Shida ya Lissu na Nyerere ni nini hasa?

Shida ya Lissu na Nyerere ni nini hasa?

Mimi sikuwepo enzi za mwalimu ila kwa simulizi mbalimbali zilizopo ni kwamba hiyo awamu yake ilikuwa sio poa. Ndo nyakati wananchi walikuwa wakisema "zidumu fikra za mwenyekiti".. kwangu mimi kikubwa alichofanya mwalimu ni kutokomeza ukabila. Ila mambo mengi yalikuwa hovyo.

..hizi habari kwamba Mwalimu alitokomeza ukabila sio za kweli. Hakukuwahi kuwa na uhasama wa kikabila.
 
..Lissu alikuwa akijibu swali la Chief Odemba.

..Na katika jibu lake alisema mabadiliko ya katiba ya mwaka 1962 ndio yaliyotuletea Raisi mwenye mabavu kupita kiasi, ya ki-mungu-mtu.

..sasa Raisi wa kwanza kuwa na madaraka yaliyopitiliza alikuwa Mwalimu Nyerere.

..Kwa msingi huo, hoja ya Lissu ina utetezi na ushahidi wa kihistoria.
Mwalimu kwa kauli zake alikiri kwamba ''katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa na hata kuwa dikteta''

Pili, Tundu yupo sahihi kueleza jinsi '' Haki za binadamu' zilivyopigwa dana dana kwa hoja ya maendeleo kwanza.
Dana dana kama hizi za katiba isubiri tujenge uchumi.

Tatu, Mwl hana ''immunity' ya kukosolewa. Kwa mfano mpango wa elimu ya msingi ulivurugwa na ''UPE'' pale aliyefeli darasa la 7 alikuwa Mwalimu. Huo ulikuwa mwanzo wa matatizo mengi katika elimu ya leo.
 
Naona mtu anaemuogopa ni Mwinyi na Kikwete tu. Bado haijamtokea kwao.

Alimshambulia sana Nyerere wakati wa mjadala wa bunge la Katiba.
Nyerere ni kiongozi wa kwanza wa Taifa huru. Sera zake zilikuwa na athari mbili
1. Sera nzuri zilijenga Taifa na tunaishi nazo. 2. Sera mbaya zilibomoa Taifa tunaishi nazo

Mfano, katika huduma za jamii kama elimu na afya Mwl alijitahidi sana kwa kuangalia uchanga wa Taifa
Alisomesha watu na kuanzisha vyuo vilivyokuwa na hadhi na heshima kuanzia Cert hadi degree.

Ubaya wa sera ni kama ule wa mwaka 1974 wa elimu ya UPE ambao madhara yake yamedumu sana
Ni kuua vyama vya ushirika kwa hofu tu

Mwinyi hakuwa na sera, alichokifanya ni 'trade liberalization' iliyoficha udhaifu wa '' grand corruption'
Pia kuanzisha vyama vingi kulifunika madhaifu yake. Hakuna mengi ya kumuongelea.

Mkapa hakuwa na sera, alipita kule kwa Mwinyi.
Vugu vugu la vyama vingi likaficha udhaifu kama wa mwinyi kuhusu ''corruption', na amekiri katika kitabu chake.

Kikwete hakuwa na sera zaidi ya kufanya kila kitu kiholela.
Uanzishwaji wa vyuo vikuu kila kijiji bila kuzingatia sifa na zao lake. Tukawa na vyuo vikuu , maprofesa ni Graduate! Kufanya kila Hospitali iwe ya rufaa bila wataalamu na vifaa ni zao la Kikwete.
Kibaya zaidi kushindwa kusimamia mchakato wa katiba.

JPM hana sera lakini ameacha makovu makubwa na nyufa nyingi katika Taifa. In short hafai kuzungumzia.

Ni sahihi Nyerere kushambuliwa au kusifiwa kwasababu alikuwa na sera na dira! tunazoziona na kuzichambua.

JokaKuu
 
Wewe umeona rais gani aliyefuata anayejielewa?
Basi wasiojielewa ni nyie raia mliochagua marais wasiojielewa kwa miaka 40. Mtu mwenye kujielewa hawezi kuchagua kichaa na kumuona kuwa ndiye anayejielewa!
 
Ukimpatia Lissu saa moja atatumia dk 45 kumdiss Mwalimu Nyerere kwa maneno makali kadri atakavyoweza.

