Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

No 12 ya kuweka mchanga ktk kidonda😀🙁😉🙂🙂🙂🙂😳😎😎
 
Sijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!
Giza likianza kuingia basi rafu zinaruhusiwa!
 
Umenikumbusha mbali ndg
 
Kuanzia Sinza Kimara Mbezi Mburahati Manzese open space zoote zimejengwa bar za makuti. Badala ya watoto wetu kucheza Dada poa wanauza utamu. Srrkali nayo inaangalia tu kisa wenye bar wanatoa ajira.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]no. 13
nilikua nikiona mpira unakuja naingia mpaka kati kati nadaka narudi nao golini[emoji23][emoji23]

team moja lazima mvue mashati ingine wavae ili mjuaje

gombania goli lazima ukifunga unamtoa usiempenda....
halafu kuna goli la upande mmoja mnaliopenda sanaa
mtu akija akiomba namba anacheza haijalishi team ina watu 20 au zaidi
mnajazana tu ilimradi.. [emoji23][emoji23]

mpira mnacheza mchana pekupeku...
uwanja ni popote
mnacheza wasichana , wavulana humo humo

akifika mchezaji bora mjinga mjinga unatolewa... au unakua kipa
 
kwenye namba4 hapo pananihusu nilikuwa nawekewa namba hata kabla sijafika
 
kuhusu jezi ilikuwa either team Ya kwanza kufungwa ndo wazue mashati (tshirt) au team iliovua jana leo hawavui
 
Nimekumbuka mbali sana kipindi hicho tupo kota...kuna jamaa ailikua ana mashuti na vyenga vingi, kuna siku ukatengenezwa mpira wa makaratasi ukawekwa jiwe ndani, sasa ile giza linaingia anatakiwa apige penati tukambadilishia mpira ...duh siji kusahau jamaa alikua na kigugumizi ila siku hiyo ailiongea vizuri kabisa kwa maumivu na vichapo vilianza.
Mimi sikua mchezaji mzuri lakini ilikua lazima nicheze, wasiponipanga mpira ukitoka nje nikiuokota speed yake watanikuta nyumbani na ndio mwisho wa mpira...Tv hamna kipindi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…