Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Akivaa kama mwanajeshi anakuwa mwanajeshi? Wanaovaa kanzu wote ni mashehe maana kanzu ni vazi la ibada.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Wewe naye! Nani kakuambia kuwa kanzu ni vazi la ibada, sehemu zenye joto watu huvaa kanzu na waarabu wanavaa kanzu bila kujali dini maana mapadri pia wanavaa kanzu.
 
Wewe naye! Nani kakuambia kuwa kanzu ni vazi la ibada, sehemu zenye joto watu huvaa kanzu na waarabu wanavaa kanzu bila kujali dini maana mapadri pia wanavaa kanzu.
Nilitaka uje hivo. Sasa nikivaa hizo nguo za rangi ya jeshi kama siyo mwanajeshi nakuwa mwanajeshi?

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Watoto wetu wazoeshwe kuvaa mavazi ya kijeshi kama Marekani, ili wakue wakilipenda jeshi na ukati ukifika wajiunge walinde nchi. Makatazi kila kona? A lot of don'ts in this TZ.
 
Tatizo lako shule haipo hapo, wapi nimeuliza swali! Kama unajua elimu yako haikidhi kuwemo kwenye JF of GT's nyamaza, kaa kimya.
 
Wewe kama unaona ni haki yako kuvaa nguo za jeshi vaa kisha pita karibu na kambi yao. Mbona hulilii kuvaa sare za jeshi la zimamoto?
 
Nguo si jeshi, jeshi ni ujuzi anaoupata mtu baada ya kupata mafunzo ya kijeshi.
Sasa hawa wanajeshi wanaogopa raia kuvaa mavazi yenye rangi ya sare zao mbona kama hawajiamini? Siku alshabab wakavaa jeans [emoji158] basi tujiandae kumalizwa maana adui anatambulika kwa kuvaa sare

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Watoto wadogo mwisho miaka 5 nadhani haina madhara lakini kwa wakubwa Big No !!
 
Hawajiamini kabisa. Lkn wanastahili kutojiamini. Si uliona Hamza alivyowapurula polisi? Yaani alikuwa hana bunduki, akawanyang"anya na kuwapurula 9. Sasa unadhani kutakuwa na tofauti sana na hawa wavaa mabaka?
 
Zipo Nchi niliona bunduki zimetundikwa Sokoni panapo uzwa vitu mbali mbali nikauliza hizi bunduki ni vipi mbona zimetundikwa hapo juu nikajibiwa kuwa zinauzwa !!πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Je unaonaje na hapa kwetu tukawaiga wale jamaa wa huko ??!
Panya Rodi tu na mibisibisi yao tunajificha mvunguni je ikiwa vinginevyo itakuwaje ??!!
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Kwanza serikali ipunguze bajeti ya kuandaa na kuajiri wanajeshi maana wapo wanokula mishahara minono wanastaafu mpaka wanakufa hawaeleweki wanafanya nini. Wenyewe wanakuambia Wana kazi nyingi ambazo hazionekani wakati usiku wanalala nyumbani na wake zao kama sisi! Kazi kutesa na kunyanyasa raia. Ngoja nipake nyumba yangu rangi ya jeshi waje waichukue

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Kuna uhusiano gani kati ya sare za jeshi na utapeli?? Hii hoja haina kichwa wala miguu.
Sisi huku bongo tuna asili ya kuwaheshimu walinzi wetu kwahiyo akija mtu mbaya amevaa hizo sare na akaniomba nimsaidie labda usafiri au kitu kingine chochote siwezi kumkatalia kama usafiri au nimuazime kitu ni lazima nitampa kwa sababu nitakuwa nimejiaminisha huyu ni mlinzi wetu na hawezi kuwa ni mtu mbaya. !!

Hivyo ndivyo tunaishi huku kwetu bongo siwezi kuanza kumuuliza mtu vitambulisho vyake ndipo nitoe msaada !!
Kila ndege huruka kwa ubawa wake ulivyo sio kila kitu cha kuiga Mkuu !!! πŸ™
 
Ni bora uahirishe huo mpango πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Lakini kwanini wavae. Hebu fikiria mtu kavaa full uniform kama mjeda au polisi huoni Kwa nchi kama yetu anaweza tumia huo mwanya kutapeli/kunyanyasa watu?
Nyingine zinapatikana katika mabaro ya mitumba, nyingi tu.
Mbaya zaidi mtu kanunua mtumbani halafu anavuliwa hata barabarani! Huu ni hudharirishaji.
 
Polisi wakitangaza hivyo watakamata mno, maana suruali zinazovaliwa nyingi zina rangi ya mavazi ya kipolisi
 
πŸ˜„ 🀣 tembea uone baba
Kuna border ya jirani zetu huko, wale waliuana sana wakatuletea na majambazi ya silaha
Huko unauziwa mpaka AK47 hata rocket launcher ukitaka unabadilishiwa kwa gunia 4 za mahindi πŸ˜„
Halafu nilienda Beirut miaka ya nyuma watoto wanachezea hand grenades
Yaani Dunia ina mambo hii

πŸ‡ΊπŸ‡Έ unaweza kuwa na jeshi la mtu mmoja yaani unanunua tu unaweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…