Sheria ya kumhudumia Mwanamke ifutwe, kwa sasa Ajira zinatolewa kwa Wote bila upendeleo

Ukianzisha familia hayo maswali yatajijibu yenyewe. So kuwa mvumilivu
Na hapa unaona umeleta jibu linaloendana na mada yako uliyoleta hapa...., Nilidhani naongea na mtu mwenye Busara na anayeongelea hoja kumbe nimekosea njia na kukutana na vioja....
 
Na hapa unaona umeleta jibu linaloendana na mada yako uliyoleta hapa...., Nilidhani naongea na mtu mwenye Busara na anayeongelea hoja kumbe nimekosea njia na kukutana na vioja....

Nimejibu maswali yako yote kwa njia rahisi ambayo wengine pia waliotaka kuuliza (kama hawajui) watapata majibu kupitia wao wenyewe
 
Nimejibu maswali yako yote kwa njia rahisi ambayo wengine pia waliotaka kuuliza (kama hawajui) watapata majibu kupitia wao wenyewe
Kwa kufanya hivyo ume-assume kwamba wewe ndio unajua ukweli wakati huo ni mtizamo wako.., Sasa ungejibu Swali uliloulizwa tungeweza kufanya dissection na kuona kama mtizamo wako una mashiko..., Umeongelea Sheria; Sasa ili tuweze kuongelea hizo so called Sheria lazima tufahamu kama tunaongelea kitu kile kile (au wewe unachokiita Sheria wala sio Sheria) au Unachokisema ni Kitu ambacho ni Muongozo wa watu wa Jamii / Imani fulani ambacho hakiwezi kubadilishwa hence your assertion being Void ab Initio...
 

Jibu nililokupa ndio jibu bora ambalo limejibu maswali yako mengine ikiwemo hii comment.

Unaniuliza maswali ya kitoto utegemee nitakujibu kama mtoto? Mimi sio mtoto Mkuu.
Hilo swali kaulize wanafunzi wa chuo au sekondari. Ili wakupe majibu yanayolingana na uwezo wako wa kuuliza maswali
 
Am Wisest Man Alive.. for I know One thing and that is I Know Nothing..., Unadhani unajua wala kumbe hujui hata unachokiongea.., Ni sawasawa unaita Pipa Kikombe unaulizwa pipa ni nini ili kuongelea hilo Pipa lako alafu unaleta story kwamba wewe sio mtoto... Kwahio Hii mada imekuja na Parental Control au Elimu fulani kwamba ukiwa haujamaliza Chuo wala Sekondari huwezi kujadili...

Yaani kwa busara zako sasa hivi tunaongelea utoto wangu na sio mada uliyoleta hapo mwanzo ?, Hii kwa ufupi inaitwa Hubris.... and we that one can never grow....
 

Swali ulilouliza ndio la kitoto na mimi nimekujibu Kikubwa. Sasa huo utoto wako mimi siujui kama unao au laa. Nilichoeleza ni kile ulichouliza.

Nakusaidia tena, Kama unakazi na umeajiriwa basi utajua maana ya sheria ni nini. Au kama umeajiri mtu huwezi kushindwa kujua maana ya sheria.

Huwezi niuliza swali la kitoto alafu utegemee nitakujibu utakavyo kama mtoto. Wanafunzi wa chuo au sekondari ndio maswali yao hayo. Mimi nilishakimbia shule miaka mingi sasa
 
Naunga mkono hoja
 
Taarifa:

Sasa hivi familia nyingi zinahudumiwa na wanawake huku mchango wa baba ukiwa mdogo.

Wenye hela kwa sasa ni wanawake.

Kwa hiyo hata sheria isipobadilika, tayari utekelezaji ulishazoeleka
Labda ww mariooo
 
Ulicho ongea kina make sense, lakini mkeo ana pesa na ww una pesa kwa nn zote zisiwe zenu ila tu huyo mwanaume ndo awe anatoa za kwake? To conclude hiyo sio ndoa ilisha jifia mapema sana.
 
Unafikiri mzee Ameir anaweza kumuhudumia mama yetu kwa kila kitu?
 
😀😀😀
 
Mwanamke kama hasaidii kazi za nyumba zile za kike anatakiwa asaidie kwenye kazi anayofanya maana wote tumeoana tunatumia muda wa familia.Mwanamke hawezi tumia muda wa familia alafu asilete faida.Kama anatumia muda wa familia Bure BIla faida yoyote ni Bora abaki nyumbani atumie muda wa familia kulea familia.
 

