Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Mkuu huyu jamaa yupo Dar, anasema hana mbele wala nyuma Dar to Tarime si chini ya 80k hapo hajafika Mwakitoryo, nafikiri ungemsaidia namna ya kufika huko ilipo kazi ingekuwa vizuri.
 
Mi nakupa mbinu nzuri sana na urudi kunishukuru.

Kwanza chukua kadi ya CHADEMA, kaanayo kisha baada ya muda Nenda Lumumba kaanze namna ya kuwadanganya umechoshwa na CHADEMA unataka kuhama.

Baada ya muda fuatilia vikao vyao, siku kuna mtawala mkubwa jichanganye na wale wanaounga juhudi.

Watakuuliza umesoma wapi, una elimu, gani na baada ya hapo watakupa Mofia, tisheti la Kijani na utapewa kadi.

Hapo sasa ndio kamata mpaka upate pande lako, Unaweza kabidhiwa kwa liz1 au Koleo Katambi, akaambiwa mpe kazi huyo.

Utakuwa umemaliza shida za tumbo lako.

Watafute CHADEMA waliohamia upande wa pili wakupe michongo namna ya kutoboa.

Vijana msikae kijinga, changamsheni akili.
 
Kweli mkuu! Mtu ambaye hajapitia haya ni ngumu kuelewa.

Lakini mpk tunafikia hatua ya kuweka wazi, ujue Hali ni ngumu! Lakini ashukuriwe Mungu, watu kama nyie mnanitia moyo.

Hamjui tu nguvu kiasi Gani mnanipa
Sarah K - Usiyeshindwa

Hakika amini kwa magumu yote upitiayo yupo MUNGU asiyeshindwa atafanya njia endelea kuamini njia zake na kamwe usifikirie kuiacha njia yake hata kama huuoni mlango.
 
Mimi nikupe ushauri kama una 20000 au 25000 huo ni mtaji nenda mabibo sokoni chukua ndizi mbichi ingia mtaani tembeza .

Au nenda stirio sokoni chukua bamia ,nyanya chungu weka kwenye mfuko ingia mtaani tembeza baada ya masaa kadhaa haukosi buku ten faida


Nenda pale kigogo sambusa kuna soko la njegere na mbaazi utakutana na vijana wa kiruguru hapo mnachanga hata wawili mnanunua gunia la njegere mnagawana unaingia mtaani kutembeza nenda mitaa ya mbagala huko unapata pesa.

Au nenda karume mida ya saa tisa usiku chukua viatu vya mitumba vikali osha vibrashi vizuri ingia mtaani kwenye mabaa hautokosa wateja.

Kwenye maisha haya usikate tamaa tabu zipo na hazitodumu milele.

Dar kila kitu kinauzika tena uswahilini ndio kuna hela. Usione aibu wewe jichanganye .

Mwandishi mmoja aliwahi kuandika hivi." Machozi ya mwanaume hayanathamani nimwanamke pekee ndiye akilia anaweza kubembelezwa." (BEN R MTOBWA) Katika kitabu cha "DARES SALAAM USIKU"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…