Alipoulizwa na Chief Odemba kwa maoni yake kuwa ipi ilikuwa awamu iliyoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, bila kumumunya maneno alidai ni awamu ya kwanza.

Kwa mtazamo wa Lissu, Nyerere alikuwa katili kuliko Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM wote kwa pamoja.

Lisu ni msomi mpumbavu sana anadhani watu wengine wote ni wapumbavu pia na hivyo yeye yuko juu yao.
 
Lissu ni janga kwa wapinzani. Hana kekima, mropokaji, mtoa mapovu utafikiri ni pacha na Mwakubusi! Sasa huyu apewe nchi kuiongoza itaenda wapi? Khaaaaa!
 
Lisu ni msomi mpumbavu sana anadhani watu wengine wote ni wapumbavu pia na hivyo yeye yuko juu yao.

..Lissu aliulizwa kuhusu madaraka makubwa ya kikatiba ya Raisi wa Tanzania.

..Katika kujibu akasema madaraka hayo chanzo chake ni mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika mwaka 1962.

..Na akasema madaraka hayo yalianza na Mwalimu Nyerere mwaka 1962 na yamekuwepo mpaka leo.

..Chief Odemba akauliza kati ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, na Samia, ni yupi alitumia madaraka hayo vilivyo?

..Jibu la Lissu lilikuwa kwamba mazingira wakati wa Mwalimu yalikuwa tofauti kwasababu wakati wake hakukuwa na vyama vya upinzani.

..Kwa ujumla Lissu alikuwa anajibu swali aliloulizwa, na majibu yake yana ushahidi wa kihistoria. Mtu yeyote mwenye uelewa wa historia na katiba angejibu kama alivyojibu Lissu.
 
Acha mambo ya kitoto kamarada Glenn....

Kama si Nyerere nchi hii ingejaa UDINI....

Kama si Nyerere nchi hii ingefurika UKABILA NA UKANDA.....

Hivi lini vijana sisi tutajifunza thamani kuu ya Nyerere ?!!

Havoc
Udini upo sana,ukabila upo sana,unaishi wapi wewe
 
If yes ,Tanzania will never ever have the best president....

Nyerere was the beacon against racism ,bigotry and religious hatred , otherwise this nation would never be the way it is.....

Without his presidency this country would be vandalized into ashes through evil ideologies of tribalism and religious terrorism....

#Never give wisdom to unworthy as it is unjust to the knowledgeables [emoji7]
Umelishwa matango pori ukayameza kama yalivyo brainwash
 
But I would say he was more close to a saint considering the epoch in which he ruled.Who expects any human being to be a saint; not even one's parents can qualify to sainthood. Again, look around in the neigborhood or around the world for that matter, at the time; where can one find a saint national leader?

It would have been more beneficial for those who have no access to the book if you had cited a few examples. to highlight what was happening during his time..
Kama unafanya mlinganisho wa Nyerere na watawala wengine kwa hisia za kawaida za kibinadamu unaweza kumuona “mtakatifu”. Na usishangae wakiwepo watu ambao nao wanaowaona AHM, BM, JK, JPM na SSH hivyo hivyo.

Utakatifu si sifa ya binadamu; ni ya Mungu na mitume wake. Na yeyote asiye mtakatifu anapaswa “critical analysis” kuonyesha hali zake zote za kibinadamu. Kwa yote aliyofanya, mema na mabaya, Nyerere alikuwa na hulka zote za kibinadamu: mbaya na nzuri.

Wale wasiotaka kabisa kusikia hulka mbaya za Nyerere hawawezi kumuelewa mtu anayezizungumzia. Ndivyo ilivyo kote. Leo hii, kwa mfano, ubaya wa JPM ukigusiwa tu, kuna watu wanahamaki kweli kweli. It’s bizarre! Viongozi si wa kuabudiwa. Lazima wachambuliwe pande zao zote.

China leo hata Mao anapigwa critique ya uhakika. Wamefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii baada ya kusahihisha makosa makubwa ya Mao.

Kitabu hicho: Remembering Nyerere in Tanzania kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers na kinapatikana online pia. Kina mkusanyiko wa maandiko kadhaa ya wadau mbalimbali kumhusu Nyerere tangu enzi za mkoloni hadi mwisho wake.
 
Ukimpatia Lissu saa moja atatumia dk 45 kumdiss Mwalimu Nyerere kwa maneno makali kadri atakavyoweza.

Alipoulizwa na Chief Odemba kwa maoni yake kuwa ipi ilikuwa awamu iliyoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, bila kumumunya maneno alidai ni awamu ya kwanza.

Kwa mtazamo wa Lissu, Nyerere alikuwa katili kuliko Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM wote kwa pamoja.

Nyerere nae, aliumiza watu Sana, na ndio alietengeneneza huu mfumo wa ccm wa kijambazi, unaotuumiza mpaka Leo,
Ye ye kwa wakati wake, kutoka na na changamoto za kidunia, za, usalama,ulikuwa unafaa,ila ilibidi ufe miaka 28 iliyopita, kuendelea kuwa na mfumo wa kipuuzi kama huu, haifai,
Ndio maana, unaona binti anabakwa, wabakaji wanajirekodi, polisi baada ya kushitqki wabakaji, wanaeleza jinsi mbakwaji alivyokuwa na tabia mbovu ya kujiuza!
 
Mbongo akifanyiwa hisani huwa haoni mbaya ya yule aliemfanyia hisani, atamsafisha kwa namna yoyote hata awe mchafu kama shimo la choo..

Hapo juu naona watu wamekomalia ati kama sio Nyerere basi Lisu asingesoma mpaka kufikia hapo.
Hata kama hiyo iwe ni kweli bado haitaondoa ubaya wa Nyerere kama upo. Hata angekua yeye ndo anamlipia ada hiyo haifuti mabaya yake kwa watu wengine, na yakisemwa usiyapinge kwa kusema ati alikusaidia kwanini unamsema vibaya.
 
Acha mambo ya kitoto kamarada Glenn....

Kama si Nyerere nchi hii ingejaa UDINI....

Kama si Nyerere nchi hii ingefurika UKABILA NA UKANDA.....

Hivi lini vijana sisi tutajifunza thamani kuu ya Nyerere ?!!

Havoc
kwa hiyo ni bora kunywa sumu inayoua taratibu kuliko kufa njaa
 
Tatizo mmelishwa matango pori..
Nyerere ndiye rais mbovu aliyejenga misingi mibovu sana ya nchi hii.
1. Ujinga mtopeo..ni yeye chanzo
2. Unafiki wa Tz ni yeye chanzo
3. Nidhamu ya uoga ni yeye chanzo
4. Nchi kuwa omba omba yeye chanzo
5. Umaskini ni yeye chanzo
Mbili na tatu nakubaliana na wewe, mengine hapana
 
Mbongo akifanyiwa hisani huwa haoni mbaya ya yule aliemfanyia hisani, atamsafisha kwa namna yoyote hata awe mchafu kama shimo la choo..

Hapo juu naona watu wamekomalia ati kama sio Nyerere basi Lisu asingesoma mpaka kufikia hapo.
Hata kama hiyo iwe ni kweli bado haitaondoa ubaya wa Nyerere kama upo. Hata angekua yeye ndo anamlipia ada hiyo haifuti mabaya yake kwa watu wengine, na yakisemwa usiyapinge kwa kusema ati alikusaidia kwanini unamsema vibaya.
Hii ni kweli, na msaada wenyewe unakuwa wa mkakati wa kupata kitu, ni aina ya rushwa ambayo tumeibariki mpaka imekuwa institution
 
Ukimpatia Lissu saa moja atatumia dk 45 kumdiss Mwalimu Nyerere kwa maneno makali kadri atakavyoweza.

Alipoulizwa na Chief Odemba kwa maoni yake kuwa ipi ilikuwa awamu iliyoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, bila kumumunya maneno alidai ni awamu ya kwanza.

Kwa mtazamo wa Lissu, Nyerere alikuwa katili kuliko Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM wote kwa pamoja.

Lissu will die one day a frustrated man but not as a former president of Tanzania.

Nahakikisha Tundu hawezi kuwa Rais. Wanaopata uRais wa Tanzania siyo wa haiba kama ya kwake au wanaopania kwa udi na uvumba kuwa maRais wa Tz.

Yeye amepewa nafasi ya pili ya kuishi baada ya Magufuli na Makonda kutaka kumuua, amshukuru Mungu tu. Ila Urais kwake ni maji marefu
 
Yule mzee alikuwa mroho wa madaraka, miaka yote ile hakukuwa na mtu mwingine wa kuwa rais?
 
uongozi siyo lele mama,lissu anaona uongozi ni kusoma kwenye vitabu wkt ni zaidi ya hapo.
 
Back
Top Bottom