View: https://youtu.be/JXLHNt0loPU
TEC wametoa tamko rasmi la kupinga mkataba wa kubinafsisha Bandari kwa serikali ya Dubai. Tamko hili lilifafanuliwa kwa ufupi na Katibu wake Padri Charles Kitima, akieleza kuwa TEC wanataka sauti kinzani ya watu wengi wenye akili timamu isikilizwe.
Mtu aliyejitambulisha kama
Shemasi George Rugambwa, kutoka Seminari ya Ntungamo ya Bukoba, amejitokeza na kuuliza maswali saba. Kimsingi anawalaumu TEC kwa kurejea ujumbe wa Kibiblia katika Mathayo 23:13, usemao kuwa; "Ole wenu Mafarisayo wanafiki."
Tumeamua kuyajibu maswali ya "Shemasi George Rugambwa" kama ifuatavyo;
1.
Shemasi ameluliza: TEC inafahamu kwamba mwaka 1992 wakati Serikali inapitisha mfumo wa vyama vingi ulikuwa umekataliwa na asilimia 77 ya Watanzania? Hata hivyo serikali ikaamua uruhusiwe. Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.
Jawabu; Kauli mbiu ya TEC ni kwamba "Sauti ya Watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kuwa "Sauti ya Watu (wote wakiwemo na vichaa) ni sauti ya Mungu," maana Mungu sio kichaa. Hivyo, maneno "asilimia 77 ya Watanzania" pasipo kikolezo (qualifier) hayana nafasi katika hoja ya TEC.
2.
Shemasi ameluliza: TEC inafahamu kwamba mwaka 2001 baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar na mauaji ya wafuasi wa CUF mwezi Januari, asilimia kubwa ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla walitaka kuwepo na mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na SMZ na SMT chini ya Mkapa haikutaka? Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.
Jawabu; Kauli mbiu ya TEC ni kwamba "Sauti ya Watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kuwa "Sauti ya Watu (wote wakiwemo na vichaa) ni sauti ya Mungu," maana Mungu sio kichaa. Hivyo, maneno "asilimia kubwa ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla" pasipo kikolezo (qualifier) hayana nafasi katika hoja ya TEC.
3.
Shemasi ameluliza: TEC inafahamu kwamba mwaka 2014 maaskofu wote Katoliki Tanzania akiwemo Kardinali Pengo na wasaidizi wake walipokea mamilioni ya shilingi pesa taslimu na nyingine kwenye akaunti zao kama Askofu Nzigilwa (milioni 80 benki) na Kilaini (milioni 40 benki). Inajua fedha hizo zilitoka katika kampuni yenye makando kando ya rushwa ya kihistoria Tanzania. Wananchi wengi walipiga kelele lakini fedha hizo hazikurudi wala hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.
Jawabu; Kauli mbiu ya TEC ni kwamba "Sauti ya Watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kuwa "Sauti ya Watu (wote wakiwemo na vichaa) ni sauti ya Mungu," maana Mungu sio kichaa. Hivyo, maneno "Wananchi wengi" pasipo kikolezo (qualifier) hayana nafasi katika hoja ya TEC.
4.
Shemasi ameluliza: Padri Kitima anasema kwa zaidi ya miaka 60 ama toka tupate uhuru bandari yetu haijawahi kuendeshwa na wageni. Hii ni kauli yake au ya maaskofu wa TEC? Ni kweli TEC haifahamu kwamba kwa zaidi ya miaka 22 Bandari yetu ya Dar imekuwa chini ya kampuni ya TICTS ikiendeshwa kwa ubia na kampuni toka Hong Kong (Hutchsons?). Kama wanafahamu, wanakumbuka wabia wazawa wa kampuni hiyo wanahusika kwenye kuwapa hela maaskofu kama Rugemalira na IPTL yake walivyofanya? Hili wamewahi kuwaambia waumini wao katika mimbari za ibada?
Jawabu; Padri Kitima anasema kwa zaidi ya miaka 60 ama toka tupate uhuru bandari yetu haijawahi kuendeshwa na wageni "pekee." Umelisahau neno hilo "pekee." TICTS ilikuwa na wabia wabantu kina Karamagi.
5.
Shemasi ameluliza: TEC wanafahamu kwamba mwaka 1998 kwenye mauaji pale Mwembechai walikufa wasio na hatia na ilikuwa rai ya mamilioni ya Watanzania kutaka kuwepo na suluhu ya kisiasa? Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.
Jawabu; Kauli mbiu ya TEC ni kwamba "Sauti ya Watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kuwa "Sauti ya Watu (wote wakiwemo na vichaa) ni sauti ya Mungu," maana Mungu sio kichaa. Hivyo, maneno "rai ya mamilioni ya Watanzania" pasipo kikolezo (qualifier) hayana nafasi katika hoja ya TEC.
6.
Shemasi ameluliza: Padri Kitima anasema wananchi wamelikataa Bunge? Ametumia kipimo gani cha Kikatiba? Maana wananchi wanalikataa Bunge kwa kutowachagua Wabunge kwenye Uchaguzi. Hii “Vox Populi Vox Dei” ya TEC imetumia kigezo gani? Wananchi wakikataa Bunge pia si wameikataa Serikali? TEC inaomba vipi busara ya Mheshimiwa Rais ambaye wakati huo huo inasema serikali yake imekataliwa? Kuna kuchanganyikiwa na haraka kubwa kwenye tamko la TEC hata namna lilivyochapwa na kupangiliwa. Inanipa mashaka kwamba chombo hiki muhimu cha Kanisa kimekubali kutumika kwa maslahi binafsi bila tafakari ya kutosha.
Jawabu; Padre Kitia anasema kuwa "Kanisa Katoliki sio kikundi ha sala." TEC wamefanya kura ya maoni katika Parokia 3500 zilizotapakaa nchi nzima.
7.
Shemasi ameluliza:Je hii “Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu” ni wengi wapi hasa? Na mungu anayetajwa hapa ni nani? Usikute mungu anayetajwa na kusemwa asikilizwe ni mungu au miungu watu waliokuwa wanaingiza miamala kwenye akaunti za baadhi ya maaskofu wetu na viongozi wengine wa dini miaka nenda rudi. Tujihadhari. Tusiigawa nchi kupitia madhabahu.
Jawabu; Kauli mbiu ya TEC ni kwamba "Sauti ya Watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu (wa watu wote)." Hawajasema kuwa "Sauti ya Watu (wote wakiwemo na vichaa) ni sauti ya miungu watu." Hivyo, habari ya "kuigawa nchi kupitia madhabahu" haina nafasi.
Dawati la Mama Amon
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga