Naona mtu anaemuogopa ni Mwinyi na Kikwete tu. Bado haijamtokea kwao.
Alimshambulia sana Nyerere wakati wa mjadala wa bunge la Katiba.
Nyerere ni kiongozi wa kwanza wa Taifa huru. Sera zake zilikuwa na athari mbili
1. Sera nzuri zilijenga Taifa na tunaishi nazo. 2. Sera mbaya zilibomoa Taifa tunaishi nazo
Mfano, katika huduma za jamii kama elimu na afya Mwl alijitahidi sana kwa kuangalia uchanga wa Taifa
Alisomesha watu na kuanzisha vyuo vilivyokuwa na hadhi na heshima kuanzia Cert hadi degree.
Ubaya wa sera ni kama ule wa mwaka 1974 wa elimu ya UPE ambao madhara yake yamedumu sana
Ni kuua vyama vya ushirika kwa hofu tu
Mwinyi hakuwa na sera, alichokifanya ni 'trade liberalization' iliyoficha udhaifu wa '' grand corruption'
Pia kuanzisha vyama vingi kulifunika madhaifu yake. Hakuna mengi ya kumuongelea.
Mkapa hakuwa na sera, alipita kule kwa Mwinyi.
Vugu vugu la vyama vingi likaficha udhaifu kama wa mwinyi kuhusu ''corruption', na amekiri katika kitabu chake.
Kikwete hakuwa na sera zaidi ya kufanya kila kitu kiholela.
Uanzishwaji wa vyuo vikuu kila kijiji bila kuzingatia sifa na zao lake. Tukawa na vyuo vikuu , maprofesa ni Graduate! Kufanya kila Hospitali iwe ya rufaa bila wataalamu na vifaa ni zao la Kikwete.
Kibaya zaidi kushindwa kusimamia mchakato wa katiba.
JPM hana sera lakini ameacha makovu makubwa na nyufa nyingi katika Taifa. In short hafai kuzungumzia.
Ni sahihi Nyerere kushambuliwa au kusifiwa kwasababu alikuwa na sera na dira! tunazoziona na kuzichambua.
JokaKuu