Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Kanzu na tobo vina hadhi sawa tu na goli
Na Tik Taka.

Hapo kwenye Darizi patamu, hasa ukimvisha mtu Darizi na kisha ukamvua, hapo watu fulu kushangilia "eeeeeeeeeeeee"

Au utasikia "Muongeze"
 
Viwanja sio issue tulikuwa tunacheza barabaran wakubwa wakipita tunashika mpira kwa kusema "heshima" wakishapita Ngoma inaendelea Na magari yakipita mwendo n huohuo
Hapo kwenye Magari umenikumbusha.

Unajua nini?

Mpira unasimama, na hapo hapo wengine tunapata nafasi ya kudandia Gari kama Gari yenyewe ikiwa Pickup Truck, au yoyote ile ambayo unaweza kudandia kwa nyuma, kisha unarudi mbio kuendelea na Mpira.

Kuna wakati kwenye kudandia Gari mara unadondoka.

Jamani
 
Mkuu usiumie sana,furahia maisha kwa wakati ulio nao coz hata huu wakati ulionao sasa pia utaujutia au utaukumbuka baada ya miaka 10 au 20 ijayo,

Sometimes you will never know the value of a moment until it becomes a memory.
Asante kwa neno la uzima.
 
Mkuu umenikumbusha kitambo sana, ilikuwa raha sana enzi hizo za mechi za utotoni. Unaandika jina la mchezaji maarufu unayetaka kufananishwa nae kwa maka pen mgongoni
 
Kuna vigoli vidogo hamna kipa. Ikitokea penati unatakiwa uzuie na mguu mmoja kama kilema.
[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] mkuu naikumbuka hii sheriaa.ilikua ni hatariii
 
Halafu gorikipa ilikua ni lazima awe mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupiga mpila goli hadi goli.

Na hapo lazima golikipa wenu anapo piga mpira timu nzima mnahamia kwenye goli la wapinzani wenu
 
Mwenye mpira alikuwa anaamua namna ya kushuti.. Mf. Hamna kupiga mandole( kwa vidole vya miguu) ili mpira usifumuke haraka.
Mkuu yawezakana ulikua mtaalam wa kuyapiga hayo madole[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kwa wale tuliokuliaa vijijin ilikuwa tamu kinomaaa...kila jioni kwenda kuchanja kuni mpira unachezwa kwanza giza likiingia ndo akili za kutafuta kuni zinaingia make ukiwahi unaibiwa ...unaingia home umechelewa fimbo zimekusubiria ...[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Mkuu umenigusa hahaaa, na wakati huo giza limeingia, inakubidi uokote hovyo hovyo hadi mbichi ilmradi mzigo ujae
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mkuu umenigusa hahaaa, na wakati huo giza limeingia, inakubidi uokote hovyo hovyo hadi mbichi ilmradi mzigo ujae
Ahaaaaaaaaaah mkuuu alafu ubaya kuna kuni home walikuwa hawazipendi wakat ndo zinapatika ...unaweka katikati ili zionekane nyingi
 
Ahaaaaaaaaaah mkuuu alafu ubaya kuna kuni home walikuwa hawazipendi wakat ndo zinapatika ...unaweka katikati ili zionekane nyingi
Hahaaa, kwetu huo mti unaitwa mfufuru mkuu, kuni jikoni inatema maji na moshi tu! Mama hapo lazima akashtaki kwa Mzee na usiombe iwe ni wakati wa mvua za masika hahaaaa
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hahaaa, kwetu huo mti unaitwa mfufuru mkuu, kuni jikoni inatema maji na moshi tu! Mama hapo lazima akashtaki kwa Mzee na usiombe iwe ni wakati wa mvua za masika hahaaaa
Aiseeee kama tulikuwa nyumba mojaa...nimeusahau jina ila kwel ulikuwa unatoaa majii na moshii
 
Nakumbuka tulikua tunachezea barabarani. Kuna kipindi walitandaza moramu tunapochezea.. Tumetoka shule tukakuta moramu, mechi ilichezeka hivihivo tena pekupeku.. Kesho yake kila mtu aliyecheza alikua anachechemea.
 
Duuuuh utoto bana
 
Sisi tulikuwa na sheria chache.
1.faulo pekee hata penati ni kushika
2.mpira ukitoka anaewahi ndio anarusha
3.hamna kona
4.hamna half time
5.giza ndio linaamua mpira uishe
6.mwenye mpira lazima acheze
7.mnyonge ndio kipa
8.hamna jezi,mwendo ni kuvaa au kuvua shati
9.hamna kucheza na viatu
10.anaejua yaani fundi lazima acheze mara nyingi huwa wanaringa sana
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] timu itakayo fungwa gori la kwanza wachezaji watavua mashati kasolo kipa
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom