Sheikh Mwaipopo: Muislam atakayehudhuria mkutano wa CHADEMA litakalomkuta ni juu yake

Kwenye Madini ni % ngapi kwa ngapi?
 
Mimi kama mkatoliki nimeshangazwa na idadi ya maaskofu kwenye huo mkutano wa kesho. Hili suala la bandari lina sura ya kidini?
Sasa kama mkataba unatetewa na Mashekhe tu ulitegemea, Maaskofu wasiupinge.

Tulikosea sana tulipoanza kuwasajili machifu, viongozi wa dini kuwapa sauti ya hoja za kisiasa.

Na kuanza kuwapa majukwaa watoe maoni yao ya kisiasa wazi wazi.

By the way utawala usio na ushawishi kwa wananchi huwatumia viongozi wa dini kama kivuli cha kufunika madhaifu yake.
 
Waislam tokeni chadema haraka iwezekanavyo.

Muislam anaebaki chadema huyo ni Muislam jina tu, siyo Muislam wa kweli.

Watu wanaupiga vita Uislam waziwazi bado mnawakumbatia tu?

Bibi umejificha uk unaleta uchochezi tz?
 
Waislam tokeni chadema haraka iwezekanavyo.

Muislam anaebaki chadema huyo ni Muislam jina tu, siyo Muislam wa kweli.

Watu wanaupiga vita Uislam waziwazi bado mnawakumbatia tu?
Kwahio twende CCM? Muislam wa kweli Ni yule mwenye kuweza kutambua zuri na baya hivyo tutachambua wenyewe chuya na wali Ni upi.
 
Hahahah, kumbe kuna watu ni wendawazimu ila hawajijui kabisa! Kwa hiyo uislam ndio iwe ticket ya kuiuza Tanganyika na watu wake? Bila kujali dini, tumeuzwa wote, na hivyo wote tutahudhuris kwenye mkutano......

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Shekhe Mwaipopo kalewa pombe kali na mambo haramu yote anatumia. Uislamu anazugia tu kuwalaghai wajinga.

Pia mshirikina. Angekuwepo enzi uislamu upo moyoni kwa watu, angeumbuliwa kweupe na huo ushirikina wake na shirki zote anazofanya akiwa gizani.

Aisubiri siku ya upanga na maangamizi. Waislamu hatujafundishwa kukubali kuuzwa na madalali hata kama wamevaa shungi, vilemba na kanzu.

Ewe mtanzania amka sasa. Nchi inauzwa ukiwa unaona. Madalali wapo kazini kukuchuuza kama mbuzi wa vingunguti.
 
Daaah we jamaa najuaga msomi na mchambuzi kwa maandiko yako marefu marefu, kumbe madini tena mfia dini hasa na kwasababu hiyo unaunga mkono CHADEMA kwasababu ya hilo maana huu uwongo ulioandika hapo ni balaa hebu kasome hata kitabu tu cha Mwinyi uone kaelezea vipi swala la OIC, halafu OIC na mabucha ya Nguruwe na pombe wapi na wapi? Uganda ni mwanachama wa OIC kunani kule?
 
Hoja kuntu kabisa hizi. FaizaFoxy njoo uzijibu.
 
Dunia ya sasa watu hawatishani kwa mambo kama haya. Dunia isingetengeneza silaha na osama asingetumia mabomu
 
Kweli dini ukiwa na mahaba nayo akili inalala!

Hivi kweli humu Jamiiforums tunae member aliyeweza ku-post ujinga kama huu?na pia inawezekana alienda kumsikiliza,hiyo dini inaharibiwa na watu kama hawa wanaofundisha watu kwamba lazima kila kitu kiende pamoja kwenye box la dini hata kwa mambo yanayoonekana wazi yanawaumiza kwenye maisha halisi wanayoishi.
 
Misimamo hivi ushafika hayo maeneo kweli?
Unaongeleaje sehemu usiyo wahi kanyaga?

Wana misimamo zaidi/ sawa na watu wa Pwani.

Usikalili
ukiwa na msimamo na huna hela na nguvu yako ya kiuchumi ndogo ni sawa na bure hamna chochote kujidanganya labda muwape nchi hao waarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…