Shehe: Hawa waarabu wamekuja kuchukua bandari yao waliyoijenga mwaka 1896 kinawauma nini?

Shehe: Hawa waarabu wamekuja kuchukua bandari yao waliyoijenga mwaka 1896 kinawauma nini?

Shehe huyu kutoka msikiti wa Madina ambao haukuweza kujulikana mara moja mkoa ulipo, amesikika akiongea kwa ukali sana akiwananga wale wote wanaomtukana mama kwa sababu ya kuuza bandari kwa waarabu. “Hawa waarabu wamekuja kuchukua bandari yao waliyoijenga mwaka 1896 kinawauma nini?” Ameuliza.

Shehe ameenda mbali zaidi kusema kwamba kipindi cha serikali ya Magufuli watu walikuwa kimya kwa sababu mtu yeyote aliyejitokeza kusema aliuawa na pia kuna baadhi ya wanasiasa waliikimbia nchi kwa kuhofia kuuawa.

Nisimalize utamu, hebu msikilize shehe wewe mwenyewe kwenye klipu hapo chini.

View attachment 2948109

MAONI YANGU
Huyu shehe namkubali lakini kitendo chake cha kuchanganya suala la kisiasa na uislamu sio vizuri. Hata kuifananisha serikali ya Magufuli na hii ya Samia kisa tu Samia ni muislamu na Mafuguli ni mkristo, ni suala lisilopendeza hata kidogo. Yeye angejikita tu kwenye hoja ya msingi bila kuingiza udini.

Nawasilisha.
Shehe anachotaka kutuambia ni kwamba kila kitu kilichojengwa na mwarabu au mkoloni, ni ruhusa kuja kuchukua vitu vyao, kwa mfano:

1. Kwa kuwa reli ilijengwa na wajerumani, basi waje waitumie bure au waje waing'oe waondoke nayo. Sasa hizi ni akili au matope?

2. Serikali ya Magufuli (mkiristo) ilikuwa inaua watu, kuwatia kwenye viroba na kuwatupa baharini lakini serikali ya Samia (muislamu) haiui watu. Hapa anatakiwa akamatwe atoe ushahidi hao watu waliuliwa wapi, na nani na kwa sababu gani. Vinginevyo, tuamini kwamba serikali ya muislamu onamlinda muislamu mwenzao.

3. Samia angehamishia serikali Didoma, wakristo wangekiwasha. Hawakiwashi tu kwa k7wa uhamishaji ulifanywa na Magufuli (mkiristo mwenzao). Anataka kutuaminisha kupwa kuhamishiwa kwa serikali Dodoma ni jambo haramu na kwamba jambo hili lilipaswa kufanywa na Rais muislamu. Sasa hizo ni akili au matope? Hivi huko madrasa hawa mashehe walienda kusomea elimu au ujinga? Cc FaizaFoxy
 
Huyu Shei

Huyu Sheikh ndo aliwahi kusema akienda Saudi Arabia huwa anapenda kwenda kuswali Kwenye Msikiti wanaoswali Majini!?
Yeah! Ndio yeye mkuu. Na inawezekana hapo haongei yeye bali anaongeleshwa na majini.
 
Shehe anachotaka kutuambia ni kwamba kila kitu kilichojengwa na mwarabu au mkoloni, ni ruhusa kuja kuchukua vitu vyao, kwa mfano:

1. Kwa kuwa reli ilijengwa na wajerumani, basi waje waitumie bure au waje waing'oe waondoke nayo. Sasa hizi ni akili au matope?

2. Serikali ya Magufuli (mkiristo) ilikuwa inaua watu, kuwatia kwenye viroba na kuwatupa baharini lakini serikali ya Samia (muislamu) haiui watu. Hapa anatakiwa akamatwe atoe ushahidi hao watu waliuliwa wapi, na nani na kwa sababu gani. Vinginevyo, tuamini kwamba serikali ya muislamu onamlinda muislamu mwenzao.

3. Samia angehamishia serikali Didoma, wakristo wangekiwasha. Hawakiwashi tu kwa k7wa uhamishaji ulifanywa na Magufuli (mkiristo mwenzao). Anataka kutuaminisha kupwa kuhamishiwa kwa serikali Dodoma ni jambo haramu na kwamba jambo hili lilipaswa kufanywa na Rais muislamu. Sasa hizo ni akili au matope? Hivi huko madrasa hawa mashehe walienda kusomea elimu au ujinga? Cc FaizaFoxy
Naam, umeniita?

Tatizo nini?
 
Hivi kumbe wanakuwa na majini humo kwenye nyumba zao za ibada?Hapa ndiyo nimepata jibu akili zao zinaongozwa na majini.
 
Tatizo ni wewe, kwani kadanganya?

Au unataka kuukimbia ukweli?
Kwa hiyo hata wewe unakubali kwamba bandari irudishwe kwa waarabu kwa kuwa waliijenga wao mwaka 1896?
 
Kwa hiyo hata wewe unakubali kwamba bandari irudishwe kwa waarabu kwa kuwa waliijenga wao mwaka 1896?
Irudishwe wapi wewe? Mbona unaongea kijinga?

Bandari washapewa Waarabu wa Dubai wanafanya yao hapo. Kaa utulizane, uone mwaka huu kuna faida au hakuna.

Wewe kama Mtanzania bado huwezi, umeshindwa. Ujinga haujakutoka.
 
Back
Top Bottom