Sheikh Mwaipopo: Muislam atakayehudhuria mkutano wa CHADEMA litakalomkuta ni juu yake

Sheikh Mwaipopo: Muislam atakayehudhuria mkutano wa CHADEMA litakalomkuta ni juu yake

Ishu ya dini ni very sensitive na mtihani sana ,acha atoe maoni yake .
 
MWAIPOPO ANA LAANA YA KUMKANA YESU

AMEKUWA TAHRA KABISA.
Mwalimu Nyerere alituonya sana na Ishu Ya UDINI.

ALISEMA WANASIASA "
walioishiwa hoja wanazungumzia UDINI"

Mwalimu Julius Nyerere.
Wewe sio mdini?? Angalia comments zako
Koran 5;51. Enyi mlio amini! (Waislamu) Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki.

DINI YA SHWETANI HII
Hadi unashika vifungu usivyovielewa kwa chuki zako tu
 
Anakemea maaskofu kushiriki siasa wakati yeye sheikh nafanya siasa.

Siasa ni maisha.
Huwezi kumchagulia mtu upande wakati humtimizii anachostahili kutoka kwako.

Ni ujinga kusema mjadala wa DP World umeshika mkondo wa udini wakati Sheikh analeta udini kwenye siasa.
 
Mwaipopo ni tapeli, hana ushekhe wowote. Wanaofahamu historia yake hawawezi kupoteza muda kumsikiliza.

Huyu bwana alikuwa mkristo. Wakati wa utawala wa Mwinyi kulikuwa na vuguvugu la kuiingiza Tanzania kwenye uislam wa siasa kali. Akaona hiyo ni fursa kwake ya kuchota pesa ya waarabu. Akaslim, Waarabu wenye misimamo mikali wakamchukua bwana Mwaipopo na kumpeleka Uarabuni. Aliporudi, yeye na shekhe Kassim (marehemu), ndio wakawa nguzo ya mahubiri ya msimamo mkali ba chuki dhidi ya ukristo. Wakatengeneza vikundi vya kuvunja bucha za nyama za nguruwe.

Na kwa Zanzibar, maduka ya pombe yakawa yanachomwa moto. Nchi ikaingizwa kwenye jumuia ya uchumi wa nchi za kiislam, ambao sharti mojawapo ilikuwa kuhakikisha utawala wa juu wa nchi mwanachama unashikiliwa na Muislam.

Yote yalifanyika kwa siri kubwa. Ilipokuja kufahamika, kelele zikawa nyingi dhidi ya utawala wa Mwinyi. Mwalimu Nyerere naye akaja juu dhidi ya Mwinyi, ndipo Mwjnyi kwa shingo upande akaitoa nchi kutoka jumuia hiyo ya OIC, na kisha kukemea na kutangaza kuwa mtu akitaka kula nguruwe au nyoka au kunywa pombe, ni ruksa. Ndiyo akapewa jina la Ruksa. Akaacha kila kitu, kiwe kibaya au kizyri kiendekee. Ufisadi ukamea kwa kiwango cha ajabu, uchumi ukaparanganyika, mfumko wa bei ukawa wa juu kuliko nchi yoyote Duniani ukifikia 30%, tukazuiwa kupata mkopo wala msaada wowote toka taasisi zote za fedha Duniani.

Hata sasa, haitashangaza kama Mwaipopo atakuwa tayari amekwishachota pesa ya DP. Huyu bwana yupo tayari kufanya lolote alimradi ahakikishiwe pesa nzuri ya kutosha.

Waislam wanafahamika, na mashekhe wa kweli wanaosimama katika misimamo ya imani yao wanafahamika sana. Jana tulikuwa kwenye tukio moja la ibada ya kikristo lililohudhuriwa na shekhe wa mkoa, aliyltoa nasaha nzuri sana, na alishangiliwa na kupigiwa makofi kuliko kiongozi yeyote aliyrpata nafasi ya kutoa salamu.

Watu wasijifiche nyuma ya dini kutimiza malengo yao machafu.

Bandari ni zetu sote wa dini zote, tunadhulumika sote. Hata wakati wa dhiki, hakuna muislam ambaye huwa anasaidiwa na waarabu eti kwa sababu ni muislam.
 
Waislam tokeni chadema haraka iwezekanavyo.

Muislam anaebaki chadema huyo ni Muislam jina tu, siyo Muislam wa kweli.

Watu wanaupiga vita Uislam waziwazi bado mnawakumbatia tu?
 
Back
Top Bottom