Hiyo ndio maana ya ndoa
 
Mimi kama tunachangia Hela nusu kwa nusu kwenye kila kitu sikufulii sikupikii sijui kukuandaa kazini Wala sikuombi ruhusa ya kitu chochote sifa Yako kama mwanaume umeshapoteza mwanaume anatakiwa atoe zaidi hiyo ni nature
Assume wewe ndio spika Tulia mshahara milioni 20 na mume wako mwalimu mshahara laki 5. Hapo utafanyaje?
 
Tafiti zangu mm The only mpaka sasa wanawake waliochaangia ni 0 ila wana view wanapita hivi.natabiri hadi uzi unaisha watachangia 6 tu nao kujifanya mume ndo kichwa .asante
 
Assume wewe ndio spika Tulia mshahara milioni 20 na mume wako mwalimu mshahara laki 5. Hapo utafanyaje?
Unaacha kazi tulia anakukopea mil 300 unafungua kiwanda cha juice mapato yako kwa mwezi yna anakuwa mil 20 pia siku akiacha uspika anarudi kuwa ceo kiwandan wewe unahamia shamba lenu kubwa la maembe ambalo yote huwa yanakuja zalishwa juice kiwandani kwenu .
Na kila mwezi kama anakatwa rejesho la mil 7 basi unamuingizia aendelee kula ile ile mil 20
 
Kwa akili ya mwanamke hawezi kumkopea mwanaume pesa mil. 300
"Khaa, nimkopee mil 300 akatumie kwa michepuko wake!"
 
Kuna vitu vipo wide na unaweza wewe tafsiri yako binafsi ikawa tofauti na tafsiri ya mtu mwingine; hence mtu anapokuuliza wewe kwa muktadha wako kwenye context hii unamaanisha nini ili tuwe kwenye same page na kuweza kujadili kilichopo kwenye hio page..., Sasa hapa kwenye hii paragraph umetoa issue za mimi kuajiri / kuajiriwa na kujua Sheria..., Inawezekana nimeajiriwa katika Msikiti hence kwangu mimi Mwanaume ndio kichwa hata iweje lazima nitoe huduma (hio ipo kwenye Imani wala siwezi kuibadilisha)....

Sasa sababu haujajibu nina-assume unamaanisha Sheria ambayo iwe sheria lazima iwe na penalty kwa mtu kuivunja kutokana na Misingi watu waliyojiwekea.., au niende further unamaanisha Kifungu Na. 63 cha Sheria ya Ndoa...... Kwa Maneno yasiyo Rasmi.....
Now kama hicho ndicho unachomaanisha..., suala ni kwamba kila case inaweza ikatatuliwa kutokana na mazingira yake..., sidhani kama Samia anaweza kumshitaki mume wake eti hajamnunulia Nyumba, au Kumpa Chakula (sababu hana uhaba huo)..., LAKINI mfano keshokutwa SAMIA (kwa kutokutumia IMANI yao bali Sheria za Nchi) akiamua kudai Talaka yake anaweza kusema huyu Bwana hatoi Huduma yoyote hivyo mimi kuendelea kuwa mke wake na kunizibia opportunity za kuwa na Bwana mwingine wakati yeye hatimizi / hachangii wellbeing yangu kwa lolote nataka uhuru wangu na aniache... Kwahio hapo atakuwa ana point... KULIKO kufuta hiki kipengele huenda ikatokea watu kuoa mtaa mzima (hence kuwazibia uhuru wao kwamba ni wake zao) wakati hawachangii lolote kwa kumfunga huyu so called mke...

Issue ya kukopa kwa Dhamana ya Mume: Sheria hii imewekwa kutokana na hii scenario
jukumu la kutunza mke na watoto ni jukumu la mume au baba. Kwa msingi huo, endapo baba amesafiri, au ametoroka na baadaye matatizo yakajitokeza yanayohitaji fedha, basi mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mume au kuweka rehani mali ya mumewe.
Sasa mfano watoto wanataka kwenda shule na mume ametoroka (kweli mama asiweke rehani gari aliloacha mume wake hapo kwenye garage)? lakini nina uhakika kama huyu Mama (SAMIA) atafanya hivyo kwa kuuza nyumba ya mume wake ili anunue lipstick Mahakama haiwezi kusema ni sawa kilichofanyika...; Ingawa akisema huyu Bwana hana mchango wowote kila mtu achukue hamsini zake anaweza kuweka kigezo cha kutokumuhudumia kama sababu ya kuachana nae....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…