika au una laumu inaonesha huelewi n ahutaweza kumwelewa labda mpaka ufanyiwe maombi ubadilishe akili uliyo nayo ikue level ya juu zaidi ya hapo.
Huenda hata wew uelewa wako mdogo zaid ndomana unafikiri kila MTU yupo km wew
 
Pascal Mayalla,

..JE, haiwezekani kwamba walielekea nyumbani kwasababu kuna ULINZI toka getini, kwa Naibu Spika, na viongozi wengine?

..Pia they did what you suggested, walikwenda eneo ambalo lina WATU WENGI.

..Inasemekana walipofika hapo Area D walikuta kumejaa magari na ilibaki nafasi moja tu ambayo walipaki gari ya Mh.Lissu.

..Kwa maana hiyo Area D kulikuwa na watu wengi, na ni eneo ambalo Mh.Lissu na dereva wako familiar nalo.

..Pia inategemea maelekezo ya Mh.Lissu kwa dereva wake baada ya dereva kumueleza wanafuatiliwa.

..Wako wanaodai kwamba kitendo cha parking lot kuwa na magari mengi kiliwazuia washambuliaji kuwa huru zaidi ktk KULENGA gari la Mh.Lissu.

..Swali lingine ni kuhusu MGUU WA KULIA kuumia zaidi kuliko wa kushoto ambako risasi zilikuwa zikitokea.

..Kwanza mguu wa kulia kuumia zaidi kunaweza kusababishwa na sehemu gani ya mguu risasi zilipita.

..Kwa mfano, kama mguu wa kushoto ulipigwa risasi lakini zikapita kwenye nyama, lakini mguu wa kulia risasi zikapiga mfupa, then mguu wa kulia utakuwa na matatizo zaidi.

..Vilevile inategemea kiungo/mfupa gani wa mguu wa kulia ulipigwa na risasi vs mguu wa kushoto.

..Vilevile inategemea humo ndani ya gari Mh.Lisssu alikuwa ktk position gani. Je, alikuwa amelalia tumbo, mgongo, au ubavu? Na ubavu upi?

..Kwa haraka, kama alilalia TUMBO, na kichwa alielekeza upande wa kiti cha dereva, basi risasi zilikuwa zinatokea upande wa KULIA kwake na huenda ndiyo sababu ya mguu wa kulia kuumia zaidi.

Cc MISULI, tindo, Mag3, Nguruvi3, chige, Magonjwa Mtambuka
 
Maswali ya kujiuuliza kwakutumia akili za kuvukia barabara 1.Kwanini CCTV Ziliondolewa 2.Kwanini Walinzi Pia wa Sehemu Zote waliondolewa 3.Nani Hupanga zamu za Walinzi wa eneo Hilo 4.Je hao walinzi ni wa Kampuni Binafsi?, Kitendo cha kuuondolewa walinzi wote kinakupa picha gani km Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, 5.Swali la Mwisho je hao walinzi walitii amri ya Derva wa Lissu kuondoka kwenye lindo? ''Pascal Mayalla when you are terrorized in a compound which is assumed to be guarded all the time with your empty hands what could you do to save your life''
 

Paskali hapa bro umechemka. Hizo points zote ungezijibu mwenyewe kwa jibu la swali moja! Wakati Lissu anafuatwafuatwa na gari moja mpaka akawapa polisi namba zake za usajili je polisi walifanya nini???? (Kumbuka hapo Lissu bado hata hajapigwa risasi) Sasa kama hawakufanya kitu je hata kama Mh.Lissu angefanya hatua hizo 1,2,3,4.....kingebadilisha kitu gani??

Jiulize hivi:

  1. Walinzi wanaolinda makazi ya Lissu na wakazi wengine siku hiyo hawakuwepo kwa nini? Kwani ni walinzi wa Chadema hao au ni wameajiliwa na serikali?
  2. CCTV mpaka leo ziko wapi na ziliondolewa na nani? Au pia CCTV ni za Chadema?
  3. Mpaka leo hakuna mtuhumiwa kesi yenye profile kubwa kama hii?
  4. RPC wa Dodoma kila mara unamuona hata akikamata bodaboda anawaita waandishi wa habari kuwapa habari. Je ulishasikia RPC wa Dodoma ameita Press conference kuwambia kesi ya uchunguzi wa jaribio la kumuua Mh. Lissu imefikia wapi??? Kwa maana hiyo hizo points zote ulizoorodhesha hata kama zingefanyika zisingebadilisha chochote!
 
Halafu CCTV cameras tuliambiwa zilikuwa kwa Kalemani ambaye Ni jirani yake Leo tumeambiwa zilikuwa kwa Lisu mwenyewe. Mpimeni na akili jamaa yenu au aanze matibabu ya kisaikolojia kama dereva.
Kwa hiyo hapakuwa na cctv camera pamoja na walinzi...yaani hilo eneo halikuwa na ulinzi wowote...!? Shetani mkubwa wewe
 
UFIPA kama wamepoteana kwenye hii thread..

Freedom of Speech inaendana sambamba na demokrasia,

Pascall katumia demokrasia kutoa maoni yake kama mtanzania..
Hawa jamaa wakija pewa nchi watakua madikteta wabaya sana kuwahi kutokea duniani.Yani kwao ni mwiko kuwahoji.
 
wewe uelewa wako ni mdogo kama hujamwelewa mayala alichoandika au una laumu inaonesha huelewi n ahutaweza kumwelewa labda mpaka ufanyiwe maombi ubadilishe akili uliyo nayo ikue level ya juu zaidi ya hapo.
Endelea kuwaza km form two mzee
 
Onesha swali moja unaloona halijajibiwa na linastahili majibu,maana naona hausomi kinachoandikwa
 
Huna hoja ya msingi hoja zako mfu kabisa!!! Hivi kama dereva kahusika ilikuaje msaidie baada tu ya wasiojulikana kuondoka? Kama kahusika si angemmalizia tu pale pale??
Je zile CCTV camera kwann kalemani aling'oa??
Swala la dereva kumsaidia lisu haliondoi uhusika wake ktk tukio.Hata wachawi hulia sana msibani na sio rahisi kuamini endapo utaambiwa huyu ndiye muuaji
 
Mbona Paschal Mayala kaongea sawa tu nashangaa mnao mtuhumu, ktk issue ya kiuchunguzi hauwezi kumuweka pembeni dereva wa Mh Lissu maana ni wao wawili tu ndo walikuwa ktk gari

Kwa mfano labda hata wewe umeenda sehemu umekaa tu kwa sababu zako afu jirani na ulipo umetokea uhalifu na wamekuja askari polisi wamekamata wote walio hapo jirani na tukio la uhalifu nawe wame kubeba kwa sababu ni lazima waanzie sehemu kuchunguza hata kama hauhusiki na hilo tukio

Tukirudi ktk mada kwa kusema tu dereva nina muamini haitoshelezi kutotiliwa mashaka huyo dereva hata kama hana hatia lkn shuku juu yake ni ya msingi na wanaoitoa wasionekane tofauti

Hata ktk maandiko matakatifu tunajua Masihi/ha alisalitiwa na mtu wake wa karibu kwa vipande vya pesa kwahiyo lolote linawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…